Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani imeeleza kuwa malipo hayo yalifanyika katika kipindi cha Julai 2022 hadi Mei 2023, kupitia mfuko wa Tuzo na Tozo wa Jeshi la Polisi.
Kati ya fedha hizo, Tsh. 948,335,400 zimelipwa kwa Askari 217 walioumia kazini na kiasi cha Tsh. 252,000,000 zimelipwa kwa Wasimamizi wa Mirathi na Familia za Asakri 16 waliopoteza maisha wakiwa kwenye majukumu yao.