LGE2024 Waziri Mchengerwa: Taarifa nilizonazo hadi sasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaendelea Vizuri na kwa Hali ya Amani nchi nzima

LGE2024 Waziri Mchengerwa: Taarifa nilizonazo hadi sasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaendelea Vizuri na kwa Hali ya Amani nchi nzima

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
1732709816056.png

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewaelekeza wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi kuwasaidia wapiga kura kusoma orodha ya majina vizuri ili wote waliojiandikisha wapate fursa ya kupiga kura.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura katika kituo chake alichojiandikishia cha Umwe Mchikichini kilichopo Ikwiriri Jimboni kwake Rufiji Mkoa wa Pwani, Waziri Mchengerwa amesema taarifa alizonazo mpaka sasa uchaguzi unaendelea kwa hali ya amani na utulivu nchi nzima.
 
Watu wengi hawajapiga kura na vituo vingi hakuna watu kabisa hasije kuongopa kesho kwamba 90% ya wapiga kura wamejitokeza.
 
Ukweli au uongo, anaujua Mwenyezi Mungu. Na kwa wakati muafaka, atatenda haki
 
Back
Top Bottom