Waziri mkuu kashauriwa vibaya na sijui kama ana watalaam wanaoweza kuangalia mambo vema.
1. Kuna wanaopenda mlima au milima kwa ''hiking'' kwamba anatembea kupitia vinjia , miamba n.k. hiyo ndiyo raha yake.
2. Kuna wasioweza hiking lakini wanatamani wangepanda mlima.
Hapa kuna kundi la Walemavu, watu wenye magonjwa mfano, moyo , kisukari, asthma n.k.
Kundi hili linatumia Viberenge kupanda katika kupata starehe ya kufika juu na kuona mandhari.
Makundi haya hayaibiani kwa namna yoyote. Anayefanya 'hike' atakuwa na wapagazi tu wale wale hata kama viberenge vipo. Na wale wa viberenge hawatatumia wapagazi kwa namna yoyote
Faida ya Viberenge ni kuwa na wigo mkubwa wa watalii, wanaotembea na wanaotumia viberenge
Kama hoja ya Waziri mkuu ni ajira, hivi tukijenga SGR na kununua Bombardier wale wauza tiketi na wapiga debe wa stendi tutawapeleka wapi? Ni lazima kama Taifa tubuni njia za maana za kusaidia watu wetu kutoka umasikini na upagazi. Watoto wao wapo International schools Kenya na South, na wengine nje wakibukua University za Ulaya!
Pascal Mayalla JokaKuu