Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasimamia nini?

Ishu kubwa hapa si centralization wala decentralization. Tena kwa watanzania decentralization ni leseni ya vitaasisi huku chini kujitafunia hela ya umma wanavyotaka.

Mi siyo muumini wa mzunguko wa pesa unaotegemea loopholes na uzembe wa serikali katika matumizi ya pesa ya umma.

Tutafute vyanzo halisi vinavyokwamisha au vitakavyoboost mzunguko wa pesa na kukuza uchumi.

Kama ningeulizwa ningesema uimara wa sekta binafsi (private businesses, etc) ndio siri ya kukua kwa uchumi.

Tukizipalilia hizi sekta binafsi (kodi rafiki, n.k) tunaweza kupata matokeo tofauti.
 
Hoja yangu wala sio kufukuza mtu
Hoja yangu hapa Nani anaesimamia hiyo kujenga uchumi??
Na kama moja ya mambo yalioumiza uchumi ni centralisation ..why centralisation inaendelea?Nani anaetakiwa kusimamia decentralisation?
Binafsi ninamsamehe mzee Mwanakijiji, nahisi uzee umemshikiria vibaya, huyu mzee ni moja ya watu walionifanya nijiunge JF but since awamu 5 imeingia madarakani hadi sasa hivi, kabadirika sana
 

Naona hunielewi kabisa..
Unaposema toka zamani zamani ipi?
Policy ya Nyerere ilikuwa kila kitu serikali
Hakuna private sector kabisa wakati wa Nyerere..
Private sector yote imejengwa na Mwinyi, Mkapa na JK..

Sasa kama Magufuli kuna mambo alijaribu kurudisha kama ya Nyerere now hayupo
Lazima serikali iwe very clear .. policy ni ipi??

Serikali sio muajiri mkuu..unataka private sector waajiri lazima wasibaniwe..wapewe hiyo nguvu...
Huwezi sema taasisi zote za serikali walinzi watoke Suma JKT halafu unasema unajali private security firms..
Huo ni mfano Tu mmoja..

Huwezi sema NHC wajenge wenyewe kila kitu
Hadi kujifanyia auditing wenyewe halafu useme eti mnapiga hatua..
Client na company ni the same
Pesa inazunguka humo humo uje useme unakuza uchumi
 
Kazi iendelee acha kulalamika
 
Kwani kwa uzoefu wako wewe ni lini ccm waliwahi kufanya jambo la kimaendeleo likafanikiwa?
 
Nchi inaongozwa na watu wasio na vision mkuu. Na siku zote sifa kubwa kuu ya kiongozi bora sio vyeti ni vision. Kama hana maono ni ubatili mtupu.
 
Sera ya ujamaa ya CCM mpaka sasa ni ipi ?

Mashiruka ya umma kama NHIF, TBA, TASAC, NASACO, NHC, SUMA JKT yameanzawaka gani ?

Na je wakati hayo mashirika yakianzishwa na kufanya kazi hali ya sekta binafsi ilikuwaje ?
 
Sasa mbona unajipinga mwenyewe?
Private sector anaanzisha kampuni ya ulinzi
Anakuta kampuni zote za Umma zimepigwa marufuku kutumia kampuni ya ulinzi ya private sector. ..wanatakiwa wote watumie
Suma JKT....
Private sector wanaanzisha kampuni za Bima
Wanakuta marufuku watumishi wa umma kutumia kampuni binafsi za BIMA
Wote wako NHIF ..
Private sector Wana kampuni ya ujenzi
Wanakuta taasisi na makampuni wanajengewa na TBA mara JKT mara kile
Private sector hata garage Tu zipitie sijui TAMESA n.k..mradi kila sehemu serikali inabana bana inafanya yenyewe biashara
Biashara imebaki kwa serikali kwa serikali

Hapo Una boost vipi private sector?

Hata makampuni Tu ya kusimamia kuajiri watu ...hayatakiwi..
Serikali inasimamia yenyewe kupitia Utumishi..
 
Ipi tofauti ya Naibu Rais na Makamu waRais ?.

Makamu na Naibu hawafukuzwi na Rais
Chama au bunge..
Ila naibu anafanya kazi za waziri mkuu
Hivyo waziri mkuu hahitajiki
Kwetu Makamu ni kama President in Waiting
 
Reactions: Ame
Mkuu na wewe umekuwaje tena? mbona unacheza nje ya chaki?hebu msome vizuri the Boss kisha uje tena
 
Centralisation ni moja ya mambo yalioua uchumi why decentralisation haifanyiki?
centralisation ni mfumo wa kidikteta uliotumika karne za 18 hadi 19 - yaani mapato yote ya nchi yanakusanywa sehemu moja then ni mtu mmoja tu ndiyo anayefanya allocation na ndiyo anayekuwa kauli ya mwisho.

Huu mfumo katu hauwezi kuisogeza nchi mbele.
 
Lakini wewe unaongeza chumvi kidogo hivi la utumishi kuajiri linakosa gani?
 
KATIBA MPYA ndio suluhishi ya yote haya.

Bila kupigania katiba mpya tutaimba hayo maswali mpaka mwisho wa dahari.!
 
Uchumi haukui kwasababu ya wizi,uvivu, udokozi na ufisadi ndani ya serikali. Hizo nyingine ni sababu shirikishi tu.
 
Kwa vile umeoongezea nyama hoja sasa nimeelewa. Mwanzoni nilifikiri decentralization kwa maana ya taasisi a serikali (hasa zile zinazokusanya pesa) kujikusanyia hela, kujipangia matumizi na kutoa tu report huko juu tu kwamba tumekusanya hiki na tumetumia hivi.

Kwa muktadha wa unachokizungumzia nadhani ni jambo linaloeleweka. Sina ubishi nalo hata kidogo. Ifahamike tu kwamba ile centralization ya Magufuli ilikuwa ni ad hoc reaction kutokana na kile alichokishuhudia kwenye awamu iliyomtangulia. Ni kama mtu aliyekuwa ndani ya sytem huku moyoni akijiwazia kuwa akiwa Rais atatupilia mbali mambo aliyohisi ni ya ovyo. Kumbe akaja kuwa. Katika kutupa mambo ya ovyo akatupa beseni na mwana aliyekuwemo ndani yake.

Kuna baadhi ya mambo ya kurekebisha ili private sector irejeea na kuoperate bila kuleta ukakasi. Miongoni mwa ukakasi huo ni pale private sector inapokosa uaminifu na uadilifu katika mashirikiano yake na serikali. Inapotokea kwa mfano habari ikaleak kwamba taasisi fulani ya serikaili imeingia mkataba fulani wa kifisadi na kampuni fulani binafsi, wapo watu kibao dizaini za Magufuli ambao hawatafurahishwa na miendendo hiyo.

Mjadala uwe ni je ni namna gani bora ya kuejesha sekta binafsi itakayodili na serikali bila janja janja?

Sometimes nafikiri kwamba the onus is on the private sector kujiprove kwamba wanastahili, wanaweza na wanaaminika. Hawahitaji janja kuishi mjini.
 
Nchi hii kama una akili timamu na ukiacha ushabiki wa kisiasa basi ukiwaza Sana unaweza kulia.Ni kama nchi Haina dira na viongozi wapo kwa ajili ya kujinufaisha wao tu.
 
Mkuu hoja yako Ina mantiki sana.

Halafu hapo hapo wanataka kodi za ajabu ajabu kutoka kwa kampuni binafsi...!
 
Hoja yangu wala sio kufukuza mtu.

Hoja yangu hapa Nani anaesimamia hiyo kujenga uchumi?

Na kama moja ya mambo yalioumiza uchumi ni centralisation why centralisation inaendelea?Nani anaetakiwa kusimamia decentralisation?
Unachosema kina mantiki kubwa sana...Infact hizi serikali mbili ya local na central ni replication na hazijajitofautisha katika roles zake kama ilivyopaswa; kisha ina weak link ndiyo maana ile ya central iliyotakiwa iweze kushughulika na policies pekee the Dejure ime nyang'anya roles za ile ya local ambayo ilitakiwa kuwa defacto i.e operational yaani tendaji at production level...

Matokeo yake kuna power struggle na inefficient allocation of resources and utilization....The total sum ni mkwamo kwenye economic growth...Tunakuwa kwakua hakuna jinsi huwezi kukua kwakua growth ni natural lakini haipo programmed wala strategized...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…