Waziri Mkuu atoa maagizo, vizuizi barabarani vinasababisha ajali

Waziri Mkuu atoa maagizo, vizuizi barabarani vinasababisha ajali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekemea utaratibu wa uwekaji wa Vizuizi na vituo vya ukaguzi barabarani bila kuzingazia tahadhari ya usalama kwa watumiaji wengine wa barabara.

Waziri Mkuu amekemea utaratibu unaofanywa na baadhi ya Halmashauri kuweka vizuizi na vituo vya ukaguzi kwa kuziba barabara bila ya kuzingatia matumizi sahihi ya barabara na hivyo kusababisha ajali.

Ameeleza hayo, leo Disemba 06, 2024 jijini Arusha wakati akifungua Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), na kusisitiza kuwa mwenye dhamana kutoa kibali cha kuweka vizuizi na vituo vya ukaguzi ni Jeshi la Polisi.

“Jeshi la Polisi kaeni na Halmashauri, vizuizi vyao barabarani vinasababisha ajali, hakuna sababu ya Halmashauri kuweka kizuizi cha kuzuia magari, mwenye kibali hicho ni Jeshi la Polisi peke yake kwa ajili ya ukaguzi wa usalama”, amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.
WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.50.06_37e41305.jpg

WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.50.07_ccb1a543.jpg
Waziri Mkuu ameeleza kuwa kuna baadhi ya Halmashauri zimeweka vizuizi barabarani kwa ajili maafisa kukusanya mapato ambapo utaratibu huo umekuwa ukiathiri watumiaji wengine wa barabara na kusababisha ajali katika maeneo hayo.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Wahandisi na wataalamu wa miundombinu kuwa kiungo muhimu katika utekelezaji wa maelekezo hayo kwa kuendelea kutoa mapendekezo ya kitaalamu ya matumizi sahihi ya barabara ili kuhakikisha kuwa dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuifanya Tanzania kuwa salama zaidi kwa wote inatimia na inapewa kipaumbele.
WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.50.05_f1fb27f1.jpg

WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.50.06_973a787e.jpg
 
WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO, VIZUIZI BARABARANI VINASABABISHA AJALI.

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa amekemea utaratibu wa uwekaji wa Vizuizi na vituo vya ukaguzi barabarani bila kuzingazia tahadhari ya usalama kwa watumiaji wengine wa barabara.

Waziri Mkuu amekemea utaratibu unaofanywa na baadhi ya Halmashauri kuweka vizuizi na vituo vya ukaguzi kwa kuziba barabara bila ya kuzingatia matumizi sahihi ya barabara na hivyo kusababisha ajali.

Ameeleza hayo, leo Disemba 06, 2024 jijini Arusha wakati akifungua Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), na kusisitiza kuwa mwenye dhamana kutoa kibali cha kuweka vizuizi na vituo vya ukaguzi ni Jeshi la Polisi.

“Jeshi la Polisi kaeni na Halmashauri, vizuizi vyao barabarani vinasababisha ajali, hakuna sababu ya Halmashauri kuweka kizuizi cha kuzuia magari, mwenye kibali hicho ni Jeshi la Polisi peke yake kwa ajili ya ukaguzi wa usalama”, amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu ameeleza kuwa kuna baadhi ya Halmashauri zimeweka vizuizi barabarani kwa ajili maafisa kukusanya mapato ambapo utaratibu huo umekuwa ukiathiri watumiaji wengine wa barabara na kusababisha ajali katika maeneo hayo.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Wahandisi na wataalamu wa miundombinu kuwa kiungo muhimu katika utekelezaji wa maelekezo hayo kwa kuendelea kutoa mapendekezo ya kitaalamu ya matumizi sahihi ya barabara ili kuhakikisha kuwa dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuifanya Tanzania kuwa salama zaidi kwa wote inatimia na inapewa kipaumbele.
 
Attachments

  • WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO, VIZUIZI BARABARANI VINASABABISHA AJALI..MP4
    76.8 MB
  • WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.36.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.36.jpeg
    446.4 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.37.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.37.jpeg
    686.6 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.37 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.37 (1).jpeg
    361.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.37 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.37 (2).jpeg
    579.1 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.38.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-06 at 14.49.38.jpeg
    546.9 KB · Views: 5

View: https://m.youtube.com/watch?v=tNBr9QHB5nM
Tutaendelea kuwapatia updates.
Njaa za uhamiaji, Polisi na watu wa ushuru wa mazao kuweka barrier kizembe imesababisha watu kufa na kujeruhiwa.

Hivi vitendo vya kuweka vizuizi au barrier bila mamlaka husika kuchukua tahadhari zikemewe kwa sauti kuu.

Inatakiwa waweke koni, alama na kadhalika umbali mrefu ili kukinga ajali au kutengeneza eneo maalum ambapo magari yatachepuka na kufanyiwa ukaguzi wa uhamiaji, mazao au shuku wa wahalifu kwa usalama zaidi.

Lawama zote ziende kwa walioweka barrier kizembe katika mazingira hatarishi.
 
Back
Top Bottom