Sooth na
Sikonge
Kuna hoja ya kutumia 'disapora' kwasababu ya uwezo wao huko walipo
Nakubali wapo Watanzania katika tasnia mbali mbali wanaofanya tusiyotarajia
Kagame amewatumia sana,wameleta culture mpya kukiwa tayari na culture ya kuwajibika na kuondoa rushwa
Nawafahamu Watanzania wengi, wahandisi, waandishi wa habari, madaktari, wahasibu n.k. wanofanya 'vitu' kwa wenzetu na wanaheshimika
Ujenzi wa rings unaweza kuwapa ikafanyika kama wanavyofanya huko waliko.
Tatizo, watakuwa 'frustrated' si kwa masilahi bali bureaucracy na rushwa
Kuna wataalam wa IT nje wangeweza kufunga vifaa 'polisi' kwa muda mfupi
na kwa ufanisi. Lakini je, wangewezaje ikiwa tunajua mradi ulihusisha vigogo? Mkataba 'umefichwa' inasemwa wamehusika ''wazito''
Mfano rahisi sana, nguli wa BBC aliletwa na kupewa shirika alibadilli.
Kweli katika muda mfupi sana watu wakaanza kutumia habari za shirika letu
Guess what! walimuondoa, hakukidhi mahitaji yao.
Huwezi kutumia disapora kwasababu 'inner circle' watakula wapi? Wanachotaka ni kampuni local ili wagawane mradi
Wagawane mradi kama ule wa machinjio ya Ruvu alioibua Mwigulu.
Nguzo zimesimama miaka nenda rudi, aliyepewa tenda, mhandisi, consultant, wenye kazi (halmashauri) wamegawana chao! ni wazawa hawa
Ili kukomesha upuuzi wa aina hii, local contractors wakae pembeni kwanza. Wajifunze maana ya kazi na si rushwa.
Tutumie Diaspora kwanza kwa kuwapa kazi moja kwa moja bila kupitia mauza uza ya bodi n.k. Najua kisheria itasumbua lakini sheria zinatungwa na watu!
Kuna nyakati lazima hatua zenye maumivu zichukuliwe
Mimi si mpenzi wala mashabiki wa 'wazawa' wanaoua wazawa wenzao kwa professional negligence inayotokana na corruptions and moral decay
Sipendi bodi kwani ni magenge ya ulaji tu, hayana masilahi na umma.
Futa bodi ya Wakandarasi, Injinia, Sumatra n.k.
Weka wazawa benchi wajifunze, tuache uzawa unaoua wazawa
Bodi hazina masilahi na umma ni maeneo ya kupatia allowance tu.