Waziri Makamba ujue siyo kila kitu ni cha kubinafisisha

mkuu Sijamsikia makamba akisema shirika libinafisishwe,wewe umetoa wapi hii taarifa
 
Unabinafisaji uendeshaji maana mswahili hawezi akaendesha kitu kwa ufanisi na ishu ya security inabakia kwenye serikali kwa national security.
Check tu mfano Tazara wameshindwa japo market ni kubwa na ya uhakika.
Anayebinafsishwa sharti asiwe mswahili ?
 
Turuhusu tuu watu/makampuni binafsi yazalishe na kusambaza umeme, soko huru kama makampuni ya simu, TANESCO shirika linaloishi kwa ruzuku na kuendeshwa kijima haliwezi kuhudumia watu milioni 70, sheria zetu za kuipa TANESCO monopoly ndio zinatuumiza, tubadilishe sheria matatizo ya umeme yataisha
 
Wanasiasa hawawezi chezea shirika binafsi
 
Ubinafsishaji huongeza tija na ufanisi, wala hatuna haja ya kutia shaka kuhusu suala hilo.
 
Wapi alipotangaza anataka TANESCO ibinafsishwe? Au chuki zako tu.
Tangu lini wakitaka kubinafsisha hutangaza. Majanuary anataka kukaa mkao wa kula. Miaka yote ubinafsishaji umekuwa ndiyo njia pekee ya kuwapelekea wakubwa kuwa mamilionea/mabilionea/matirilionea. Majanuary anataka wahi, mkishtushtuka atakuwa tayari kafunga bao na kukimbilia USA.
 
Chuki zitakuua.
fanya kazi uwajengee maisha bora wanao ili nao wawe kama familia ya Makamba wasigeuke wapiga stori za vijiweni.
 
Chuki zitakuua.
fanya kazi uwajengee maisha bora wanao ili nao wawe kama familia ya Makamba wasigeuke wapiga stori za vijiweni.
Labda wewe, mimi kila kitu kwenye maisha yangu kiko sawa. Nina chakula cha kutosha, ninavaa vizuri, nina kibanda cha kulala na sina matamanio mengine, na pia sikufika nilipo kwa njia haramu. Kazi ya chaki ndiyo imenifikisha nilipo.
 
Reactions: Ame
Chuki zitakuua.
fanya kazi uwajengee maisha bora wanao ili nao wawe kama familia ya Makamba wasigeuke wapiga stori za vijiweni.
Mkuu unafikili basi nao familia zao ziko njema kihivyo asilimia 100,nenda kakague miji yao wanayotokea barabara na nyumba zinazowazunguka ni mbovu kuliko mfano,watumishi wa uma huko wanakotoka wanatamani kuhama kila siku maana hakuna hata motisha.kifupi hawa viongozi wanasiasa vijana ni walafi wa mali ya uma na wakati huo huo wana choyo hata kwa maendeleo ya kaya zao.
Wanafisadi fedha za miradi alafu wanazikimbiza nje huko kwa wazungu wakifa ndio zimeishia huko huko.

Magu kawapa somo ndani ya miaka 6 kaacha alama kubwa kule Chato hakuna taasisi ya kiserikali imekaa kiholelaholela.
 
Ivi waziri yupo siliazi au?
 
Ni lini ametamka kubinafsisha?

Na kama kweli anataka kubinafsisha ujue ndio anaanza kuiba pesa kwa kula rushwa za wawekezaji na kuingia mikataba ya kula pesa

Huyu na Nape Nnauye pamoja na Ridhiwani ni wa kuwa nao makini sana
 
Watu wamerukia kumshutumu JM bila hata kujiridhisha kuwa kayasema hayo mambo ya ubinafsishaji.

Mtoa mada athibitishe kwanza kuwa JM anataka kubinafsisha Tanesco la sivyo ni chuki binafsi.

Kwanza Tanesco haiwezi kubinafsishwa bila ridhaa ya rais, baraza la mawaziri na bunge. Tanesco ikibinafsishwa hao wote hawawezi kukimbia hilo jukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…