Waziri Mkenda asema ufaulu somo la hisabati ni janga linalotakiwa kutafutiwa ufumbuzi

Waziri Mkenda asema ufaulu somo la hisabati ni janga linalotakiwa kutafutiwa ufumbuzi

Uko sahihi kabisa. Hiyo ni case iliyotokea kwako nakubaliana na wewe. Nataka uamini kwamba sijawadharau walimu wa hisabati shule za msingi na sio wote ila wengi wanaolifundisha somo la hisabati kwa level za chini baadhi yao uwezo ni mdogo ama hukabiliwa na majukumu ya ufundishaji makubwa sana kwa sababu ya uchache wao na wanafunzi ni wengi. Hili somo linataka full 100% participatory yaan mwanafunzi afatilie kila hatua kwa makini na baada ya hapo mwalimu nae afatilie vitendo anavyovifanya mwanafunzi. Sasa unakuta mwalimu wa hisabat kwa wiki anavipindi 72 na wanafunzi anahudumia wapo kama elfu 1 yeye yupo peke yake.
Mkuu nimeishi sana na walimu...

Walimu wanaojua kufundisha ni wale wenye elimu ndogo (certificate).

Hawa wenye degree wanatakiwa wafundishe watu wazima wenzao....

Kuna jamaa alifeli kabisa form four akaamua kujiajiri kwa kufundisha somo la hisabati tu kwenye mashule yanayomuhitaji....anafundisha darasa la saba tu...

Asikwambie mtu huyo jamaa ukimpa darasa januari hadi wafanye mtihani karibu nusu ya darasa watapata "A"..

Lakini yeye alipata F form four...akapata "ZERO" matokeo ya jumla...

Nilikutana 2018 akiwa shule moja hivi huko KILOSA.

Alisema wakati yupo O LEVEL alikuwa na matatizo ya kifamilia..

Alifiwa na wazazi wake wote wawili...

Hakuwa na ndugu wa kumsaidia.. alikuwa anafanya mishe zake mtaani shule anaenda kufanya mtihani.

Baada ya matokeo kutoka...kafeli vibaya.!!

Na shule ya msingi alikuwa kichwa tu...

Akaanza kufundisha mtaani kama tuition....walimu waliona mabadiliko ya wanafunzi wanaosoma kwake..

Wakamvuta school kabisa...

Baada ya hapo amekuwa maarufu kwa kazi hiyo tu..

Kufundisha hisabati....

Ualimu ni kipaji zaidi kuliko ELIMU...kuna wenye wa kufundisha wenzao kwa urahisi hata elimu zao ziliishia kidato cha nne....

SERIKALI iajiri walimu.....iache kutafuta sababu kwa hawa waliopo kazini...

Kuna shule ya sekondari home haina mwalimu wa mathematics....waliopo wanafundisha kwa kuwa mwenye uwezo wa kufundisha hawapo
 
Zamani miaka ya 80, ukifeli sekondari inaenda ualimu! Ilifika mahali ikahalalishwa division 4 ni ualimu!! Sasa aliyefeli anafundishaje? Tuige Ujerumani, anaefaulu vizuri ndiye anaechukuliwa ualimu. Chunguza kwa makini wanaofundisha Kiingereza na hesabu!
Wewe kama ulifaulu kamfundishe mwanao.Waliomaliza form four wakienda ualimu hawafundishi sekondari, bali shule za msingi na wanakuwa na cheti.Wanaofundisha sekondari ni waliomaliza form six na kuendelea.
 
Zamani miaka ya 80, ukifeli sekondari inaenda ualimu! Ilifika mahali ikahalalishwa division 4 ni ualimu!! Sasa aliyefeli anafundishaje? Tuige Ujerumani, anaefaulu vizuri ndiye anaechukuliwa ualimu. Chunguza kwa makini wanaofundisha Kiingereza na hesabu!
Watu wanakwenda course za afya kwa Div IV ya D mbili na wanawadunga sindano za mpododo mnaona poa, mnawashupalia walimu.
 
Nilichosema hakina ukweli? Fanya utafiti wa kina. Sawa form four wanaandaliwa kuwa waalimu wa msingi, je waliofaulu vizuri? Sasa kama alifeli hesabu , atafundisha hesabu? Wengi wanakwepa hilo somo. Siku hizi waliomaliza shahada ya kwanza masomo ya Sanaa ualimu wanapangiwa shule za msingi, na hesabu inawapiga.
 
Bado swala la Elimu kwa ujumla nchini kwetu ni changamoto!
Kama hayati Mkapa alivyosema kunahitajika Mjadala wa Kitaifa kuhusu Elimu akapuuzwa na Mwendazake bado jambo hili siyo la kupuuza.Hali ya elimu kwa ujumla ni mbaya tu.
 
kwa maoni yangu tatizo lipo kwa wataalamu wetu walio jazana Wizarani na NECTA hawaumizi vichwa kubaini tatizo na kutoa mapendekezo ya kuboresha Elimu yetu.
Haiwezekani miaka nenda miaka rudi!...changamoto zile zile zinapigiwa kelele.....ohhh!......Mfumo wa Elimu yetu ni mbovu......, lakini cha ajabu wataalamu wetu wanaokula mishara wapo kimyaaaaa! kama vile hawahusiki !!
 
Ndipo hapo sasa mjadala unahitaji ili kutoa nafasi kwa wadau kuchangia mawazo hatimaye Taifa litoke na ajenda moja ya jinsi ya kukwamua Elimu ambayo naona inazidi kuzama.
 
Mtoa mada una uhakika kuwa wanaofundisha hesabu walifeli somo hilo au ndo yaleyale, mwendo wa kukaririshwa upumbavu humu mitandaoni?!!

50686E43-C571-4CE4-8B42-B3B008235145.jpeg
 
MKUU .. em edit kidogo uzi wako kumradhi.. sio walimu wote wanaofundisha hisabati walifeligi MKUU.. tunakuheshimu MKUU na unafahamu hilo tafadhwali
 
Mitaalam yenyewe yakizamani mtu unamfundisha mitopic usiyoitumia katika maisha ya nini sasa?
Mitaala kwanza iangazwe sio hesabati tu kila somo hasa masomo ya sayansi.
Huyu nae asipokuwa makini atakuwa kama prof. Mwenzie alyemtangulia ambae alikuwa hata lugha muhimu ilimshinda!
Tatizo la ubora wa elimu Tanzania hauko kwenye hisabati tu bali kwenye masomo yote!! Hivyo ukitaka kuboresha elimu ni lazima uichambue yote in totality!! Toka Mitaala ya masomo na relevance yake kwa Taifa, quality of teaching, vitendea kazi (madarasa na vitabu). Baada ya kufanyia utafiti kwa kina yote hayo ndipo unaweza kupata njia ya kuweza kuboresha elimu. Otherwise utaishia kutoa statements mbovu mbovu tu na kuwa kituko na uprofesa wako.
 
Back
Top Bottom