Naam, Hijja haihusiani na madhambi binafsi ya mtu. Kutenda dhambi sio sababu ya Muislam kuacha kufanya Wajibu. Ijapokuwa Muislam anatakiwa kuacha dhambi anazozifanya, ila kuzifanya kwake/kutoziacha dhambi sio sababu ya kuacha Wajibu na kuacha kumcha Mola wake.
Halafu kuwa Muislam Mcha Mungu haimaanishi kuwa haiwezekaniki kabisa kwake kutenda dhambi. Muislam Mcha Mungu inawezekana akatenda dhambi, tena kubwa, ila tofauti ni kwamba Ana sifa ya kutubia anapotenda dhambi na huwa hafululizi madhambi akabakia ndani yake (bila ya kutubia).
Angalia miongoni mwa sifa za wachaMungu;
ayat 133 from Surah Al Imran
﴿۞ وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ﴾
[ آل عمران: 133]
Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa
wachamngu,
ayat 134 from Surah Al Imran
﴿الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ﴾
[ آل عمران: 134]
Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema;
ayat 135 from Surah Al Imran
﴿وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴾
[ آل عمران: 135]
Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo yafanya na hali wanajua.
Kwahiyo sio kwamba Muislam Mcha Mungu haiwezekaniki kabisa akatenda dhambi au sharti ni lazima awe hatendi dhambi kabisa kabisa.
Na sio kwamba Muislam anayetenda dhambi ikawa sababu ya kuacha kufanya Twaa. Hii ni Twaa na hii ni dhambi. ANATAKIWA KUACHA DHAMBI, ila kutoacha kwake sio sababu ya kuacha Twaa.
Muislam anaweza akawa mlevi na wakati huo huo anaswali Swala 5. Anatakiwa kuacha dhambi zake, ila kutoziacha hakumzuii kutenda mema na kutekeleza ya Wajibu.
Sikiliza
View attachment 3344929
Sitetei dhambi za Muislam yeyote
Ila nilitaka kuliweka jambo hilo sawa.
Allah anisamehe nilipokosea. Na anipe ikhlaasw katika hili nililoandika na matendo yangu mema na anisamehe madhambi yangu
Na Allah ni Mjuzi zaidi
Allah awaongoze watawala wa kiislam katika njia iliyonyooka.
Namuomba Allah anifishe katika Tawheed na Sunnah. Aamiin.