Tumekusikia jana ukitoa maelekezo ya kutosha Baraza la michezo jinsi Wizara yako mnavyotaka isimamie mpira wa miguu “as if” Baraza la Michezo kazi yake ni kusimamia mpira wa miguu tu na huku ukijisahau kuwa wewe sio Waziri wa mpira wa miguu peke yake. Okay tuliacahe hilo.
Tumesikia maoni ya wizara yako (sijui ni yako binafsi) kuhusu suala zima la Waamuzi wa mpira wa miguu na mapendekezo uliyoyatoa ikiwemo kuwashirikisha TAKUKURU katika semina za uwezeshaji waamuzi !!? Kweli Takukuru Mchengerwa!!
Haya hili tuliache, huku ukielewa kuwa bajeti ya wizara yako ni ndogo karibia kuliko wizara zoote unakuja na wazo la VAR na kwamba kama wizara mna mpango wa kuagiza VAR kwa ajili ya viwanja vitano (5) tu kwa kuanzia. Kweli Waziri umefikiria saana hili au umedanganywa na akili za yule Waziri mwenzako “mpigaji” ambaye lazima VAR moja aagize ifungwe Singida!
Ahaa... Kweli Mchengerwa najua umecheza mpira wa miguu na unamiliki timu kama alivyo huyo waziri mwenzako anayekupotosha. Kweli tatizo la soka letu Bongo ni waaamuzi? Umeangalia viwanja vyetu, vipi posho na maslahi ya wasimamizi wa mpira wa miguu!!
Camera zenyewe za kurekodi mechi zinatosha, vipi kuhusu taa? au Unajua gharama ya VAR moja. Hapa Africa ni Morocco peke yake wameweza kutumia VAR wewe fikiria hata Champions League Africa imetumika kwenye mechi moja tu ya Fainali mwaka jana.
Vile vile elewa unapoamua kuzungumzia michezo hapa nchini hiyo ni agenda kubwa saana lakini kikubwa sote tunaelewa katika nchi maskini kama zetu tuna vipaumbele vingi saana kuliko michezo na ndio maana wizara yako inakuwa haipewi kipaumbele saana kama wizara nyingine.
Kama unataka kusaidia michezo na kuna pesa kidogo wekeza kwenye michezo iliyosahaulika na sio mpira wa miguu. Mpira wa miguu ni wa mwisho kwani umeshasimama saana kulinganisha na michezo kama kuogelea, kuruka juu na chini n.k….vipi UMITASHUMITA ipo kweli!!
Ushauri wangu Bwana mdogo Waziri:
Ukitaka mama asizidi kukupoteza pamoja na ukaribu mlio nao angalia na tafakari juu ya huu msemo. Akili kuambiwa changanya na yako...JMK