Magu ndio kipimo? Alimpiga pembeni kwa sababu alitaka aweke ndugu yake wa kusema uongo na kuiba nothing else.
Kwani Vijijini kuingiza umeme Kwa 27,000 kumeisha? Wewe ndio una bibi peke yako? 😁😁.
Ukweli mchungu ni kwamba mwendazake hakufanya repair ndiovyo Tanesco wamesema.
Boss,
Uchumi umeongezeka maana yake matumizi ya umeme yame ongezeka, kama wateja wame ongezeka maana yake mitambo yetu inatakiwa iongezewe capacity kukidhi ongezeko la watumiaji, kama kweli ni hivyo basi Tanesco wana takiwa ku upgrade mitambo Yao ya awali Kwa kuiongezea uwezo zaidi na kupanua njia za usafirishaji, hii ni kuangalia tufanye nini katika mitambo yetu ya sasa kuongeza uzalishaji sio ku repair , repair haiongezi uzalishaji wa umeme na haina uhusiano na uchumi.
Pili kama mitambo haiwezi kuwa upgraded na Kuna capacity limitations kifuatacho ni kufanya nini expansion, expanding uzalishaji wa umeme Kwa kujenga vituo vipya vikubwa au vidogo kwa haraka Kwa matumizi ya sasa na miaka ijayo kadri ya ongezeko la mahitaji,sasa new build takes time, inahitaji pesa lakini ni solutions ya kudumu zaidi kuliko njia zingine, ndio maana Kuna ujenzi wa kinyerezi 1,2,3,4 na kuendelea, ndio maana Kuna stieglers, Kuna solar energy, makaa ya mawe na etc.
Repair ni aibu hata kusema kuwa wakirepair uzalishaji utaongezeka, ni aibu kubwa Kwa Tanesco na waziri kutoa taarifa ambayo hawajui maana yake nini, chukua mfano, una daladala yenye abiria 10, lakini unapofika kituoni una kuta Kuna abiria 20, hivyo una beba abilia wako 10 na wengine kuwaacha, so ukitaka kuwabeba abiria wote utapeleka gari lako likafanyiwe repair ? Jibu ni no, Bali utafanya yafuatayo;
1. Expansions Kwa kuongeza seat ya abiria kama gari lina nafasi, kama halina una weza hata fumua bodi ukaongeza ili upate nafasi.
2. Baada ya kuongeza nafasi, fumua bodi,je engine uwezo wake utafaa? Kama engine capacity ni kidogo una upgrade.
3. Suluhisho la kudumu ni kununua daladala ya pili iweze kubeba hao abiria wengine (new build).
Matengenezo hayaongezi uzalishaji na kukidhi mahitaji ya umeme hapo Tanesco wana paka ragi upepo, hakuna jitihada wanazifanya zaidi ya kutokili kuwa wamefail na wana mshauri vibaya waziri, makamba sio mtalaamu wa umeme na hajui anacho ongea, yeye anatakiwa awabane Tanesco waache kutoa sababu za uongo Bali wajikite kutafuta njia mbadala na kuondokana na tatizo hilo,waache kukaa ofsini wakisubiri tatizo ,
Tanesco nadhani utendaji ni mbovu watu wanafanya kazi Kwa mazoea.