Waziri wa Utumishi wa Umma, Mhe. Mchengerwa amesema watumishi wengi wenye uwezo mzuri wa kiutendaji wana fanyiwa mizengwe na majungu ya kuharibiwa kazi, na mbaya zaidi mabosi wao wanakuwa ni sehemu ya kuwaharibia.
Waziri Mchengerwa amedhamiria kuondoa hali hiyo katika idara zote za Serikali ameeleza kuwa tatizo hilo limekuwa ni kama kansa ktk utumishi wa umma.
Kwa maneno hayo ya Mhe. Waziri inaonekana kuna tatizo kubwa sana tena sana. Viongozi wa juu yaani mabosi wana waonea sana watumishi wa chini, ukionekana mwerevu tu unapigwa nyundo ya kichwa. Kuna baadhi ya watendaji wenye dhamana wanajiona wao ni miungu watu
Ushauri:
kama kweli Waziri Mchengerwa amedhamiria kuwafuta machozi wanao nyanyaswa basi aunde tume maalumu itakayo fuatilia kero za watumishi ktk kila idara za Serikali nchi nzima.
Uchunguzi ufanyike kila idara, kuna uonevu mkubwa sana, watu wanaonewa na viongozi wao bila sababu za msingi, watu wanalia hakuna wa kuwasikia.
wapo watumishi wa umma wanatamani hata kuacha kazi kutokana na uonevu wanao fanyiwa na viongozi wao wa juu, wanachafuliwa kwa maksudi ili wasisonge mbele.
Hali hii ni hatari sana endapo itaachiliwa iendelee, lazima jambo lifanyike;
kwanza kubaini matatizo hayo ktk Idara zote za Serikali, lkn pia kuwaondoa viongozi watendaji ambao wamekuwa na tabia za uonevu kwa walio chini.