Kifimbocheza
JF-Expert Member
- Aug 7, 2008
- 494
- 121
Mwenye audio aweke humu ili tusikilize
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waziri aliyepewa dhamana na rais kupitia kwa wananchi wa jimbo la kilosa alimtukana mtangazaji wa wako redio wakati alimpomhoji maswala ya DECI. Alimtukana stupid na shenzi live redioni wakati anasikilizwa na watanzania wote.
Huyo ndiye Waziri wa Fedha, nani kampa jeuri hiyo?
Historia inaonyesha kuwa ndio kiburi yake hasa anapokuwa na madaraka. Wafanyakazi waliofanya nae kazi kote alikopita wanasema ndo hulka yake na kiburi
Je nani kampa hiyo jeuri ya kutukana!?
Ni rais au pesa?
Apparently Huyu ni mmoja wa watu wachache wanaozaliwa na kijiko cha fedha midomoni mwao.Huyu amebahatika kuwa sehemu nzuri tokea aanze kazi na mwishoni baada ya kustaafu akabahatika kurudi tena uwanjani kikubwa - uwaziri.
Ni bahati mbaya sana kama ameweza kutukana maana nimjuavyo ni mtu pleasant mwenye kutabasamu wakati wote.
Hili la DECI nadhani linamshtua ukiangalia kasheshe iliyotokana na sakata hili na hata yeye kidogo auingie mkenge kuizundua jimboni mwake huko Kilosa. Huyo mtangazaji kumuuliza kuhusu DECI ni kama kuongeza chumvi kwenye kidonda.
Nakubaliana nawe dada but ndo yamtoke matusi?..... He could behave better than that!
Dr dau hakuleta jipya pale NSSF yote yalianzniashwa na mhishimiwa sana mjinga,stupid mkulo dau aliyakuta.Waulizeni wakubwa walokuwa na mkulo pale nssf na sasa wako na dau.Tatizo la mkulo ni matusi pamoja na tabasamu ila mdomo wake umejaa matusi kwa wa chini yake.Alipoondolewa nssf alipauka hadi tukadhani tayari!!!! sasa ushikaji umemsaidia hadi kuwa waziri.Tanzania yetu hiyo hahahahahahahaaaaaaaaaaaa.Unakumbuka JK aliulizwa swali wakati alipopata Urais kuwa itakuwaje kwa wale washkaji wake walokuwa kijiweni akasema atakuwa anachati nao katika simu,ndo hiyo simu hadi uwaziri,hahahahahaaaaaaaaaa
Ni ubabe ubabe tu wa viongozi wetu walio wengi... kwani nina amini hayo maswali aliyoulizwa iwapo angeulizwa na chombo kama CNN au BBC maswali hayo hayo akiwa nje ya nchi au hata akiwa hapa hapa Bongo asingejibu kinamna hiyo, au basi angenyamaza kimya badala ya kumfyatukia anayemhoji.
Swala hili linaelezea aina moja ya dharau zilizokithiri dhidi ya wenyewe kwa wenyewe zinazo didimiza bara letu la Afrika.
Alimtukana stupid na shenzi live redioni wakati anasikilizwa na watanzania wote.
Huyo mtangazaji atakuwa stupid kweli kama hakuchangamkia ulaji huu na kubaki kulalama humu kwenye jamvi! Ushahidi anao. Anangoja nini?
Amandla.......
nakubaliana na wewe kama ushahidi upo, huyo mwandishi ashauriwe amshitaki!Anaweza kushitakiwa na kulipa fidia kwa kumdhalilisha mtangazaji akiwa kazini kama vile yeye akiwa pale wizarani halafu aje mtu amuulize kitu amtukane......anastahili kupelekwa mahakamani akalipe fidia ...................kwa kudhalilisha..tena kwa umma....sijui mnawatoa wapi watu kama hawa....ambao hawajui..............hata nini maana ya madaraka
na nyie waandishi muwe mnauliza vitu vinavyoendana na wakati,mtu yupo kwenye masuala ya bajeti we unamletea masuala ya deci,na unajua huku nako kalikoroga we ulitegemea nini na unabahati anapigaga vibao
Mkullo alisemaje, kama alivyotamka?
Defence attorney kashaingia sasa, maneno yanaombwa verbatim.