Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasimamia nini?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasimamia nini?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Samia anasema anajenga uchumi.

Nani msimamizi wake mkuu?

Majaliwa? Au Mpango?

Tofauti ya awamu ya tano na sita kiuchumi ni ipi?

Centralisation ni moja ya mambo yalioua uchumi why decentralisation haifanyiki?

Why mawaziri bado wanaimarisha centralisation?

Mashirika yanaendeshwa na Utumishi.

Na Mawaziri wakurugenzi wote ni Rubber stamps.

Makusanyo yote serikali kuu.

Halafu wanapangiwa bajeti ambayo haitoshi.

Kwanini decentralisation haifanyiki kwa haraka? Tunaua uchumi huku bado tunasema tunafufua uchumi?
 
Haiwezi kua ghafla bin vuu uchumi ukakua subira inahitajika mkuu,lakin kwa nn tunayumba kama nchi ?hatuna mifumo imara kila anaekuja anakuja na yake kwa utaratibu huu hatuwezi fika popote.
 
Mkuu The Boss, wakubwa wapo busy kuufungua uchumi na kupambana na ugaidi nchini. Think tank ndani ya chama imeona ni vyema utekelezaji wa ilani ya chama yenye kurasa 303 iwekwe pembeni kwa muda ili kudhibiti kwanza tishio la agenda ya kigaidi yenye kubeba fukuto la madai ya katiba mpya hapa nchini.
 
Labda rejea nafasi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais. Hizi mbili haziko ngazi moja hata kidogo. Makamu wa Rais ni cheo kikubwa sana kuliko Waziri Mkuu. Samia anaweza kumfukuza Majaliwa lakini hawezi kumfukua Mpango kwa neno lake tu.

Hivyo, msimamizi wa mawaziri wengine wote ni Waziri Mkuu chini ya Rais na ndio muwakilishi wa Rais Bungeni (anazungumzia serikali yote). Hata hivyo, maamuzi yote ya executive branchi yanafanywa na Rais na by extension na Makamu Wake.
 
Labda rejea nafasi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais. Hizi mbili haziko ngazi moja hata kidogo. Makamu wa Rais ni cheo kikubwa sana kuliko Waziri Mkuu. Samia anaweza kumfukuza Majaliwa lakini hawezi kumfukua Mpango kwa neno lake tu...
Hoja yangu wala sio kufukuza mtu.

Hoja yangu hapa Nani anaesimamia hiyo kujenga uchumi?

Na kama moja ya mambo yalioumiza uchumi ni centralisation why centralisation inaendelea?Nani anaetakiwa kusimamia decentralisation?
 
Haiwezi kua ghafla bin vuu uchumi ukakua subira inahitajika mkuu,lakin kwa nn tunayumba kama nchi ?hatuna mifumo imara kila anaekuja anakuja na yake kwa utaratibu huu hatuwezi fika popote

Policy haziko clear
Tunendelea na policy za Magufuli za kila kitu hazina? Au mashirika yaanze kuwa independent?..yajiendeshe?Yawe na policy za wafanyakazi tofauti? Hazina inakusanya kila kitu?Au Wana Uhuru wa kupanga mipango yao?
 
Hoja yangu wala sio kufukuza mtu
Hoja yangu hapa Nani anaesimamia hiyo kujenga uchumi??
Na kama moja ya mambo yalioumiza uchumi ni centralisation ..why centralisation inaendelea?Nani anaetakiwa kusimamia decentralisation?
Unachotaka kifanya kifanyike ni possibly ni complete privatisation, kitu ambacho serikali haijaamua kukifanya. Serikali bado inaamini kwenye kushikiria na kuendesha vitega uchumi.
 
Mimi nauliza tu, why Raisi, Makamu wa Raisi na waziri mkuu at the same time?

Naamini kuna nafasi hapo haihitajiki, ni basi tu!
 
Unachotaka kifanya kifanyike ni possibly ni complete privatisation, kitu ambacho serikali haijaamua kukifanya. Serikali bado inaamini kwenye kushikiria na kuendesha vitega uchumi.
Hapana unless hauko informed
Ntakupeleka mfano
Zamani wakati wa Mkapa na JK
Mashirika mfano NHIF walikuwa
Wana ajiri
Wanachagua suppliers wenyewe
Wana kusanya hela ..
Wanafanya manunuzi
Wanaweka motisha kwa wafanyakazi wao..
Wanatengeneza vision za makampuni
Kupitia board zao wanajiendesha ingawa yalikuwa makampuni ya umma..

Alipokuja Magufuli akafanya centrelisation.
Hanunui chochote Hadi waziri aseme
Makusanyo yote yanapelekwa hazina.
Hawaruhusiwi kutoa tender lolote hasa kampuni binafsi..
Wakitaka ujenzi TBA
Ukitaka bima NHIF
Sijui ulinzi .Suma JKT..
Kuajiri . Utumishi..

Matokeo yake ndo uchumi kuyumba
Sekta binafsi kufa...n.k..

Sasa kaja Samia kasema anafufua..
Cha kushangaza centrelisation inaendelea
 
Hapana unless hauko informed
Ntakupeleka mfano
Zamani wakati wa Mkapa na JK
Mashirika mfano NHIF walikuwa
Wana ajiri
Suala la Ajira zote za serikali kupelekwa UTUMISHI nadhani ipikuwa ni maboresho na kupunguza malalamiko ya upendeleo
Alipokuja Magufuli akafanya centrelisation.
Hanunui chochote Hadi waziri aseme...
Bado uko kwenye maana yangu ile ile. Serikali bado inaamini inaweza kuendesha njia kuu za uchumi na kuanzisha vitega uchumi.

Ndio maana hata taasisi nyingi ulizozitaja hazikuanza wakati wa Magu, alizikuta na zinafanya kazi.

Issue iliyopo kutoendesha soko kwa ushindani, ambao kidogo huwa unapelekea ubora wa huduma na kupumua kwa sekta binafsi.

Na suala hili mara zote limekuwa linategemea utashi binafsi wa Rais, ndio maana licha ya mashirika hayo kuwepo tangu zamani lakini sekta binafsi zilikuwa zinapewa kazi
 
Back
Top Bottom