Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amelitaka Baraza la Kumi na Tatu (13) la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kuhakikisha linasimamia kikamilifu kufanyika kwa mafunzo na tafiti zinazolenga kutatua changamoto katika Sekta ya Usafirishaji na kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi nchini
Prof Mbarawa ametoa maagizo hayo wakati akizindua Baraza la 13 la Uongozi wa chuo Cha Taifa Cha usafirishaji ambapo alisema chuo hicho kina wajibu mkubwa wa kuisaidia Serikali kuandaa sera madhubuti katika masuala yote ya uchukuzi
Alisema hatua hiyo itawasaidia kuendana na mpango mkakatia wa chuo wa miaka mitano unaolenga kuboresha ubora wa Elimu na mafunzo ilikukidhi mahitaji ya soko la ajira la kisasa katika sekta ya usafirishaji na kuimarisha miundombinu ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na maabara, maktaba na teknolojia ya kisasa
"Napenda kuwahakikishia kuwa Wizara na Serikali kwa ujumla, itaendelea kutoa ushirikiano na msaada unaohitajika ili kuhakikisha kuwa Chuo hiki kinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi" alisema