The Eye
JF-Expert Member
- Oct 29, 2020
- 278
- 393
Mkuu nimeishi sana na walimu...Uko sahihi kabisa. Hiyo ni case iliyotokea kwako nakubaliana na wewe. Nataka uamini kwamba sijawadharau walimu wa hisabati shule za msingi na sio wote ila wengi wanaolifundisha somo la hisabati kwa level za chini baadhi yao uwezo ni mdogo ama hukabiliwa na majukumu ya ufundishaji makubwa sana kwa sababu ya uchache wao na wanafunzi ni wengi. Hili somo linataka full 100% participatory yaan mwanafunzi afatilie kila hatua kwa makini na baada ya hapo mwalimu nae afatilie vitendo anavyovifanya mwanafunzi. Sasa unakuta mwalimu wa hisabat kwa wiki anavipindi 72 na wanafunzi anahudumia wapo kama elfu 1 yeye yupo peke yake.
Walimu wanaojua kufundisha ni wale wenye elimu ndogo (certificate).
Hawa wenye degree wanatakiwa wafundishe watu wazima wenzao....
Kuna jamaa alifeli kabisa form four akaamua kujiajiri kwa kufundisha somo la hisabati tu kwenye mashule yanayomuhitaji....anafundisha darasa la saba tu...
Asikwambie mtu huyo jamaa ukimpa darasa januari hadi wafanye mtihani karibu nusu ya darasa watapata "A"..
Lakini yeye alipata F form four...akapata "ZERO" matokeo ya jumla...
Nilikutana 2018 akiwa shule moja hivi huko KILOSA.
Alisema wakati yupo O LEVEL alikuwa na matatizo ya kifamilia..
Alifiwa na wazazi wake wote wawili...
Hakuwa na ndugu wa kumsaidia.. alikuwa anafanya mishe zake mtaani shule anaenda kufanya mtihani.
Baada ya matokeo kutoka...kafeli vibaya.!!
Na shule ya msingi alikuwa kichwa tu...
Akaanza kufundisha mtaani kama tuition....walimu waliona mabadiliko ya wanafunzi wanaosoma kwake..
Wakamvuta school kabisa...
Baada ya hapo amekuwa maarufu kwa kazi hiyo tu..
Kufundisha hisabati....
Ualimu ni kipaji zaidi kuliko ELIMU...kuna wenye wa kufundisha wenzao kwa urahisi hata elimu zao ziliishia kidato cha nne....
SERIKALI iajiri walimu.....iache kutafuta sababu kwa hawa waliopo kazini...
Kuna shule ya sekondari home haina mwalimu wa mathematics....waliopo wanafundisha kwa kuwa mwenye uwezo wa kufundisha hawapo