Waziri Mkuu aelezea ubadhirifu wa mamilioni uliofanywa Bohari ya Dawa (MSD), asema ataenda akiongozana na Polisi na TAKUKURU

duu hii MSD ni jipu linaloligharimu hili Taifa
Hakuna cha jibu wala nini? Ni uzembe wa hawa hawa akina Majaliwa. Hivi kweli mnategemea kuona maendeleo kwa kuongozwa na watu kama hawa? Ni kipi waliweza?
 
Yaani unagundua tatizo badala ya kuamuru mhusika/wahusika kushikiliwa Leo unaagiza kukutana J3 kwa mantiki hiyo umewaambia wakabadili namba.
Tangu uanze kutusemea uongo hata mtoto wa skuli anakukimbia.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Huu ni mkwala mbuzi wala hakuna chochote. Hao kina Siro wenyewe wapigaji. Majaliwa mwenyewe mpigaji. Hamna lolote.
 
Hiyo MSD inabidi iwe ndani ya premises za ikulu maana imeshindikana kabisa.
 
Kwani hapo MSD si palikuwa panaongozwa na mjeshi?wabongo noma sana hawakuogopa hata zile gwanda
Mjeshi mwenywe ndo balaa sasa, kumbe huna taarifa; brigedia jizi sana lile liliamini watu wataogopa magwanda yake
 
Bahati mbaya taarifa hii Waziri Mkuu amedanganywa, vyanzo mbalimbali vimedokeza.
 
Taarifa za ubadhirifu ni nyingi kuliko hatua zinazochukuliwa. Si yo sifa kuripoti wizi bila ya hatua.
 
Daa! Inauma sana, tatizo Mkuu amebaki peke yake!
 

Anachojifanya anapambana nacho ndio kilichompitisha bila kupingwa kwenye uchaguzi wa 2020. Mtu ambaye yuko madarakani kwa njia zisizo za kiuadilifu, anapata wapi nguvu ya kuhoji wasio waadilifu wenzake? Tunaposema viongozi waingie madarakani kwa ridhaa ya umma, ni pamoja na kuwa na uhalali wa kuhoji haya. Kinachofanyika hao watendaji wanaamua kuwa wezi kwani viongozi nao wanaingia madarakani kwa wizi wa kura ili wapate ulaji. Na wao wanatumia nafasi zao kupata ulaji.
 
Asiishie Msd acheze na ripoti nzima ya CAG
 
Kwani hapo MSD si palikuwa panaongozwa na mjeshi?wabongo noma sana hawakuogopa hata zile gwanda
Fuatilia vizuri utakuta huyo mjeda ndio alikuwa mpigaji balaa.
 
....mawaziri na raisi wenyewe wanaapishwa na madudu kibao!!!

Naona ni kama kiki ya kuzima mambo ya inflation na issues za mafuta!!
 
Ukifuatilia kwa umakini unaweza kukuta gharama ni halali na zilipitishwa kwenye tenda na bodi ya zabuni na wala mkuu wa ugavi hana kosa.
Ana siasa nyepesi.
 
Hawa wanajuana vizuri na wanatumana wao kwa wao sijui
Haiwezekani kila zinapopigwa hela wanakuja hadharani kutuambia kuwa na hizo zimepigwa

Ikifika uchaguzi tu kampeni hela zipo tena
Nyie sawa tu dundulizeni tu

Halafu tunafarijiwa kwa kusikia “kamata huyu
Taku… mpo? Mchukueni huyu
 
Sasa mh. Waziri mkuu hapo msd hakuna tiss Wala mwana inteligensia wa kuwainform takukuru na tiss headquarter juu ya wizi unaotarajiwa kutoka ili uthibitiwe?
Au ndio madhara ya kuwaajiri watoto wenu wasio na weledi au uvccm chawa kwenye idara nyeti?
Waziri wa afya anasemaje kwani Hadi wewe uingilie kati? Basi sawa, mfagilie mbali na yeye Kwa kushindwa kuisimamia idara yake!
Mnajichora Kwa wananchi chukueni hatua bila kumuonea yeyote!
 

Huu wizi ni michongo yao Sisi tunaaminishwa tu kuna wizi bali ni hela zinakusanywa

Haiwezekani hatuambiwi huyu mkurugenzi kaiba au mkandarasi kaiba na kafungwa miaka 30 hakuna na hautasikia
Jiulize kwanini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…