Waziri Masauni afanya Ziara ya Kikazi Wilayani Kilosa

Waziri Masauni afanya Ziara ya Kikazi Wilayani Kilosa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Hamad Y. MASAUNI (Mb) amefanya ziara ya siku mbili kikazi Wilayani Kilosa, ambapo alipata nafasi ya kutembelea ujenzi wa Gereza la Wilaya hiyo, kuzungumza na kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya pamoja na kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi katika Mji mdogo wa Mikumi.

Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa Idara, Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mheshimiwa Denis Lazaro Londo pamoja na viongozi wa CCM wilaya hiyo.

Fuatilia matukio katika Picha.

IMG-20230220-WA0769.jpg
IMG-20230220-WA0776.jpg
IMG-20230220-WA0777.jpg


#Kilosaye2Fursaze2
#Uongoziwapamoja
#MaendeleoEndelevu
IMG-20230220-WA0761.jpg
IMG-20230220-WA0763.jpg
IMG-20230220-WA0762.jpg
IMG-20230220-WA0764.jpg
IMG-20230220-WA0771.jpg
IMG-20230220-WA0771.jpg
IMG-20230220-WA0774.jpg
 
Mm nilidhani Simbachawene ni waziri wa mambo ya ndani. Kumbe ni huyu? Sasa Simbachawene ni waziri wa nn?

Maana hivi sasa mawaziri wamekuwa wakigeuzwa geuzwa kama chapatihadi hatuelewi?
 
Alienda kumsalimia dogo lake bwana shaka h shaka, aliyekuwa mcc mara mnec hadi mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya.

Huyu jamaa wamemshusha, sijui alikosea nin, bora angepelekwa hata huko ubalozn hata burundi
 
IMG-20230220-WA0340.jpg


Nawasalimu kwa Jina la JMT,

Naamini mtakubaliana na Mimi, ni Wakati wote,Viongozi wengi wa Kitaifa na Kimkoa au kiwilaya hupendelea zaidi kufanya ziara zao hasa kwenye maeneo yenye viongozi wenye nia, Utayari na Uhitaji wa kuona maeneo wanayoyaongoza yanapiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa haraka,

Pamoja na maeneo mengine Wilaya ya Kilosa mara baada ya ujio wa mkuu mpya wa Wilaya hiyo Mhe Shaka Hamdu Shaka viongozi wengi wa Kitaifa na kimkoa Wameanza kumikinika Kilosa kwaajili ya Ziara za kikazi ili kutekeleza Ilani pamoja na kutoa support kwa DC huyo anayeonekana anayo kiu na hamu ya kuifanya Kilosa na Morogoro kuwa Mkoa/Wilaya ya kupigiwa mfano Kitaifa katika Utekelezaji mzuri na waharaka wa Ilani ya CCM ya 2020|25 pamoja na Mpango wa maendeleo wa Taifa,

[WAKATI NAANDIKA MAKALA HII TAYARI WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MHE HAMAD YUSUPH MASAUNI YUKO KATIKA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI KILOSA]

====
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Y. MASAUNI (Mb) amefanya ziara ya siku mbili kikazi Wilayani Kilosa, ambapo alipata nafasi ya kutembelea ujenzi wa Gereza la Wilaya hiyo, kuzungumza na kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya pamoja na kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi katika Mji mdogo wa Mikumi.

Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa Idara, Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mheshimiwa Denis Lazaro Londo pamoja na viongozi wa CCM wilaya hiyo.

#Kilosaye2Fursaze2
#Uongoziwapamoja
#MaendeleoEndelevu
IMG-20230220-WA0335.jpg
 
Hao sio viongozi bali ni majizi ya kura yanatembeleana.
 
Kumpa UDC SHAKA ni matumizi mabaya ya rasilimali watu Jamaa level yake sio hiyo
 
Wanafika hapo kuna alama yoyote wanaacha kwa wanajamii wa husika?
 
Sim
Mm nilidhani Simbachawene ni waziri wa mambo ya ndani. Kumbe ni huyu? Sasa Simbachawene ni waziri wa nn?

Maana hivi sasa mawaziri wamekuwa wakigeuzwa geuzwa kama chapatihadi hatuelewi?
simba wa wenyewe ni Waziri wa sera, bunge na kazi
 
Naona Kilosa itainuka kwa kasi sana Kama mwendo huu hautakuwa gasi ya soda
 
Back
Top Bottom