Waziri Makamba, Uteuzi wako wa Mama Maajar kuwa mjumbe wa bodi ya TANESCO una mgongano wa maslahi

Utaratibu ni kwamba Wakati wa kuunda Bodi Waziri anapeleka majina yasiyopungua matatu kwa nafasi ya Mwenyekiti na Majina ya Wanaopendekezwa kuwa Wajumbe wa Bodi
Wote hao wanafanyiwa Vetting
Baada ya hapo Rais anateua mwenyekiti kutoka hao watatu au anakataa wote na kuteua anayeona anafaa
Majina ya Wajumbe yakipitishwa baada ya Vetting yanarudishwa kwa Waziri kuyatangaza pamoja na jina la Mwenyekiti aliyeteuliwa

So kama kuna tatizo lingeonekana wakati wa vetting

naomba kuwakilisha
 
Tena maslahi ya moja kwa moja kwa gharama za nchi na bado anaaminiwa sijui ni kwa sababu zipi za maana.

Bunge lina wabunge zaidi ya 300+ lakini wameletwa watu wale wale wa miaka yote waliowahi kuhusishwa na kashifa za aibu ni Mungu tu ndiye anaweza kupindua meza vinginevyo ukoo wa wakora umeingia jikoni kujipakulia chakula pamoja na akiba ya miaka mingi mbeleni
 

Hata waziri naye ni sehemu ya vetting. Kufeli kwa vetting siyo excuse kwa mtu mwenye mamlaka ya maamuzi kuteua vimeo au watu wasiostahili
 
Mkuu acha kabisa kuongea hivyo,kama hana influence wangeliachwa wale wa zamani. Impackt ipo tena kubwa tu.
Tafuteni vijana wapya si tunajidai tunawasomi wabobezi.
Shida wasomi na wenye akili hamwataki wanaenda Upinzani ndo maana JPM aliamua kuwachukua akina Silinde na kuwapa uwaziri maana hawa jamaa ni akili kubwa same kwa mawakili, wale wa serikali huwa wanastrugle sana kushinda kesi.
Ndo maana hawajawahi kumshinda Lissu hata kesi moja na upinzani kwa ujumla tu huwa naumia sana. Kuona wanaotuongoza wanashindwa na waongozwa sa Sad.
 
Watanzania mna vituko!!!...Tuache siasa kwenye Mambo ya Msingi!!..Mama Maajar ni Mtu makini sana kwenye Kazi na atatupeleka mbali kwenye sekta hii ya Umeme!!
Kama ni makini kwa nini alishauri Tanesco kuvunja mkataba na dowans ilihali anajua italeta impact mbaya kwa Shirika?
 
Eti tatizo lingelionekana,kwa hao wanaoteua nakupangua hata kabla mtu hajala kiapo anatenguliwa.
Mafano mzuri Mkurugenzi wa TPDC.
 
'The worst employees are always considered for promotion'
 
ukisikia msoga jazzy band returning in the system ndo hii tujiandae kusikia akina lugemalila walikua sawakwakila kitu
 
January ni mtu mwadilifu sana
Ebu fafanua uadilifu sana huo wa January kwa kuhusisha na haya mambo matatu:
1.Tuhuma dhidi yake kuhusu wizi wa Mitihani kule Galanosi
2.Tuhuma za Utapeli wa bilioni 2 yeye na dada yake Mwamvita dhidi ya Mtaliano aliyekuwa mpenzi/boyfriend wa dada yake.
3.Tuhuma dhidi yake ya kuwatumia wanachama hewa wa SACCOS yake kukwapua bilioni 2 NSSF na kushindwa kulipa mkopo!
Kuna tuhuma za "Unga" dhidi ya Dada yake Mwamvita ( hilo tuliache kwanza).
 
Mfalme Nebukadineza wa Babel alipomkosea Mungu kama mtawala Mungu alimpeleka porini ambako aliishi Kwa Kula nyasi na kutembea kama ng`ombe. Hivyo Mungu huwaadhibu watawala wasiotenda haki kwa wakati wake.
 
Tatizo la Makamba ni kuwa it seems anatengeneza timu yake ya uchaguzi wa rais after 2030.
This behaviour will not work well for him!
 
Kama ni makini kwa nini alishauri Tanesco kuvunja mkataba na dowans ilihali anajua italeta impact mbaya kwa Shirika?
Nadhani hukua unajua kwanini lazima Shirika Ilitakiwa ivunje mkataba!!.. Anyway unajua Dowans ndio ilikua Richmond au hujui?
 
Waziri Makamba Nakuomba kwa heshima na taadhima fuatilia tuhuma za tanesco mkulanga yule meneja wa pale a nakula rushwa yeye pamoja na baadhi ya watendaji, tume peleka malalamiko na amekua hayafanyii kazi tunajua kwamba uteuzi huu wa bodi ya wakurugenzi wa tanesco lengo ni kubolesha utendaji wa shirika la Tanesco kama hautoshughurikia hili basi uwepo wa bodi hii utakuwa hauna tija yeyote kwa wananchi na shirika la Tanesco kwa ujumla.
 
Kweli kijana ameandaliwa kwa jambo la hovyo siku za usoni
 
Muongezee kuwa alimpiga Muitaliano akishirikiana na Sista
 
Hoja namba 1 uliona mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…