Naomba niwape uhalisia wa hili jambo japo kwa uchache tu, mwaka jana kikao kilikaa na mwalimu mkuu wa hiyo shule alihudhuria hicho kikao. Na baaada ya kikao mwalimu mkuu alikabiziwa pesa taslimu milioni moja na chenchi, na alitoa ahadi hadi kufikia mwezi wa 12 mwaka jana viti na meza kwajili ya walimu wa shule yake vitakuwa vipo tayari.
Ila kwa maelezo ya mtendaji, yeye alisema alimpigia simu mwalimu mkuu wa hiyo shule kuulizia zoezi hilo limefikia wapi na ilikuwa mwezi wa 12 kwenye tarehe 24. Mwalimu akajibu vipo katki hatuwa ya mwisho hadi kufikia januari shule kufunguliwa kilakitu kitakuwa sawa.
Mtendaji alienda asubuhi wiki hii akiwa na mgambo kama moja ya majukumu yake kukaguwa hali ya hapo shuleni ili ajionee mwenyewe, ila kilicho msikitisha alikuta madawati ya wanafunzi ndio walimu wamekalia ofisini, na mwalimu mkuu hakumkuta hapo shuleni😡....
Anyway mimi namuunga mkono mtendaji kwa hatua aliyochukuwa.
°Kama pesa ilitoka na akapewa mwalimu mkuu, na hakuna kilicho fanyika, hiyo pesa aliipeleka wapi?
°Je kati ya mwalimu na mwanafunzi, ni nani anatakiwa kutumia madawati?
(Hiyo ni shule ya msingi na kuna wanafunzi wanakaa chini ila madawati yamerundikana staff room et walimu ndio watumie)