Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wazanzibari wakati fulani wakisema kuwa Tanganyika imevaa koti la Muungano huwa nawaelewa.
Hivi Waziri Mkuu huwa anafanya kazi za Tanzania ama huwa anafanya kazi za Tanganyika ndani ya Tanzania?
Protokali inasemaje kuhusu Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu. Jee Waziri Mkuu anawajibika kwa Rais wa Zanzibar?
Katiba ya Zanzibar inatambua uwepo wa Waziri Mkuu wa Tanzania. Na inawezekana Waziri Mkuu akawa ni Mzanzibari?
Mamlaka ya Waziri Mkuu Kwa Zanzibar yakoje. Jee Waziri Mkuu anaweza kutoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na Wilaya wa Zanzibar na wakalazimika kuyatekeleza?
Waziri Mkuu kuitwa wa Serikali ya Muungano Tanzania, jee mamlaka yake yanaakisi utanzania ama utanganyika?