"Rev. Kishoka, post: 22904175, member: 18"]Nashukuru kwa majibu kuhusiana na master plans. Je tumeshawahi kufanya tathmini ya kweli (Serikali) kujua kwa nini mipango miji imeendelea kukwama?
Mkuu Tanzania hatuna upungufu wa sera, plan au wataalam.Tuna upungufu wa management na mfumo (system).
Upungufu wa management si knowledge bali kuna 'mdudu' corruption
Mipango miji inakwama kwasababu ya corruption na system isiyoweza kuzuia hilo
Mfano, je kulikuwa na Ulazima gani kuongeza Maghorofa katikati ya Jiji la Dar badala ya kupanua mji viungani na kujenga new Dar Es Salaam?
Tunarudi hapo juu, kwamba master plan ya Jiji inaeleza, lakini master plan haina nguvu kuliko vi-memo.
Kama kuna ujinga ni huu wa Dar kuwa na maghorofa katika mji wa zamani.
Infrastructure hazikuruhusu ujenzi wa maghorofa kwani zilikuwa designed 100 yrs ago
Vimemo vinasema wapewe vibali na vina nguvu kuliko plan yoyote
Tembea majiji makubwa duniani, kuna new city na old city.
Hakuna sababu kuwa na maghorofa makubwa kati kati ya Jiji tukiwa na ardhi bwerere
Swala ni pesa? kwamba hatuna uwezo? je kuweka foundation ya planya mji mpya na kuruhusu ujenzi wake kuendelea kutumia sekta binafsi hauko?
Suala si pesa wala uwezo. Ni failure ya system inayotokana na corruption tu.
Sikonge an Nguruvi3 mmeongelea Dom kuwa na multiple districts ambazo ziko designated kwa mambo maalum, can Dar adopt the same? How about Mwanza, Mbeya, Iringa, Kigoma, Arusha na Morogoro?Just curious..
Dar haiwezi kurudi katika hali ya multiple districts, ni beyond repair na gharama sana
Mbeya haipangiki kutokana na ujenzi wa hovyo. Mbeya ni ''big village''
Mwanza, yes inawezekana at least infrastructure zake haziharibika sana
Tena Mwanza wangekuwa makini ingelikuwa Jiji la nchi nne. Wanaweza
Arusha, kuna fursa. Wana eneo. Kosa ni ku centralize kila kitu karibu na AICC kama Dar
Siasa zinachangia, niliposikia EAC imeomba eneo na ikawa shida kuwapa kwa upuuzi tu
Morogoro, Wana infrastructure nzuri. Wanachotakiwa ni kuendeleza districts zilizopo Morogoro si mji wa kazi au biashara, ni ''Hub''kiunganishi cha kanda ya kati , nyanda za juu na mashariki. Moro wazingatie huduma za jamii kuliko utawala au biashara
Eneo la stendi mpya hadi Kingolowira linatakiwa kuendelezwa kukidhi haja ya 'Hub'
Tayari SUA kupitia Mzinga-Mzumbe ni academic district
Eneo la kati la mji liwe shughuli za utawala na starehe
Tanga. Ni mji uliopangwa vizuri sana na Wajerumani. Wanachohitaji ni ring roads kwasababu sasa hivi ni kama square kukiwa hakuna kiunganishi cha maeneo.
Wana eneo wafikirie kuhamishia shughuli maeneo Pongwe na Pangani Road n.k
Mkuu inawezekana , kinachokwamisha ni management tu ya ku organize haya mambo
Ili kufanikiwa mambo yafanywe kitaalam na system si mtu au watu kwa idea zao