Mzeya usilete majibu mepesi kwenye suala muhimuNenda na helikopta au machela.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzeya usilete majibu mepesi kwenye suala muhimuNenda na helikopta au machela.
Majaliwa hajui . Inaelekea hana exposure. Watalii wengi bado watalenda kupanda kwa Maui. Kwao suala muhimu ni endurance ikiwamo kufika kileleni. Watu Kama hao hawawezi kupata hitaji lao kwa kuapanda na kiberenge. Mwaka juzi nilikwenda Cape Town na baada ya shuguli zangu niliamua kwenda kwenye Table Mount. Pale kuna option ya kupanda na cable cars na kupanda kwa mguu. Tulipokuwa tunanunua ticket niliona watu wengi wananunua ya kupanda kwa mguu. Mimi nikapanda na cable car. Hivyo PM asiwe na wasiwasi. Soko la wapanda mlima kwa mguu litendelea kuwapo kwa muda mrefu na halitakufa.Wachaga wana mambo ya kizamani sana!
Sasa hapo wachaga wamehusikaje? Ndio waliopendekeza viberenge vitumike? Wao hawataki hizo ajira za kuwa Porters?Wachaga wana mambo ya kizamani sana!
Mnashindwa kuelewa maana pana ya utalii. Kuna adventure tourism - watu wa kupanda kwa siku 8 wataendelea kuwapo na hao wa siku moja watakuwepo...kumbukeni kuna watu wenye matatizo ya afya lakini wanataka kupanda mlima...pia wako watalii wana budget ndogo au kubwa na muda mchache wa safari...hii ni fursa.Kabisaa.
Yani safari ya siku 8 ifanyike kwa 1 hour mlima utachukuliwa poa kama kichuguu tu na hautakua na value tena coz safari ya usd 2500 itafanyika kwa usd 100.
Safari ambayo ingewahusisha wafanyakazi 12 itakua inachukua mfanyakazi 1 tu.
Wanaccm hawaachiani maji ya kunywa mezani - KikweteWaziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wadau wanaopendekeza matumizi ya viberenge katika kupanda Mlima Kilimanjaro kutathimini kwa kina mpango huo ambapo ameonyesha kutoridhia mikakati hiyo.
"Nasikia mnataka kuweka kiberenge cha kupanda Mlima Kilimanjaro, mnataka kuua mlima? Mkiweka machuma ya kupanda mlima mtaharibu, nataka mje mseme wapagazi mtawapeleka wapi na hizo ndiyo ajira zao, endeleeni kulijadili hilo mje na sababu zilizo tosha,” amesema Waziri Mkuu.
Ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa akiwa Chuo Cha Ushirika Moshi katika kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathon mkoani Kilimanjaro, leo Jumapili Februari 27, 2022 alipokuwa mgeni rasmi.
Yuko sahihi kwani uharibifu mkubwa sana wa kukata miti utafanyika, ni wazi kutakuwa na barabara mbili ya kupanda na kushuka, pia muda wa watalii kukaa hotelini utakwisha na ajira za wapagazi zitakoma pamoja na wauza kahawa na vitu vya asili watakosa wanunuzi na mwisho watalii wa mazingira watasusa kuja kutokana na uharibifu utakaofanyika.
Kasema yataua Mlima.....! Hajasema yataharibu Mlima....upo sahihi,lakini simuelewi PM hoja yake ya kwamba machuma yataharibu mlima
Unapozungumzia hizo cable ondoa swala la wapagazi, kambi za kulala mlimani na siku za kulala hotelini.Kweli uharibifu wa mazingira unaweza kutokea, kama ujenzi wa njia za trolleys utafanyika. Economically, however, upo uwezekano wa negative impact kuwa minimal, kwasababu ya volume ya wapanda mlima kuongezeka. Wale watu ambao, for age or health reasons, sasa hivi hawawezi kuupanda huo mlima, nao watageuka kuwa wateja. Volume ikiongezeka sana, hopefully, wapagazi watakuwa absorbed na ukuaji wa shughuli za kiuchumi utakasababishwa na hilo ongezeko.
All in all, without data-driven analysis, it’s hard to gauge the economic viability of this contemplated move!
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wadau wanaopendekeza matumizi ya viberenge katika kupanda Mlima Kilimanjaro kutathimini kwa kina mpango huo ambapo ameonyesha kutoridhia mikakati hiyo.
"Nasikia mnataka kuweka kiberenge cha kupanda Mlima Kilimanjaro, mnataka kuua mlima? Mkiweka machuma ya kupanda mlima mtaharibu, nataka mje mseme wapagazi mtawapeleka wapi na hizo ndiyo ajira zao, endeleeni kulijadili hilo mje na sababu zilizo tosha,” amesema Waziri Mkuu.
Ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa akiwa Chuo Cha Ushirika Moshi katika kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathon mkoani Kilimanjaro, leo Jumapili Februari 27, 2022 alipokuwa mgeni rasmi.
Unapozungumzia hizo cable ondoa swala la wapagazi, kambi za kulala mlimani na siku za kulala hotelini.