Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza zawadi ya cheni aliyopewa mkewe iuzwe ili kujenga bweni la Wanafunzi Simanjiro

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza zawadi ya cheni aliyopewa mkewe iuzwe ili kujenga bweni la Wanafunzi Simanjiro

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1643378337705.png

MAJALIWA AAGIZA CHENI YA MKE WAKE IUZWE.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameishukuru kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary (T) LTD ya mkoani Manyara,kwa kumzawadia mkewe, Mama Mary Majaliwa mkufu wa Tanzanite.

Hata hivyo,Waziri Mkuu ameagiza mkufu huo uuzwe, ili ipatikane fedha,itakayosaidia kujenga bweni la wanafunzi katika moja ya shule zilizopo wilayani Simanjiro.

Waziri Mkuu amehitimisha Ziara yake ya Siku nne, Mkoani Manyara.

Source: Watetezi TV
 
Kipindi cha Mzee Mkapa, Mkapa akiwa Rais na Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi waliwahi kupewa dhahabu na GGM! Mkapa alipewa tofali na Magufuli koreo,sasa sijui waliyapeleka wapi hawa watu
Na siyo dhahabu iliyo katika model ya beberu 🐐?
(Jamaa alibeba akapeleka home hata hivyo)
 
PM yuko makini bana,kwa miaka hiyo aliyokalia hicho kiti huwez kumshikisha yai bovu kirahis rahis hvy😄😄aaayaaah!

Liuzen nyny wenyew na tusikie mmejenga bweni za watot wenu. Na tutahtaji kujua value for money ipo....!

Bwege snaa nyieee
 
Unless it was staged, sisi wanawake tunajijua vizuri sana.

😁😁😁😁

Hakuna rangi Mheshimiwa ataacha kuona. 🤭🤭🤣🤣
Am pretty sure PM ameepuka kujiweka kwenye deni na hao watu. A person anakupa Tanzanite later on atakupa bangili kisha atakuambia uwe mwenyekiti wa bodi baadaye anaanza kuomba favors.
 
Mke wake atakua kalazimishwa tu akubali waiuze hiyo zawadi.PM ni dikteta kiaina[emoji57]
 
Back
Top Bottom