John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Wadau kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa pamoja wametembelea Wizara ya Katiba na Sheria na kukutana na Waziri George Simbaachawene ambaye ameteuliwa kushika nafasi hiyo akichukua nafasi ya Prof. Palamagamba Kabudi.
Msafara huo wa THRDC uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao huo, Jaji Mstaafu, Joacquine De Melo, akiwa na Mratibu THRDC, Onesmo Olengurumwa, mjumbe wa bodi ya mtandao na Mkurugenzi wa ANGOZA kutoka visiwani Zanzibar, Hassan Juma, Mratibu wa THRDC Kanda ya Kati na Mkurugenzi wa Taasisi ya PLAJC, Jaruo Karebe, Mwakilishi kutoka THRDC-Zanzibar, Shadida Omar, Wakili Nuru Maro, Afisa Uchechemuzi kutoka THRDC, Neema mwakilishi kutoka Taasisi ya WOWAP,
Kwa upande wa Wizara, kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri Simbachawene, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Marry Makondo, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Nkasory Sarakikya pamoja na wajumbe wengine wa wizara hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amempongeza Waziri Simbachawene kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo adhimu, huku akiutambulisha mtandao na kutoa baadhi ya mapendekezo ya mtandao huo katika kuboresha mashirikiano baina yake na serikali kupitia wizara hiyo.
"Tuna wanachama zaidi ya 200 waliogawanyika katika kanda 11 nchini ambao hufanya Kazi katika maeneo yote ya haki za binadamu, ikiwemo maeneo ya wanawake, pamoja na watoto ambapo wanachama wetu wamekuwa wakishirikiana na wizara ya katiba na sheria pamoja na wizara ya jinsia na watoto, maeneo ya elimu, afya, amani, pamoja na utoaji wa msaada wa kisheria," Olengurumwa.
Olengurumwa ameongeza kwa kueleza kazi za mtandao ambapo umekuwa ukifanya kazi kwa mashirikiano na wizara pamoja na Taasisi zingine za kiserikali ikiwemo, Tume ya Haki za binadamu na utawala bora, Mahakama, bara na visiwani, TAKUKURU, TRA, pamoja na Ofisi ya Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Olengurumwa ameeleza kuwa baadhi ya maeneo muhimu ambayo AZAKI zimekuwa na mchango wa moja kwa moja kwa Serikali ni pamoja na eneo la utoaji wa huduma za afya, usafi wa mazingira, maji, ambapo kulingana na uchambuzi uliofanywa na serikali katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa (FYDP III), AZAKi zimekuwa zikichangia 40% ya uwekezaji katika sekta ya afya.
Katika majadiliano na wizara, THRDC imefanikiwa kutaja baadhi ya maeneo ambayo yanaweza kufanyiwa maboresho na wizara ikiwemo;
a) Wizara Kuwa na utataratibu mzuri wa kufahamu, kuripoti na kutambua Kazi zinazofanywa na Watetezi wa Haki za Binadamu kama Wadau muhimu wa wizara hiyo.
b) Kufanyika kwa maboresho katika maeneo ya utoaji wa msaada wa kisheria nchini.
c) Uboreshwaji wa mifumo ya utoaji Haki nchini.
d) Maboresho ya baadhi ya sheria ikiwemo sheria ya NGO, hasa katika upatikaji wa vibali vya tafiti ambavyo huyalazimu mashirika kupitia TAMISEMI Ili kupata vibali hivyo pamoja na sheria zingine.
e) Ushiriki wa wizara katika mikutano na majukwaa ya kimataifa.
f) Tanzania kurudi katika mahakama ya Afrika mashariki.
Pamoja na meneo hayo, THRDC imefanikiwa kutoa mapendekezo ya kufanyiwa kazi na Wizara katika kuboresha shughuli za utetezi wa Haki za Binadamu nchini. Mapendekezo hayo ni pamoja na;
1) kuboreshwa kwa mfumo wa utekelezaji (Human Rights Enforcement Mechanism - BRADEA) Sheria iliyokuwa inaweka utaratibu wa kulinda Haki za kikatiba.
Olengurumwa ameeleza kuwa mabadiliko yaliyofanyika yameweka vikwazo/ vingi kwa Mtanzania mmoja mmoja au taasisi zao kutekeleza agizo la ibara ya 26/2 ya kulinda katiba.
"Kumekuwa na vigingi vingi ambavyo tunaweza kufanya majadiliano na maboresho kupitia wizara hii ambavyo yatatoa fursa kwa Watanzania na Taasisi za Haki za Binadamu kwenda Moja kwa Moja katika mahakama hii kwa lengo la kulinda na kutetea Haki za Binadamu kupitia mlango wa kikatiba," - Olengurumwa.
2) Kuwepo kwa National Human Rights Action Plan (Mpango Kazi wa Taifa wa Haki za Binadamu).
"Serikali iangalie namna ya kuharakisha kukamilika kwa mchakato huo Ili Kuwa na andiko litakalotoa mwongozo utawaunganisha wadau wa haki za binadamu na serikali," -Olengurumwa.
3) Kuwepo na Sera ya Haki za Binadamu ambayo inaweza kutoa mwongozo kwa taasisi binafsi na serikali kuhusiana na Maswala ya Haki za binadamu.
Sera hii itawatambua na kiwalinda Watetezi wa Haki za Binadamu. Hii ni kuwawezesha wadau pamoja na serikali kuwa na uelewa wa pamoja wa maswala ya utetezi na watetezi wa haki za binadamu nchini.
4) Eneo la utekelezaji wa Hukumu/maamuzi ya Mahakama za ndani na za kimataifa.
"Kumekuwa na changamoto za utekelezaji wa maamuzi wa mahakama hasa katika maeneo ya upatikanaji haki 'access to justice' katika kesi za Haki za Binadamu, lazima uje Dar es Salaam. Tunapendekeza serikali iruhusu kila mahakama yenye hadhi ya mahakama kuu iwe na uwezo wa kusikiliza kesi hizo katika mikoa kesi hizo ziliporipotiwa," - Olengurumwa
Baada ya wasilisho hilo wawakilishi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria walipata wasaha wa kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa na THRDC.
Akijibu hoja ya kuwepo kwa Mpango Kazi wa Haki za Binadamu (Human Rights Action Plan), Mkurugenzi wa Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Nkasory Sarakikya ameeleza kuwa wizara hiyo inatarajia kutoa Andiko hivi karibuni huku akitaja changamoto kadhaa zilizochangia kuchelewa kwake ikiwemo mchakato wa UPR, lakini kwa kushirikiana na wadau wizara inatarajia kuhakikisha Andiko Hilo linazinduliwa hivi karibuni.
Nkasory amejibu kuhusu Mikataba ya Haki za Binadamu iliyoridhiwa na Tanzania, kwa kueleza kuwa bado kuna taarifa za nchi ambazo Tanzania inatakiwa kuwasilisha, ambapo wizara imeendelea kufanyia kazi maandiko kadhaa ikiwemo CRC na SIDO ambayo yanaandaliwa na wizara za maendeleo ya Jamii, jinsia na watu wenye ulemavu kwa kuwa walishaandaa rasimu zao, hivyo wizara ya Katiba na sheria inatarajia kufanya uhakiki na kukamilisha michakato kwa ajili ya kuwasilishwa kwake. Maandiko ya ACCPR pamoja na Maputo Protocol yote yatawasilishwa hivi karibuni.
"Tukiwa tunaandaa taarifa za nchi, mara zote serikali imekuwa ikiwahusisha wadau wa Haki za Binadamu ikiwemo CSO's zote Tanzania bara na visiwani. Hii inatusaidia sana kujua nini kinaendelea Nchini kwani nyinyi mna reach kubwa sana mnatusaidia kufika kule tusipoweza kufika msaada wenu unakuwa mkubwa sana kwetu," - Nkasory Sarakikya.
Katika suala la utolewaji elimu kwa wasaidizi wa kisheria, wizara imeeleza kuwa inaona umuhimu mkubwa na ipo tayari kushirikiana na wadau kutoa elimu kwa wasaidizi wa kisheria.
Naye Waziri Simbachawene ameelezwa kufurahishwa na ujumbe uliomtembelea ambao umezingatia usawa wa kijinsia pamoja na kujumuisha Wadau kutoka pande zote za muungano.
"Tanzania ni nchi ambayo inatambua, inaheshimu, inatunza na kulinda haki za binadamu, hivyo sisi tunashirikiana na ninyi taasisi hizi za wadau na wa Haki za Binadamu katika kazi nyingi mnazozifanya kweli zinasaidia Serikali," - Waziri Simbachawene na kuendeleza:
"Wizara ya Katiba na sheria imefurahi kuona mpo na itaendelea kushirikiana na nanyi katika kila jambo ambalo mtapenda tushirikiane," Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene amewataka watetezi wa Haki za Binadamu nchini kuhoji na kuzungumza na wizara pale kunapotokea jambo lenye ukakasi katika serikali, badala ya kupeleka hoja katika majukwaa ya kimataifa na kuiondolea heshima nchi. Ameeleza kuwa Nchi ya Tanzania ndiyo mama yetu, hivyo inapaswa kujengwa kwa ushirikiano.
Akijibu hoja ya Tanzania kujitoa katika Mahakama ya Afrika, Waziri Simbachawene ameeleza kuwa, katika suala hilo zilikuwepo na sababu, lakini haziwezi kuwa za kudumu, hivyo mazungumzo yanaendelea ndani ya Serikali na anaamini Tanzania itarudi tena katika Mahakama hiyo.
"Mahakama hii ipo Tanzania, inakuwa si vizuri sana kama tena sisi Watanzania kutokuwa kule. Tupewe muda, mchakato unaendelea nina imani si muda mrefu maamuzi yatatolewa na serikali," alisema Waziri Simbachawene
Source: THRDC