PreGE2025 Waziri Mchengerwa: Wanaoleta Vurugu Dar wanatoka nje ya Nchi, Chalamila washughulikie

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu akiachiwa aendelee kutoa vitisho atamaliza watanzania,kauli kama hii alipomaliza kuitoa kule mbeya Mdude akatekwa na hajapatikana mpaka sasa hivi Kuna haja ya kumhusisha na haya yanayoendelea ya utekaji.
 
Watanzania hawavumilii bali wanawachana makavu. Kupewa makavu ndio wao hawataki wanaita uvunjifu wa amani😂! Yani ukisema wazi wasichokipenda wana mbogamboga jua your days are numbered.
Waambie ukweli Hawa machawa uchwara hawajitambui kabisa!
 
Huyu naamini hata kikundi Cha utekaji kipo chini yake,ni lini Dar kumetokea vurugu?halafu analeta ubaguzi kwa mikoa mingine eti wanatoka nje ya Dar huyu anajifanyaga yeye mwenyewe ni waziri wa mambo ya ndani.
 
Mimi nawaomba waTanzania, wawanyime hawa majangiri vyote: "legal legitimacy'; kwa kutimiza "NO ELECTION", na wawanyime "political legitimacy", kwa kutopiga kura kabisa.
Hiki ndicho CCM na Serikali yao wanakiogopa. Wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanaua NRNE baada ya kubaini imewaingia Wananchi vizuri. Kuna mabilioni yametengwa! huwezi amini
Wanachotaka ni hao 5M, halafu akina Rungwe na Zitto wapewe Ubunge ili kuwe na upinzani japo feki.
Hawa milioni tano hawafiki hata asili mia 25 ya watu wenye sifa ya kupiga kura Tanzania. Sasa sijui kweli kama hiyo bado itakuwa ni "legal legitimacy' ya kuzungumzia popote!
Katika uhuni CCM hawajali namba, wanachotaka ni watu laki 2 basi wanaenda kujiapisha uwanja wa Taifa
Ninaamini kabisa kwamba waTanzania safari hii wanaweza kabisa KUZUIA uchaguzi usifanyike, kama kutakuwepo na uongozi wa ku-coordinate vizuri juhudi zao za kukataa kunyimwa HAKI yao ya msingi, i.e., kuchagua viongozi wanaowataka wawaongoze.
Tatizo ni njaa za baadhi. Kuna mabilioni yametengwa
 
Tatizo ni njaa za baadhi. Kuna mabilioni yametengwa
Unajuwa?

Hayo "mabilioni" yaliyo tengwa yasingeweza kuwanunua waTanzania walio elimika vizuri juu ya kuhujumiwa HAKI yao ya msingi. Tatizo lililopo ni muundo uliopo unaowawezesha CCM kuwa kila mahali, tokea kwenye sina, (nyuma kumi kumi), mitaani; kwenye kata; Tarafa; Wilaya; Mikoani hadi kitaifa.
Juhudi zao (za CCM) kushinda kila mahali wakati wa uchafuzi wa Serikali za mitaa (2024), lilikuwa ni hilo hilo la kuweka na kutumia ushindi huo kuhakikisha huu wa Kitaifa unakuwa rahisi.
Sasa watakacho fanya ni kusambaza hayo mabilioni kwenye hizo ngazi za chini; wakilenga hasa hao viongozi wao, ambao ndio watakaofanya kazi ya ziada huko mitaani kuhakikisha mabilioni yanazalisha ushindi.

Lakini, endapo kama wananchi watakuwa wamepata elimu ya kutosha, na kuwepo na uongozi wa kuwapa mbinu za kuzuia uchaguzi siku hiyo ya uchafuzi; inawezekana kabisa kukomesha hata hayo mabilioni yasiweze kuwanunuwa hao wenye bei hiyo.

Haitahitaji watu wengi sana waliojipanga vizuri kuzuia uchafuzi wa aina hiyo. Watuu hao watakuwa huko huko mitaani, waliko hao wa CCM wanaonunua waTanzania wenzao.
 
Anademka tu maana sio hizo vurugu huku mijini......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…