Waziri Mkuu ashangaa Tanzania kuwa na wachambuzi wengi wa mpira huku haina kocha hata mmoja anayefundisha nje

Hakuna mchambuzi mwenye sifa hapa Tz,labda kidogo mimi hapa 🤣🤣
 
Wanatenda kutimiza wajibu wapate ugali.Kati yao waliyoena chuo cha ukocha hata miezi6 hawafiki nusu.Na ukiwambia haya leo waingiye uwanjani kuupiga utacheka.
 
wachambuzi ni watu wajuvi wa ufundi wa mpira, na kocha anatakiwa kuwa na vigezo hivyo hivyo...
Sasa wanauwezo wakutransfer kilichopo kichwani kwao kupeleka in practice kwa wachezaji ?
 
Muheshimiwa Kasim kaacha kuwatolea mfano makocha wote Duniani kuona Alteta na Arsenal ndo wanafaa kuwatolea mfano wa Arsenal tumefungwa kwasababu ya ubovu wa Alteta.
Mh. Kasim mchambuzi mwingine huyu hapa.

Enhee NAWATAFUNA hebu muelezee mheshimiwa waziri mkuu kwanini wewe sio kocha wa Arsenal.
 
Lakini hata hao wachezaji wa zamani ambao ni wachambuzi pamoja na kuwa na uzoefu wa kucheza kwenye mashidano yao, ni wachache sana wanaofanikiwa kufanya la maana katika mpira....mchambuzi /pundit kazi yake ni kutoa opinion huwezi kutegemea ukiwa na wachambuzi wengi ndio utakuwa na makocha wengi kama Waziri anavyoshangaa....ni vitu viwili visivyohusiana.

[emoji16][emoji16][emoji16].
Ibrahim masudi maestro.
Oscar Oscar.
Jemedari saidi kazumari
Jeff leah
 
Hata wachambuzi pia hatuna kuna wachambuzi wa matembele2 na maharage wachumia tumbo
 
1)Hata huko nje wachambuzi wamejaa tele.

2) Language barrier. Makocha wa Bongo Kiingereza, Kifaransa,kiarabu utata.

3) Burundi,Rwanda,Kenya mishahara midogo.
 
Hili sikatai. Ila nimeelezea jinsi Tanzania kulivyo na watu wa maneno kuliko vitendo. Kwenye mpira ndiyo hasa kama kuna laana. Watu wamekalia kufanya vitu kwa midomo na siyo vitendo. Na kuwa na wachambuzi wengi ni lazima kuwe reflected na mambo mengine kama uchezaji bora, ufundishaji wa kiwango kizuri etc. Kuwa na nchi iliyo specilize kwenye kuchambua soka tu wakati ina uchezaji na ufundishaji wa kiwango duni ni kituko kikubwa.
 
Sasa wanauwezo wakutransfer kilichopo kichwani kwao kupeleka in practice kwa wachezaji ?
Ni kuwaeleza tu, kwani makocha wana kingine zaidi ya kuwaeleza wachezaji mbinu
 
1)Hata huko nje wachambuzi wamejaa tele.

2) Language barrier. Makocha wa Bongo Kiingereza, Kifaransa,kiarabu utata.

3) Burundi,Rwanda,Kenya mishahara midogo.
Mzee kocha wa Yanga anajua Kifaransa tu, lugha sio ishu
 
Unajua kukosoa jinsi chakula kilivyopikwa ila wewe hujui kupika? Wewe utakuwa ni tapeli
 
PM yuko sahihi, ila uchambuzi na ukufunzi ukocha ni vitu viwili tofauti, na hao wachambuzi kuwa makocha sio kitu rahisi sana inahitaji kujifunza sana maana ukocha ni zaidi ya uchambuzi
 
Kwa hiyo mtu anaweza kukosoa jinsi mpishi anavyopika chakula ila yeye ukimpeleka jikoni hajui lolote? Huyo anajuaje sasa mpishi anavyokosea?
 
PM yuko sahihi, ila uchambuzi na ukufunzi ukocha ni vitu viwili tofauti, na hao wachambuzi kuwa makocha sio kitu rahisi sana inahitaji kujifunza sana maana ukocha ni zaidi ya uchambuzi
So mchambuzi anawezaje kumkosoa kocha kila wakati wakati yeye hajui lolote kuhusu ukocha? Au ni blah blah tu?
 
Ndo maana hatuna makocha...everyone's thinking ni an easy job.
Hao wachambuzi wanawezaje kumkosoa kocha kila wakati huku wakiwa hawajui lolote kuhusu ukocha?
 
Kwa hiyo mtu anaweza kukosoa jinsi mpishi anavyopika chakula ila yeye ukimpeleka jikoni hajui lolote? Huyo anajuaje sasa mpishi anavyokosea?
Kwahio sababu huwezi kutaga inamaanisha kwamba huwezi kutambua yai Viza ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…