Waziri Mbarawa ataja sababu za kubinafsisha bandari zetu kwa wageni

Waziri Mbarawa ataja sababu za kubinafsisha bandari zetu kwa wageni

Huyu professor naye na Fala kama mafala wengine. Serikali inashindwa kuwasimamia watumishi wake itaweza kwa secta binafis
Sasa kipi unachopendekeza ?!!![emoji15]

Ya kwamba upembuzi yakinifu kufikia uamuzi huu haujafanyika?!!!

Ni kuwa kuhitaji mifumo ya tehama kusomana Kati ya TRA na TPA si suluhisho la changamoto katika bandari zetu?!!!
 
Binafsi mimi ninaona ni jambo jema ila mkataba huu upitiwe na Wataalam waliobobea katika masuala ya bandari. Mfano kama Bandari tunapata 700bn/= kwa mwezi na wenyewe wakitupa 1.5trn/- kwa mwezi kuna mbaya gani. Nadhani watapewa masharti ya kuweka vifaa vya kisasa na mengineyo mengi.
[emoji106]
 
Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi Katika Shughuli za Uendelezaji na Uendeshaji wa Bandari

229. Mheshimiwa Spika, Ushirikishaji wa Sekta Binafsi katika uendeshaji wa shughuli za bandari zilianza kuchukuliwa na Serikali mwishoni mwa miaka ya 1990 kupitia Tume ya Kurekebisha Mashirika yaUmma (Parastatal Sector Reform Commission-PSRC).

Mwaka 2000, Serikali iliamua kuingia Mkataba na Kampuni binafsi ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) kwa ajili ya uendeshaji waKitengo cha Makontena Gati Na. 8 – 11 katika Bandari ya Dar es Salaam. Katika kipindi chote cha utendaji kazi wa TICTS, Serikali kupitia TPA imepata mafanikio yafuatayo katika kipindi cha mwaka 2001 hadi 2021.

i. Uwekezaji katika manunuzi ya mitambo ya kuhudumia shehena, miundombinu, mifumo ya TEHAMA na kuwajengea uwezo wafanyakazi;

ii. Kuongezeka kwa shehena ya makasha kutoka makasha ya futi ishirini 382,000 mwaka 2012 hadi kufikia makasha 642,000 mwaka 2021 sawana ongezeko la wastani wa asilimia 8.0 kwamwaka; na94

iii. Kampuni hiyo iliweza kulipa kodi na tozo nyinginezo za Bandari kutoka kiasi cha Shilingi bilioni 235 mwaka 2012 hadi kufikia Shilingi bilioni 635 mwaka 2021.230.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo kumekuwa na changamoto kadhaa zikiwemo:

i. Kushindwa kuchagiza shughuli za kibandarikatika mnyororo wa usafirishaji;

ii. Uwekezaji mdogo katika mitambo ya kupakia nakupakua mizigo;

ii. Urasimu wa uondoshaji wa mizigo bandarini;kutokuwa na maeneo ya kutosha nje ya bandariili kupunguza msongamano bandarini;

iv. Kutofanya ukarabati wa miuondombinu yabandari, kutofanya ukarabati wa mitambo kwawakati; na

v. Kutokuwa na mikakati ya kuvutia shehena kupitia Bandari ya Dar es Salaam; kutowekeza katika mifumo ya TEHAMA ya kisasa inayosoma na na mifumo iliyopo TPA.

Kwa kutambua kuwa, TPA pekee haitaweza kutatua changamoto za Bandari zilizopo na kuongeza ufanisi wa bandari nchini, Serikali iliamua kuanzisha jitihada zakutafuta wawekezaji ambao watakuwa na uwezo wakutatua changamoto zilizobainishwa hapo juu.

231. Mheshimiwa Spika, hatua hizo zimehusisha kukutana na kufanya majadiliano na wawekezaji mbalimbali. Baadhi ya wawekezaji waliojitokeza wameonesha nia ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya bandari nchini ikiwemo; Bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Tanga, Bandari ya Mtwara, Maeneo ya Bandari Kavu na Bandari za Maziwa Makuu ili kulenga soko la nchi zinazotuzunguka, ambalo linakua kwa kasi.

Kama ilivyo kawaida, Bunge lako Tukufu litashirikishwa ipasavyo wakati wa kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yaDubai (Inter Governmental Agreement – IGA) kwa ajili ya ushirikiano wa kuboresha, kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari nchini.
Waliingia hiyo mikataba kwa ruhusa ya nani?
 
Kwani mh.Mpina naye hataki kuona mifumo ya TEHAMA kati ya TPA na TRA inasomana?!!!
Anataka. Ila mkataba wa IGA ndo anashauri kuutathimini madhara yake hasa kujilock kwa mwekezaji na mbadala tutumie tu M o U kama sekta nyingine.
....sina hakika kama tuko pamoja endapo uko busy huko BBT
 
Huyu professor naye na Fala kama mafala wengine. Serikali inashindwa kuwasimamia watumishi wake itaweza kwa secta binafis
Mimi siku nyingi sana nimeomba tuanze na kuwatafuta wawekezaji wa kutuendeshea serikali yetu kwa ufanisi, kwa sababu matatizo yetu yote yanasababishwa na hawa watu waliomo serikalini.

Huyu Profesa Makame hapo zamani nimchukulia kuwa mtu makini, kumbe hana kitu chochote cha maana.

Hovyo kabisa!

Hata haoni aibu, TICTS wamekaa hapo zaidi ya miaka 20, lakini bado haoni jinsi maelezo yake yanavyopingana yenyewe!
 
Ufisadi mwingine huo unatengenezwa.

Mtu anasimama bila aibu kabisa kutetea wizi.

Haya mambo Mungu hayapendi jamani tuyaache.
 
Huyu professor naye na Fala kama mafala wengine. Serikali inashindwa kuwasimamia watumishi wake itaweza kwa secta binafis
Ni mzanzibari, wazanzibari ni watu wa cherekochereko tu wavivu kufikiri, arudi akaendeshe bandari za kwao,
 
Back
Top Bottom