Waziri Mkuu aelezea ubadhirifu wa mamilioni uliofanywa Bohari ya Dawa (MSD), asema ataenda akiongozana na Polisi na TAKUKURU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amkute katika ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) Jumatatu saa nne asubuhi, baada ya kubaini madudu katika ununuzi wa vifaa vya matibabu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika ufunguzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma jijini Arusha ambapo ametaja gharama kubwa iliyotumika kununua vifaa hivyo tofauti na bei halisi za soko, na hivyo kupoteza fedha nyingi za umma na kuwakosesha wananchi huduma kwani vifaa vilivyonunuliwa ni vichache.

Akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi hayo kama vile ununuzi wa seti moja ya vitenganishi kwa ajili ya awamu moja ya kusafisha damu kwa shilingi 65,000, lakini wakanunua kwa shilingi 189,000.

Aidha, MSD walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

Ametoa mfano mwingine ambao ni kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini MSD wamenunua kwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

"Kwanini hili linatokea? kwa maslahi ya nani?" amehoji Waziri Mkuu

Kutokana na PSPTB kuwa na jukumu la kuwachukulia hatua wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaokiuka sheria, Waziri Mkuu Majaliwa ameiagiza kufika ofisi za MSD akisisiitiza kuwa serikali haiwezi kukubali hali hiyo kuendelea.

"Na mimi sitasita kwenda na Kamanda Sirro, na Kamanda Hamduni, ili washughulike na watu. Lazima tuanze na watu hawa wanaofanya kazi hii, wakae nje, hatua nyingine zifuate," amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa

Ameongeza kuwa pengine wasimamizi wa vitengo vya ununuzi na ugavi wanahitaji kuapishwa, kutokana na unyeti wa nafasi zao katika kutoa huduma kwa Watanzania.
Mbogamboga wamewafanya watumishi kuwaiga kuiba
IMG_20220505_184932.jpeg
 
Huyu haaminikiki, ndiye aliyetuficha wakati Magufuli amekwisha kufa akatudanganya eti alikuwa ofisini!! Ni mbwekaji mzuri lakini hana meno.
Katelefoni mwongo jamani, yaani majaliwa kajaliwa huyu baba kwa fix fix. Akiongea kama mtu kweli
 
Uzuri mmepewa bunge na Kila kitu kwanini msipeleke hoja ya dharura na maazimio yachukuliwe kushughulikia wizi as per report ya CAG??

Mmeachiwa Kila kitu ila Bado mnalia lia? Tulidhani upinzani na mabeberu ndio wanatuchelewesha kumbe CCM wenyewe mnatukwamisha!!

Tunawasubiri 2025
Nikweli tunawasubiri 2025
Lakini hao ccmmajizi wanaelewa sisi wananchi hatuna chetu kwasababu baada ya kupiga kura, jukumu la kuhesabu kura kituoni wanakabidhiwa ramadhani kingai+jumanne+mahita+wakuregenziccm
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amkute katika ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) Jumatatu saa nne asubuhi, baada ya kubaini madudu katika ununuzi wa vifaa vya matibabu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika ufunguzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma jijini Arusha ambapo ametaja gharama kubwa iliyotumika kununua vifaa hivyo tofauti na bei halisi za soko, na hivyo kupoteza fedha nyingi za umma na kuwakosesha wananchi huduma kwani vifaa vilivyonunuliwa ni vichache.

Akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi hayo kama vile ununuzi wa seti moja ya vitenganishi kwa ajili ya awamu moja ya kusafisha damu kwa shilingi 65,000, lakini wakanunua kwa shilingi 189,000.

Aidha, MSD walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

Ametoa mfano mwingine ambao ni kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini MSD wamenunua kwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

"Kwanini hili linatokea? kwa maslahi ya nani?" amehoji Waziri Mkuu

Kutokana na PSPTB kuwa na jukumu la kuwachukulia hatua wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaokiuka sheria, Waziri Mkuu Majaliwa ameiagiza kufika ofisi za MSD akisisiitiza kuwa serikali haiwezi kukubali hali hiyo kuendelea.

"Na mimi sitasita kwenda na Kamanda Sirro, na Kamanda Hamduni, ili washughulike na watu. Lazima tuanze na watu hawa wanaofanya kazi hii, wakae nje, hatua nyingine zifuate," amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa

Ameongeza kuwa pengine wasimamizi wa vitengo vya ununuzi na ugavi wanahitaji kuapishwa, kutokana na unyeti wa nafasi zao katika kutoa huduma kwa Watanzania.
Nikikumbuka ishu za BOT na wizara ya fedha walivyokurupuka na kuishia kuufyata naona ni maigizo ya makamera tu.
 
Mimi nataka kuliongelea hili kwa upana zaidi, ukiona kuna jambo kama hili limetokea na kuongelewa basi yako makubwa kama alfu moja yamefanyika na hao vidagaa tu haya mambo yako sana, sasa watakuja hao wanunuzi watasema sisi tumefuata utaratibu hii quote ndio ilikuwa ya chini na sheria zetu zinasema wa chini ndio anashinda kosa langu ni nini? Je kama quote zote zilikuja na huyo aliyeshinda ndio bei ndogo hao wengine wali quote kiasi gani? Najuwa hili jambo linaumiza kichwa na ndio maana nasema haya madudu yako makubwa zaidi ya haya hii ni kama uchaguzi inaitwa poll tu. Navyojuwa mimi kuna cost contro kuwa sisi tunakisia bei ina range hivi zikija quote juu sana mna cancel mnatoa bei elekezi na profit margin % sasa ukienda hivyo pia unaweza kuulizwa ukimpa huyu kwa misingi gani kwanini hakuna quote? Kuna haja ya kungalia mfumo mzima wa manunuzi serikalini maana kuna mawili hapa wafanyakazi wanapiga au wafanya biashara wanapiga pia kwa kujuwa pesa za serikali nzuri lakini mpaka ulipwe inachukuwa muda mtu anapiga hesabu zake pesa kama imekaa tu. Hawa jamaa wanaweza kushinda na kusema tumefuata process na huyo ndio alikuwa bei ya chini sasa tumpe wa juu zaidi? Huko serikali hizo ndio trend kitu cha million kitanunuliwa 10 kila idara ya serikali na uhakika na hilo.
 
Kwani hizo zabuni hazikushindanishwa? Hawakutumia mfumo WA manunuzi?
Kama hawajafanya hayo Wana shida.
Nilivyosikia mimi aliyeshinda zabuni ndio wa bei ya chini katoa hiyo sasa shida iko wapi? nakubaliana na wewe kama walienda sole basi lazima justification japo sidhani. Maswali yako machache ndio ya msingi ukiona process ilifuatwa na tumeishia huko basi jua uozo uko kila sehemu na process zetu zinahitajika kufanyiwa marekebisho makubwa.
 
Ukifuatilia kwa umakini unaweza kukuta gharama ni halali na zilipitishwa kwenye tenda na bodi ya zabuni na wala mkuu wa ugavi hana kosa.
Ana siasa nyepesi.
100% correct hakuna jipya hapo, hii ni technic kuwapoteza watu kwenye fuel trend kuonesha shida zetu zinaletwa huko kwenye manunuzi.
 
Ndugu Kassimu ni sound tu..vitendo sifuri
Sound kweli huyu jamaa unakumbuka lile jengo la tanesco jipya huko sijui bukoba alikuta kibanda cha mlinzi kimejengwa kwa mil17 na akawaka kama hivi lakini hadi leo hakuna aliyechukuliwa hatua
 
Hivi alishwahi kumchukulia hatua yeyote hapa nchini? Kama maneno yake yangekuwa kweli. Leo ingekuwa inakaribia mwaka tangu trein ya mwendo kasi kuzinduliwa
Umenikumbusha ripoti ya kuungua kwa soko la kariakoo
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amkute katika ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) Jumatatu saa nne asubuhi, baada ya kubaini madudu katika ununuzi wa vifaa vya matibabu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika ufunguzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma jijini Arusha ambapo ametaja gharama kubwa iliyotumika kununua vifaa hivyo tofauti na bei halisi za soko, na hivyo kupoteza fedha nyingi za umma na kuwakosesha wananchi huduma kwani vifaa vilivyonunuliwa ni vichache.

Akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi hayo kama vile ununuzi wa seti moja ya vitenganishi kwa ajili ya awamu moja ya kusafisha damu kwa shilingi 65,000, lakini wakanunua kwa shilingi 189,000.

Aidha, MSD walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

Ametoa mfano mwingine ambao ni kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini MSD wamenunua kwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

"Kwanini hili linatokea? kwa maslahi ya nani?" amehoji Waziri Mkuu

Kutokana na PSPTB kuwa na jukumu la kuwachukulia hatua wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaokiuka sheria, Waziri Mkuu Majaliwa ameiagiza kufika ofisi za MSD akisisiitiza kuwa serikali haiwezi kukubali hali hiyo kuendelea.

"Na mimi sitasita kwenda na Kamanda Sirro, na Kamanda Hamduni, ili washughulike na watu. Lazima tuanze na watu hawa wanaofanya kazi hii, wakae nje, hatua nyingine zifuate," amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa

Ameongeza kuwa pengine wasimamizi wa vitengo vya ununuzi na ugavi wanahitaji kuapishwa, kutokana na unyeti wa nafasi zao katika kutoa huduma kwa Watanzania.
Na yeye zile amburence zilizokuwa zimefichwa bandarini, atajichukulia hatua lini?
 
Wahusika wangekuwa wanafirisiwa, wao na ndugu zao lingekuwa jambo jema sana
 
Hivi viongozi wetu ni nani aliyewaambia kwamba watanzania wote ni wajinga? Umekuwa ukifura siku zote baada ya hapo hkn cha maana kinachofanyika. Mwaka jana ulifura sana Temeke khs usifadi wa ujenzi wa barabara ya kijichi mpk kigamboni. Baada ya kufura ni nini kiliendelea? Ni heri mkae kimya na kuendelea kulamba hiyo asali kuliko kuendelea kutuona kama sisi sote ni hamnazo.
 
Back
Top Bottom