Waziri Mkuu auponda mpango wa kutumia viberenge kupanda Mlima Kilimanjaro

Tuna viongozi chenga sijapata kuona, sasa mbona wanajenga reli ya umeme, dar dom itakuwa masaa mawili sijui ma3 wenye basi watenda kuka wapi!? Wangtoa huduma ya simu tuendelee kutumiana barua kwa shirika la posta.

Haya ndio madhara ya teknolojia, hayakwepeki.
 
Wanaopandaga milima wanapanda kwa sababu ni challenge au adventure fulani, sio kwa sababu tu wanataka kufika kileleni. Wakiwekanviberwnge watavipanda wenyewe, wazungu walishaanza kuipinga hiyo idea zamani tuu, sasa kama wateja wenyewe hawaafiki kwa nini wanataka kuendelea na huo ujinga
 
Tutatoka kwenye advanture safari kuwa matembezi, advanture safari si kupanda mlima peke yake, ni pamoja kuona mabadiliko ya uoto kwenye mlima kulingana na kina, kujipima ukakamavu wa mwili wako, kupiga kambi njiani, kukutana na watu aina tofauti na kufahamiana na matukio njiani, mambo ambayo cable haikupi. Ninaamini cable itapunguza idadi ya watalii ambao wengi wao lengo si kufija juu tu ni pamoja na advanture safari, tunaweza tukajikuta tuna wapiga picha za harusi, siku ya kuzaliwa na kuvishana pete kuliko watalii ambao wanamnyororo mrefu wa mapato.
 
Waziri mkuu kashauriwa vibaya na sijui kama ana watalaam wanaoweza kuangalia mambo vema.

1. Kuna wanaopenda mlima au milima kwa ''hiking'' kwamba anatembea kupitia vinjia , miamba n.k. hiyo ndiyo raha yake.

2. Kuna wasioweza hiking lakini wanatamani wangepanda mlima.
Hapa kuna kundi la Walemavu, watu wenye magonjwa mfano, moyo , kisukari, asthma n.k.
Kundi hili linatumia Viberenge kupanda katika kupata starehe ya kufika juu na kuona mandhari.

Makundi haya hayaibiani kwa namna yoyote. Anayefanya 'hike' atakuwa na wapagazi tu wale wale hata kama viberenge vipo. Na wale wa viberenge hawatatumia wapagazi kwa namna yoyote

Faida ya Viberenge ni kuwa na wigo mkubwa wa watalii, wanaotembea na wanaotumia viberenge

Kama hoja ya Waziri mkuu ni ajira, hivi tukijenga SGR na kununua Bombardier wale wauza tiketi na wapiga debe wa stendi tutawapeleka wapi? Ni lazima kama Taifa tubuni njia za maana za kusaidia watu wetu kutoka umasikini na upagazi. Watoto wao wapo International schools Kenya na South, na wengine nje wakibukua University za Ulaya!

Pascal Mayalla JokaKuu
 

Hii concern yako siyo kitu cha kushangaza. Ni kawaida yetu binadamu kuwa na hofu juu ya namna mpya ya kufanya mambo yetu. Ukweli ni kwamba sisi hatuwezi kuwa wa kwanza kuwa na trolleys/cable cars. Kwingine pia zipo na hazijaathiri experience ya watalii kiasi cha kupunguza idadi yao na revenue. Remember, hizo cable cars zimetengenezwa with the rider experience in mind. More importantly, hiyo ni investment kubwa inayohitaji economic justification. Obviously, return on investment ni kitu cha kwanza kufikiriwa. Vilevile, kama cable cars zingekuwa zinaumiza local economies, hakuna mahali wangetaka kuwa nazo!
 
Huenda tunatofautiana kwenye kujua kwanini watu wanapanda mlima Kilimanjaro, huenda tungeijua sababu basi wote tungeongea lugha moja.
 
Cable cars zitaongeza idadi ya watalii, wanaopanda kwa miguu wataendelea kuwepo na ndio watakaokua wengi.

Tusifananishe jengo la ghorofa lenye lift na ngazi, utalii wa kupanda mlima unafurahisha kuanzia mwanzo wa safari mpaka kufika kileleni.
 
Huyu jamaa naye anaishi sijui karne ya ngapi hapa duniani?
 
Siku zote silaha na utajiri wa maskini ni matusi. Na utakufa ukiwa mpagazi. Maana hakuna namna. Wenye hela tunasubiri hivyo viberenge vya umeme vianze ili tuje kutalii.
Wenye hela utakuwa wewe..au ndo wale matajiri wa nyuma ya key board 🚮🚮🚮 Mi sio mpagazi, mi ni mtalii wa ndani. Mlima nimepanda for fun hadi kileleni...na mbuga zote za wanyama za kaskazini nimetembelea, namaanisha zote, nimetembelea. Na wanyama wote nimeona. Wewe mwenye hela umeenda wapi?
 
Naunga mkono hoja, lack of exposure, kuwa ill informed na ushamba ni tatizo kubwa kwa viongozi wetu, ndio maana tunasisitiza viongozi wasafiri nje wakaone mambo huko duniani.

Hatua hiyo ita double au hata ku triple wapanda mlima, kwa sasa mlima unapandwa na mountaineers only, lakini waki introduce viberenge, kila mtu atapanda.

PM aende Uswisi akaone kwenye Swiss Alps au Uchina Mt. Everest, watalii ambao sio mountaineers ni wengi kuliko mountaineers .

Wale mountaineers ni watu wa adventures, wataendelea kuja na kupanda kwa 5-7 days, huku wale wapandaji wa viberenge for 2 hours wakipiga 10 trips per day, each trip 10 -,20 people!.

P
 
Naunga mkono hoja, lack of exposure, ill informed na ushamba ni tatizo kwa baadhi ya viongozi wetu.
P
 
Mambo lazima ya badilike, watakao panda kwa miguu na wapande viberenge ndiyo mambo ya sasa.
Kupanda milima kama hiyo ni mchezo kama michezo mingine hususani soka. Sasa ukianza kutumia viberenge au viroboti au dawa za kuongeza nguvu, hiyo inakuwa si soka tena.

Unatumia lift kupanda mlima kilimanjaro ìli ukaone kitu gani kilicho cha ajabu huko juu? Itafika mahali sasa watajenga na mahoteli ya kitalii huko juu ya mlima kilimanjaro.
 
point bora kabisa kwa kujibia essay ya consequences of using cable cars to Mt Kilimanjaro
 
Kichwani wewe utakuwa mweupe sn, kuna vilema, wagonjwa, watu wenye matatizo mbalimbali ambao hawawezi kutembea tu hata kwa kawaida sembuse kupanda mlima, kwanini isiwe option anayetaka apande na asiyetaka atumie kiberenge? mfano watu wamefunga harusi wanataka kupiga picha juu ya mlima wanaweza wakaenda kupiga picha na kurudi ukumbini, acheni mawazo mgando.
 
Ambao wako physically challenged na wanataka kupanda tunawasaidiaje?fikirieni vizuri mpaka mwisho
 
Ungejua huu mradi ni wa mwekezaji kwa 100% tena si mzaawa usingeongea haya. Wasiwasi wangu ni mikataba yenye tax holiday mpaka pale mwekezaji atakaporudisha inflated cost zake. Kama Tanapa wako serious watuwekee hapa framework ya huo mradi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…