Waziri Mkuu aelezea ubadhirifu wa mamilioni uliofanywa Bohari ya Dawa (MSD), asema ataenda akiongozana na Polisi na TAKUKURU

PPRA kazi yake kuu hasa ni nini naona haifanyi majukumu yake ipasavyo
Tatizo watumishi wengi wa serikali/umma hawafanyi kazi kwa kufuata taratibu/miongozo ya kazi zao, bali hufuata matakwa ya wanasiasa (wenye maslahi binafsi). Ndio maana hata kwenye kesi ya Mbowe ulikuwa unasikia afisa wa polisi anaulizwa kuhusu vifungu vya PGO ambayo ni muongozo wa utendaji wao wa kazi lakini anasema hajui
 
Hapa MSD ubadhirifu wote ulisababishwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu yule Mwanjeshi Gabriel Mhidize,yeye kila kitu alikuwa anataka kifanyike Kijeshi na kuweka taratibu pembeni,hivyo wale wataalam wote waliokuwa sehemu ya Menejimenti ambao walikuwa wanapenda kufuata taratibu walikuwa ni Maadui kwake na alifanya mpango akawaondoa wote,binafsi nilisikitika sana kuondolewa kwa mtaalam mmoja somebody Pondamali,alikuwa anapiga kazi hasa na kufuata taratibu kitu ambacho Mjeshi Mhidize hakukipenda,matokeo yake ndio kukawa na Wizi sana,sisi Wafanyakazi wengine tukabaki tunaangalia tu,yule Mwananjeshi alikuwa na matatizo sana
 
Hivi alishwahi kumchukulia hatua yeyote hapa nchini? Kama maneno yake yangekuwa kweli. Leo ingekuwa inakaribia mwaka tangu trein ya mwendo kasi kuzinduliwa
Huyu haaminikiki, ndiye aliyetuficha wakati Magufuli amekwisha kufa akatudanganya eti alikuwa ofisini!! Ni mbwekaji mzuri lakini hana meno.
 
Asante Waziri mkuu
 
Uzuri mmepewa bunge na Kila kitu kwanini msipeleke hoja ya dharura na maazimio yachukuliwe kushughulikia wizi as per report ya CAG??

Mmeachiwa Kila kitu ila Bado mnalia lia? Tulidhani upinzani na mabeberu ndio wanatuchelewesha kumbe CCM wenyewe mnatukwamisha!!

Tunawasubiri 2025
 
Ccm ni mafiii tunataka rais FULL DICTATOR MZALENDO
 
Dawa aina moja bei ya iliyotengenezwa Kenya, Tanzania, India China nk zinatofautiana na ya UK ukubwa wa kifo na kusinzia. Sijui kwa mashine na vifaa vingine vya tiba kutoka hizo nchi ukinganisha na vya UK.
 
Kassim utauawa mapema! MSD, TANESCO, Bandari, nk ni vyungu vya asali alivyosema Makamba Sr.
 
Kwani hizo zabuni hazikushindanishwa? Hawakutumia mfumo WA manunuzi?
Kama hawajafanya hayo Wana shida.
 
Hawa Panya Road wangejua umuhimu wa katiba mpya wangekuwa na sababu ya kustrike kwakua ushujaa wanao.
 
Kuna uwezekano wa kuwa na matumizi mabaya ya fedha MSD lakini turudi nyuma na tuache kuwalaumu sana kwa kazi ngumu wanayo ifanya. Siku zote, Sera ya serikali imekuwa kuhakikisha kwamba huduma za afya zinawafikia wananchi katika makundi tofauti ambapo huduma huwa bure kwa watoto chini ya miaka mitano, wazee waliozidi miaka 60 na kadhalika. Kama taasisi MSD inatakiwa ipokee malipo kutoka kwa hospitali na vituo vya afya baada ya kuhakikisha kwamba wanapata dawa na vifaa tiba. Tatizo la MSD linaweza lisihusishwe sana na matumizi mabaya ya fedha bali ni shirika kushindwa kujiendesha lenyewe kwasababu ya kuidai serikali mabilioni ya fedha. Afya bure kwa wote ni maneno ya kutafutia kura, hali halisi haipo hivyo
 
Atoke aende wapi? Magomeni au Kariakoo?
Rais yuko bize na majukumu yake - Kassim Majaliwa

Mpaka leo sijawahi kumuamini tena
 
Hivi alishwahi kumchukulia hatua yeyote hapa nchini? Kama maneno yake yangekuwa kweli. Leo ingekuwa inakaribia mwaka tangu trein ya mwendo kasi kuzinduliwa
Nikuongezee

1. Report ya Kuungua Soko la Kariakoo

2. Kuungua soko la Karume

3. Mauaji ya kijana mfanyabiashara wa madini Mtwara yaliyofanywa na Mapolisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…