Waziri Mkuu aokoa mamilioni, atembea kwa miguu kwenda ofisini

Haya ni maigizo kuliko yale ya tuhuma za mil 10, yani only 200 metres inagonga vichwa vya habari...hii ni sehemu ambyo angekuwa anaenda kwa miguu kila cku..magari 6? Ya nini kwa mita 200.
 
Mimi nadhani labda umbali wa mita 200 watu wangeujua kwanza ni sawa na umbali gani.ndio waanze kujadili ameokoa kiasi gani, kwawasio fahamu mita 200 ni sawa na umbali wa viwanja viwili vya mpira wa miguu gori to gori.kwahiyo mm ninaona ni sehemu ya waziri kufanya mazoezi sio jambo kubwa mpaka la kutoa attention kwa jamii.au ndio hile tunaambiwa ata wakidondosha kijiko watu wanapiga makofi..?
 
Mshana hapa umekurupuka, unaandika na kujenga hoja kama wale villaza wa udom
 
JPM alitoka ikulu hadi wizara ya fedha kwa miguu ikawa ni stori kubwa. Sijui pana umbali gani pale?
 
Aisee ujue nilikuwa nakuheshimu sana
 
Mamilioni kiasi gani?? Taja digits..
Na wewe ulishawahi kumuona akitembea mara ngapi.../kila siku anatembea kuelekea ofisini?
 
Umbali wa kutoka Goli moja la mpira wa miguu hadi goli lingine kisha ukarudi hata kama ni kwa gari utatumia mafuta ya Tshs ngapi??

Labda tuanze hesabu zetu kwa style hii. Tufanye makisio/assumptions zile gari za msafara wa Waziri Mkuu zinaenda kilometa 7 kwa lita 1 ya mafuta. Na tufanye labda kila lita 1 inauzwa Tshs 2,000. Kwa hiyo kwa afuta ya Tshs 2,000 ambayo ni lita 1 zitaenda umbali wa kilometa 7.

Sasa basi kilometa 7 hizo ni sawa na mita 7,000. Kwa hiyo mafuta ya Tshs 2,000 ambayo ni lita 1 yanaweza kwenda umbali wa mita 7,000. Ndio kusema kwamba kila Tshs 1 inayotumika kwenye mafuta ina uwezo wa kuifanya gari iende mita (7,000 / 2000) = mita 3.5.

Au pia unaweza kusema kila mita 1 ina uwezo wa kuchukua mafuta ya Tshs 2000/7000 = Tshs 0.28. Yaani gari hizi kila zikisogea umbali wa mita 1 zinakua zimekula mafuta ya Cent 28. Na kama zitasogea umbali wa mita 200 basi zitakula mafuta ya Cent 28 x 200 ambayo ni kiasi cha Tshs 57.

Hizi gari kama ziko 7 basi tufanye zinakula mafuta ya Tshs 57 x 7 = Tshs 400 kwa zote saba kutembea umbali wa mita 200. Na kama zitarudi jioni basi itakua ni ara mbili ambayo inafikia Tshs 800. Labda tuseme na sababu zingine zingine basi zinakula mafuta ya Tshs 1,000 jumla kwa safari ya kwenda kumpeleka PM na kurudi nae jioni kwa siku moja.

Ili Msafara huu uweze kuokoa tuseme kiasi cha Tshs 1illion tu kwa hesabu hizi za Tshs 1,000 kwa siku basi inatakiwa uwe umetembea siku zipatazo (Tshs 1,000,000/ Tshs 1,000 kwa siku) = siku 1,000. Yaani PM akifanya misafara au siku 1,000 inayookoa Tshs 1,000 kwa siku ndio atakua ameokoa kiasi cha Tshs 1,000,000. Sasa hizo "mamilioni" zilizookolewa sijui itakua ni siku ngapi.

Mi naishia hapa, ila hizi hesabu zina assumptions zake mbalimbali, na pengine zinaweza kukuchanganya kama kwako hesabu ni tatizo.
 
kama hizo mita 200 ameokoa mamilioni ya fedha, siku alizokuwa anatumia magari kwa hizo mita 200 alikuwa anapoteza mamilioni mangapi? na je? ni leo tu ndio ataokoa hayo mamilioni au baada ya leo ataendelea kuyapoteza? kumbuka mita 200 ni sawasawa na urefu wa viwanja vya mpira wa miguu viwili
 
Sasa vumbi vipi? Kila akifika ofisini lazima kiwi....
 


Tanzania yangu imekuwa kituko, waziri mkuu kutembea kwa miguu mita 200 nayo habari ya kuripoti na kudai kuwa imeokoa mamilioni ya fedha? siku Rais atakapoamua kula wali kwa maharage na waandishi wa habari wakaona watadai ameokoa mabilioni ya pesa.
we are not serious
 
Ameokoa kiasi gani? acha mbwembwe

Kama huko Dodoma mnasema Majaliwa kaokoa mamilioni kwa kutembea kwenda ofisini basi huku Makonda ametumia mara mia ya hizo zilizookolewa huko kwa kwenda kuzurula na msafara wa magari ya serikali zaidi ya ishirini!! Sasa hapo kama nchi tumeokoa nini? Tafakari.
 

Sina tatizo na kutembea kwa miguu na kiukweli moja ya kazi ya miguu ni kutembelea. Sina tatizo na kubana matumizi. wasiwasi wangu wale jamaa waona mbali wamehusishwa na uamuzi huu? maana Mungu aepushie mbali likitokea lile ambalo taarifa yake huanza na "ilikuwa majira ya saa..... Waziri mkuu alipokuwa anaelekea... ghafla...." Zitaanza tume , itifaki, protoko na mambo kibao ambayo kwa kweli ni muhimu kuyazuia.
 

Na hayo magari yote yatamfuata ofisini kumrudisha nyumbani. Gharama zinabaki pale pale
 
Jamani me nina shida na jinsi ya kupata mkopo biasha yang ni ya matunda sasa kila sehem wanasema tin no naombeni ushauri na naombeni km kuna mtu anaweza kunikopesha kwa liba nipo tayar nipo kwenye hari ngumu nilisimama kutokana na matatizo nawaombeni sana jamani[emoji17]
 
NA UHAKIKA HUJAMUELEWA MTOA MAADA
Huyu jamaa hesabu zimempita kushoto labda hajui vipimo, Mita 200? Viwanja 2 vya Mpira wa miguu,wengine tunapoishi kwenda msalani 300M,jikoni 200M,uhani 250M yaani ni urefu wa mtoto kutamba kwa dakika kadhaa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…