Waziri Mkuu aagiza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kutopewa mradi huku akimtaka Mtendaji Mkuu kujitathmini

Acheni utani, yaani hiyo floor moja ya nne na paa moja la jengo la kuhifadhia vifaa ndio vina account ongezeko la karibu mara tatu???!!!!! Huyo QS aliesahau kuingiza hizo item kwenye BOQ kachukuliwa hatua gani for such negliegence

Ukute ni Eng ww unasema QS. Hakun mtathimini majenzi mjinga kama huyo. Kilichotokea walifanya Lumpsum kwasabab ya muda
 
Acheni utani, yaani hiyo floor moja ya nne na paa moja la jengo la kuhifadhia vifaa ndio vina account ongezeko la karibu mara tatu???!!!!! Huyo QS aliesahau kuingiza hizo item kwenye BOQ kachukuliwa hatua gani for such negliegence?

Kwa TBA hili si la kushangaza...

Kuna sehemu nondo za ghorofa moja za beam & 1st floor yoote zilisahaulika kwenye BOQ...

Mjengo ulikuwa wa Serikali...

Lilichua muda sana kukalimika na gharama zaidi...

Hi FALSE AKAUNTI ingeanza kipindi hicho tungejenga miundu mbinu mingi sana kwa gharama nafuu...
Mkuu hii TBA kupewa mradi bila tenda ndio force account
 
.”

Waziri Mkuu ameagiza mkandarasi atakayepatikana ahakikishe mradi wa ujenzi huo unakamilika katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa na lijengwe kwa kutumia mfumo wa force account.
Yani utumie mkandarasi alafu utumie force account?
 
Katika miradi ya ujenzi Kuna kitu wataalam wanaita variation. Lakini sijawahi ona variation ambayo inashusha BoQ kuwa ndogo. Siku zote huwa naona variation ambayo inafanya BoQ kuwa kubwa.

Kwasababu Variation inatokana na change of scope nafikiri umenielewa. Change hii mara nyingi anayesababisha ni client au washauri wake inapelekea kazi material nguvu kazi na muda kuongezeka hii huongeza gharama

Kwa hiyo ni wajibu Qs na PM wamradi kupitia hizi variation na kuhakikisha price haukuwa exaggerated pia kupunguza maelekezo kwa contractor yatakayopeleka gharamaa hizi iuibuka

Lakini client au washauri wake wanaweza kufanya Value Engineering ilikupunguza gharama za ujenzi
 
Acheni utani, yaani hiyo floor moja ya nne na paa moja la jengo la kuhifadhia vifaa ndio vina account ongezeko la karibu mara tatu???!!!!! Huyo QS aliesahau kuingiza hizo item kwenye BOQ kachukuliwa hatua gani for such negliegence?
Hawa TBA hutoa makisio madogo yasiyo na uhalisia ili kuitoa kabisa sekta binafsi kwenye hili eneo; ushindani halali ni muhimu kila eneo.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro ajitathmini kuhusu utendaji kazi wake huku akiwasimamisha kazi wakurugenzi watatu wa wakala huo.

“TBA tunaihitaji lakini watu wake wana shida. Hatuwezi kuwaacha, TBA wasipewe miradi kwa sababu hawawajibiki na wanadhani kwa kuwa ni taasisi ya Serikali ndio wataachwa wafanye mambo ya hovyo.”

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi wakurugenzi hao leo (Jumatatu, Novemba 18, 2019) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi, Arch.Humphrey Killo, Kaimu Meneja wa Miradi, Abdallah Awadh na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushauri Arch. Hamis Kileo.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika miradi mbalimbali waliyopewa na Serikali ukiwemo ujenzi wa jengo la NEC ambalo ujenzi wake ulianza Julai, 2017 na ulitakiwa ukamilike Juni 2018 kwa gharama ya sh. bilioni 13. Hata hivyo mradi huo bado haujakamilika na ujenzi wake umesimama.

Akiwa katika eneo la mradi wa ujenzi wa ofisi ya NEC Waziri Mkuu alihoji sababu za mradi huo kutokamilika kwa wakati ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi alisema jengo hilo limeshindwa kukamilika kwa sababu wakati walipokuwa wanaanza kazi walibaini kuwa kuna vitu vilisahaulika wakati wa uandaaji wa Bill of Quantities(BOQ). TBA ndio waandaaji wa ramani ya jengo hilo na ndio wajenzi.

“Bajeti ya awali ilikuwa sh. bilioni 10 wakati wa uandaaji wa michoro ya ujenzi gharama ziliongezeka na kufikia sh. bilioni 13 ambazo ndizo tulikubaliana katika mkataba. Wakati tunaendelea na kazi tuligundua kuna vitu vimesahaulika kwenye BOQ jambo lililoongeza bajeti ya ujenzi na kufikia sh. bilioni 32.” Amesema Arch. Killo.

Waziri Mkuu akahoji tena “kutoka sh. bilioni 13 hadi kufikia sh. bilioni 32 je unaona inakuja vizuri hiyo” sh. bilioni 10 hadi sh. bilioni 13 tena hadi sh. bilioni 32 inazungumzikaje hii na je mwenye jengo mlikubaliana naye? Awali mwenye mahitaji alisema ana sh. bilioni 10 sasa imefikaje 32 je mlimshauri muhusika kuhusu ongezeko hili?

Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi Arch. Killo alipotakiwa kueleza sababu za kuongezeka kwa gharama za ujenzi huo amesema waligundua tofauti wakati wakiwa kwenye eneo la ujenzi kwamba kuna kazi zilitakiwa zifanyike lakini katika mkataba hazipo na hawakuwasiliana na muhusika.

Miongoni mwa vitu vilivyosahaulika katika BOQ ya mradi huo ni pamoja na kutokuwepo kwa ghorofa ya nne katika jengo moja wanalolijenga katika mradi huo ambalo ni la ghorofa nane, pia hapakuwa na paa la jengo la kuhifadhia vifaa mbalimbali vya NEC.

Waziri Mkuu amesema miradi mingi inayojengwa na TBA katika maeneo mbalimbali imeshindwa kukamilika kwa wakati, hivyo amemwagiza Waziri wa NchiOfisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama asitishe mkataba huo wa ujenzi na atafutwe mkandarasi mwingine aje amalizie.

“Jengo la TAMISEMI lililopo katika mji wa Serikali limejengwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.7, nyie wataalamu gani na kwa nini tuendelee kuwaacha ndani ya taasisi? TBA hamfanyi kazi vizuri wakuu wa mikoa na wilaya wanalalamika majengo hayakamiliki ni Serikali gani itakayowavumilia, mmeshindwa kutambua majukumu yenu.”

Waziri Mkuu ameagiza mkandarasi atakayepatikana ahakikishe mradi wa ujenzi huo unakamilika katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa na lijengwe kwa kutumia mfumo wa force account.

Kuna mtu ameelewa kilichoandikwa hapo kwenye bold anieleweshe na mimi ngumbaru? Inawezekanaje jengo la ghorofa nane (8) likakosa ghorofa ya nne (4)?
 
Pepo anatoa Pepo mwenzake.
Serikali inajidanganya kwenye mambo mengi sana, Majaliwa anajua hilo ila JIWE NI KICHWA NGUMU.
MAJENGO yote wanapewa TBA, kwa nidhamu ya woga wakaamua kufanya quotation za chini, sasa wameingia field hali ni nyingine.
JIWE ameua ushindani, hakuna maana ya kuwa na makampuni binafsi huku FCC wakiwa wamekaa kimya.
 
Mi ningeshauri hiyo kandarasi apewe yule nguli aliyetujengea Hostel za Choo Kikuu kwa robo gharama
 
Kuna mtu ameelewa kilichoandikwa hapo kwenye bold anieleweshe na mimi ngumbaru? Inawezekanaje jengo la ghorofa nane (8) likakosa ghorofa ya nne (4)?
limekosekana kwenye quotation , yaani msanifu alipigia mahesabu ila akairuka hiyo ghorofa, nafikiri alikuwa amelewa
 
Kwa TBA hili si la kushangaza...

Kuna sehemu nondo za ghorofa moja za beam & 1st floor yoote zilisahaulika kwenye BOQ...

Mjengo ulikuwa wa Serikali...

Lilichua muda sana kukalimika na gharama zaidi...

Hi FALSE AKAUNTI ingeanza kipindi hicho tungejenga miundu mbinu mingi sana kwa gharama nafuu...
Kwa faida ya wengi, Nini maana ya Force Account???
 
TBA ni Class I contractor, meaning wana uwezo wa kila kitu ktk ujenzi wa majengo yote, yaani manpower, technology + financial capabilities. Sasa sijui kwanini TBA ni wazembe sanaaa sanaa, miradi kibao inashindwa kumalizika na gharama zao ziko juu sana sana, Mh. Rais pia alihoji pale Vingunguki ktk ujenzi wa machinjio ya kisasa yaani ghorofa 2 na basement 1 eti gharama ni Bil 14. Na wajenzi ni hao hao TBA, kuna uwizi pale sana inaonekana.. TBA gharama zao sijui wanatoa wapi, hatari sana, i wish i could be PM, hiiii hiiii TBA ningepitisha uchunguzi mkaliiii sana sbb hizi gharama na uzembe ningefukuza woteee alafu naajiri wapya haraka sana.. Hiii hiiii[emoji44][emoji44]
Mbona mnapenda kujidai mnajua wakati hamjui? Toka lini TBA akawa mkandarasi? Unaelewa maana ya mkandarasi?
 
TBA nafanya kila kitu, wacha ujinga wewe, usiwe kama mwakyembe digrii nne anazidiwa na ROMA darasa la 7 B kupambanua mambo
 
Mkuu Class A contractor ikoje hii kwenye mfumo wa CRB? Maana wao wana Class I, II, III -VII.

Hiyo Class A vipi wameanzisha utaratibu mpya wa kusajiri kampuni?
Huyo jamaa ni kichwa maji achana nae.
 
Wanatoa gharama ndogo kumfurahisha fulani kama kawaida halafu wanadai wamesahau kuorodhesha baadhi? Hapo hakuna kutumbua kwani wahusika ni wapendwa.
Kwa wenye kumbukumbu, hivi TBA si ndio walijenga hostel za UDSM kwa bllion 10!?
Na je, hili jengo la NEC waliloahidi kulijenga kwa hizo billion 10, kimwonekano na kiukubwa linalingana na hostel!? Msaada tafadhali kwa wajuzi wa haya mambo.
 
Back
Top Bottom