Waziri Mkenda hawa walimu walikosea nini hadi wapewe hii adhabu ya kuporwa madawati ya kukalia?

Waziri Mkenda hawa walimu walikosea nini hadi wapewe hii adhabu ya kuporwa madawati ya kukalia?

Hata kama mnadharau walimu ifike mahala waheshimike jamani.Upokonye walimu madawati ya kukalia kweli?Kosa ni Lao au la serikali?Kwa hiyo mitihani ya wanafunzi wanasahisha wakiwa wamekaa sakafuni au juu ya vitabu? Watu wanawafundishia watoto badala muwathamini mnawadharau,na wakiacha kuingia darasani?HII NI DHARAU KUBWA MNO KWA WALIMU NA WALIOFANYA HIVYO WACHUKULIWE HATUA
Kibaya zaidi wakiacha kuingia darasani wanafukuzwa kazi na hao wakurugenzi …hivi kweli mwalimu gani atapenda watoto wafaulu?
 
Mi sipendagi dharau kiukweli huwezi nifanyia huo upuuzi tena mtendaji sijui mwenyekiti wa kijiji Alooooooohh

Kitendo cha kukubali huo upuuzi Elimu haijawasaidia hao walimu kiukweli!

Afu sasahivi Kuna changamoto sana ya madawati mashuleni

Hii Elimu bure kuna sehemu imekwama
Walimu wanadharauliwa sana sana na wao wanakubali kabisa…..
 
Kama waliweza kumnunulia fomu ya uchaguzi mama inakuwaje washindwe kujinunulia viti vyao, usiwatetee hao, pia wapigwe marufuku kukalia vitabu kwani kutabu hakisomwi kwa makalio kinasomwa kwa macho.
Hao ni wajinga wajinga lakini hawa walimu hawana kosa la kuwafanya waadhibiwe kwa fedheha kabisa ….
 
Walipewa msaada wenye msaada wao wameyachukua wamejifunza kwa semaji haji manara mkigombana unachukua mali zako. wasubirie ya serikali
 
View attachment 2882455
Any connections with this discussions?
 
Hivi kumbe mtendaji wa Mtaa ni Boss wa Mwalimu, yaani kweli unamaliza ujana wako kusomea BAed kuja kuendeshwa na takataka za certificate zinazosubiri rushwa na hela za wauza viwanja ili ziishi.... ningemchapa kofi huyo mtendaji na kazi yake naacha apo
Mimi nawashangaa sana hata hap walimu walipata hata ujasiri wa kuendelea kusahihisha madaftari eti wamekaa juu ya madaftari………. Yani kama ningelikuwa wao nisingeyagusa kabisa hayo madaftari kisa hao so called takataka wa mtaaa….huu ni udhalilishaji wa kiwango chajuu hati wakae kwenye sakafu…

Hao taka taka kwenye ofisi zao za mitaa wana furniture nzuri tuu na kunafungu kabisa….aiseee kwakweli jua ni kali kweli kweli kwa Walimu…
 
Nchi hii ina watu wenye upeo mdogo wanapitwa hata na panya.

Inapoitwa shule masna yake;
Ina madarasa yenye madawati
Ina ofisi ya walimu yenye samani zake.

Kuna kenge maji zinagirojoka humu tu.

Sema waalimu hao pichani nao maandazi, mimi huninyang'anyi kiti eti niingie ofisini au darasani kufundisha
Hao walimu nao wameni dissapoint sana kwa woga wa kufukuzwa kazi hii ni aibu…..
 
Duh kuna walimu vilaza,ila mimi sio kilaza,kiti changu kingekuwa cha mwisho kupelekwa kwa wanafunzi baada ya kumung'oa jino mwenyeketi wa bodi/kamati yashule na mtendaji kurudi kwake akiwa na bandeji usoni.


Walimu tujitambue,tuache kuwa wanyonge.
Aisee ni fedheha sana wanafanyiwa..,
 
Mimi nawashangaa sana hata hap walimu walipata hata ujasiri wa kuendelea kusahihisha madaftari eti wamekaa juu ya madaftari………. Yani kama ningelikuwa wao nisingeyagusa kabisa hayo madaftari kisa hao so called takataka wa mtaaa….huu ni udhalilishaji wa kiwango chajuu hati wakae kwenye sakafu…

Hao taka taka kwenye ofisi zao za mitaa wana furniture nzuri tuu na kunafungu kabisa….aiseee kwakweli jua ni kali kweli kweli kwa Walimu…
Hao,wametaka waonekane.
Wanapenda kulialia&kutaka public sympathy.
Sijui ni kwa nini hawajipendi,hivi kweli hata furnitures tu wanashindwa kutengeneza kupitia fedha za elimu bure?
Maafisa wazima na elimu zao,wanafurahia kukalia madawati ya wanafunzi?
Aah...ni ajabu.
 
Back
Top Bottom