Waziri Masauni, IGP Wambura na Ukimya juu ya mauaji ya kikatili yanayoendelea nchini

Waziri Masauni, IGP Wambura na Ukimya juu ya mauaji ya kikatili yanayoendelea nchini

Fortilo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,807
Reaction score
17,416
Wakuu Salam.

Mauaji ya kikatili yanayoendelea nchini hasa mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, ona sasa Mtwara yanastua, yanakera, ni hali ya kutisha, hujui lini na wewe utafikiwa.

Imefika mahali jamii inauliza hivi nchi hii sheria hakuna? hata tamko la mkuu wa jeshi la polisi kwa eneo husika hakuna zaid sana ni mwenyekiti wa kitongoji au kijiji anazungumzia mauaji.. i mean murder! na maisha yanaendelea.

kwa bahati mbaya zaid sababu za mauaji ni ukatili na vurugu za nyumbani, ikiwemo visa na visasi.

Imefika mahali raia kadhaa wanaungana kufanya uhalifu na wanaitwa wananchi wenye hasira kali, hasira gani za kusababisha mauaji, na pengine sababu hiyo hiyo ya kutunza uhai, serikali yetu haijawahi kutekeleza hukumu ya kifo.

Hoja yangu hapa ni ukimya wa Waziri Masauni na IGP Wambura, kwenye mauaji ya watu mbalimbali hapa nchini, angalau basi wakuu wa polisi wa maeneo husika watoe maelezo ya kueleweka kuliko kumuachia mwenyekiti wa kijiji au polisi wa kawaida kwani ushahidi unaweza kutoweka kwenye mazingira ya namna hiyo.

Kwa nchi za wenzetu hakuna tukio la mauaji linalopita hivi hivi bila kelele na amri za kutosha kutoka kwenye vyombo vy usalama na wauaji kutiwa nguvuni.

Angalao, kipindi cha Kova au yule RPC wa dodoma, kulikuwa na operation mbalimbali za kuziuia uhalifu, sasa hivi ukimya wenu unatuambia nini?

Waziri Masauni na IGP Wambura ukimya wenu unatia shaka sana juu ya uhalifu unaoendelea nchini.
 
Back
Top Bottom