Waziri Mkuu aokoa mamilioni, atembea kwa miguu kwenda ofisini

Waziri Mkuu aokoa mamilioni, atembea kwa miguu kwenda ofisini

Kutembea mita mia mbili kaokoa mamilioni ya fedha.....!!!
Hii sasa ni too much asee
 
Umbali wa kutoka Goli moja la mpira wa miguu hadi goli lingine kisha ukarudi hata kama ni kwa gari utatumia mafuta ya Tshs ngapi??

Labda tuanze hesabu zetu kwa style hii. Tufanye makisio/assumptions zile gari za msafara wa Waziri Mkuu zinaenda kilometa 7 kwa lita 1 ya mafuta. Na tufanye labda kila lita 1 inauzwa Tshs 2,000. Kwa hiyo kwa afuta ya Tshs 2,000 ambayo ni lita 1 zitaenda umbali wa kilometa 7.

Sasa basi kilometa 7 hizo ni sawa na mita 7,000. Kwa hiyo mafuta ya Tshs 2,000 ambayo ni lita 1 yanaweza kwenda umbali wa mita 7,000. Ndio kusema kwamba kila Tshs 1 inayotumika kwenye mafuta ina uwezo wa kuifanya gari iende mita (7,000 / 2000) = mita 3.5.

Au pia unaweza kusema kila mita 1 ina uwezo wa kuchukua mafuta ya Tshs 2000/7000 = Tshs 0.28. Yaani gari hizi kila zikisogea umbali wa mita 1 zinakua zimekula mafuta ya Cent 28. Na kama zitasogea umbali wa mita 200 basi zitakula mafuta ya Cent 28 x 200 ambayo ni kiasi cha Tshs 57.

Hizi gari kama ziko 7 basi tufanye zinakula mafuta ya Tshs 57 x 7 = Tshs 400 kwa zote saba kutembea umbali wa mita 200. Na kama zitarudi jioni basi itakua ni ara mbili ambayo inafikia Tshs 800. Labda tuseme na sababu zingine zingine basi zinakula mafuta ya Tshs 1,000 jumla kwa safari ya kwenda kumpeleka PM na kurudi nae jioni kwa siku moja.

Ili Msafara huu uweze kuokoa tuseme kiasi cha Tshs 1illion tu kwa hesabu hizi za Tshs 1,000 kwa siku basi inatakiwa uwe umetembea siku zipatazo (Tshs 1,000,000/ Tshs 1,000 kwa siku) = siku 1,000. Yaani PM akifanya misafara au siku 1,000 inayookoa Tshs 1,000 kwa siku ndio atakua ameokoa kiasi cha Tshs 1,000,000. Sasa hizo "mamilioni" zilizookolewa sijui itakua ni siku ngapi.

Mi naishia hapa, ila hizi hesabu zina assumptions zake mbalimbali, na pengine zinaweza kukuchanganya kama kwako hesabu ni tatizo.
Safi GT..
 
Isichukuliwe kama dhihaka! Isichukuliwe kama maskhara na furahisha genge! Bali ikupe fikra fikirishi ya huko tunakoelekea na dhana nzima ya kubana matumizi.

Akiripoti kutoka Dodoma mwandishi wa kituo cha WAPO RADIO, amesema wananchi wa Dodoma Leo wamesifu kitendo cha Waziri Mkuu cha kutembea kwa miguu UMBALI WA MITA 200 kutoka makazi yake-Ikulu ndogo ya Dodoma hadi ofisini kwake (zingatia mita 200)akiwa na walinzi wachache.

Kitendo hicho kimetajwa kama kitendo cha aina yake chenye UADILIFU kilichookoa MAMILIONI YA PESA ambayo yangetumika kwenye msafara wa magari yasiyopungua sita.
Tuupinge kwa nguvu zote huu upuuzi, mwendo wa mita 200 katika uhalisia wake mtu anaweza kupanda gari na msafara?

Je kama Leo imeonekana ni ajabu ina maana siku zote ndivyo ilivyo?
Je kutembea mita 200 ni kubana matumizi?
Ni habari za namna gani hizi jamii inapewa?
Ina maana Dodoma leo kuanzia asubuhi hakukuwa na habari nyingine zaidi ya hii?

Hii breaking news imeniacha na maswali mengi.
mbona unaandika kama umepagawa na pepo? unamsifu au unampondea? eleweka.
 
Jamani mita mia 2 si mtu anafanya mazoezi maana haitoshi hata kuzunguka uwanja mara moja, au ni km 2?
 
Maigizo at work, kutembea mita mia mbili unaita waandishi wa habari wakutangaze ulivyookoa mamilioni ya pesa? Angetuambia hizo milioni alizookoa ni kiasi gani ndo tungejua alivyobana matumizi.
kwahiyo lowasa hawezi tembea mita 200? sasa nimeona umuhimu wa kuhamia dodoma, ngosha go go go, watanyooka tu, waziri akihamia dodoma uza gari lake atembee.
 
Ntamuulizia wapi..?
Ww si ulimskia sema hayo mamilion ni mangapi au ni upunguani ulionao unakusumbua na mihemko ya kipuuzi tu?
Mimi na wewe ni nani punguani wewe mwandishi kakuambia waziri kaepusha mamilioni ya fedha unaniliza mimi milioni ngapi? Muulize mwandishi au Waziri ndie anaejua katumia sh ngapi? Pia hata ukijua itakusaidia nini?
 
Maigizo at work, kutembea mita mia mbili unaita waandishi wa habari wakutangaze ulivyookoa mamilioni ya pesa? Angetuambia hizo milioni alizookoa ni kiasi gani ndo tungejua alivyobana matumizi.
kwahiyo lowasa hawezi tembea mita 200? sasa nimeona umuhimu wa kuhamia dodoma, ngosha go go go, watanyooka tu, waziri akihamia dodoma uza gari lake atembee.
 
Wafanye na mazoezi jamani kutwa kwenye gari, wakistaafu wanapata shida sana sababu ya kulemaza mwili.
 
Isichukuliwe kama dhihaka! Isichukuliwe kama maskhara na furahisha genge! Bali ikupe fikra fikirishi ya huko tunakoelekea na dhana nzima ya kubana matumizi.

Akiripoti kutoka Dodoma mwandishi wa kituo cha WAPO RADIO, amesema wananchi wa Dodoma Leo wamesifu kitendo cha Waziri Mkuu cha kutembea kwa miguu UMBALI WA MITA 200 kutoka makazi yake-Ikulu ndogo ya Dodoma hadi ofisini kwake (zingatia mita 200)akiwa na walinzi wachache.

Kitendo hicho kimetajwa kama kitendo cha aina yake chenye UADILIFU kilichookoa MAMILIONI YA PESA ambayo yangetumika kwenye msafara wa magari yasiyopungua sita.
Tuupinge kwa nguvu zote huu upuuzi, mwendo wa mita 200 katika uhalisia wake mtu anaweza kupanda gari na msafara?

Je kama Leo imeonekana ni ajabu ina maana siku zote ndivyo ilivyo?
Je kutembea mita 200 ni kubana matumizi?
Ni habari za namna gani hizi jamii inapewa?
Ina maana Dodoma leo kuanzia asubuhi hakukuwa na habari nyingine zaidi ya hii?

Hii breaking news imeniacha na maswali mengi.
Kwa sasa Kipao mbele chetu kikuu i Shisha.
Hayo Mambo ya 200 Mitas hebu jaman mtupatie Break
 
Mimi na wewe ni nani punguani wewe mwandishi kakuambia waziri kaepusha mamilioni ya fedha unaniliza mimi milioni ngapi? Muulize mwandishi au Waziri ndie anaejua katumia sh ngapi? Pia hata ukijua itakusaidia nini?
Nikijua itanisaidia nini? Ona ulivyo jinga..
Hiyo ni kodi yangu na wewe tunayolipa lazima tujue jinsi inavyotumika! Sihtaji mjadala sana na mpuuzi kama wewe!
 
Nikijua itanisaidia nini? Ona ulivyo jinga..
Hiyo ni kodi yangu na wewe tunayolipa lazima tujue jinsi inavyotumika! Sihtaji mjadala sana na mpuuzi kama wewe!
Ndio hivyo yamebanwa mamilioni ukataka kadai risiti.
 
Nikijua itanisaidia nini? Ona ulivyo jinga..
Hiyo ni kodi yangu na wewe tunayolipa lazima tujue jinsi inavyotumika! Sihtaji mjadala sana na mpuuzi kama wewe!
Wewe pia jinga sasa kama ametembea ela imetumikaje kwa hayo matumizi unayoyataka
 
Duh yan mita 200 unasema. Ameokoa mamilion? Hizi ni zaidi ya zarau
 
Sasa mita 200 ni sehemu ya kutembea na gari ,au tusifu nini hasa watu wanapiga km 10 kufuata maji au kwenda shule
Ndio maana magonjwa ya ajabu hayaachi kuwaandama kwa kuendekeza uvivu

Halafu hawa ndugu zetu wa Dodoma dah wacha niishie hapa
 
Back
Top Bottom