Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kujiuzulu, kitengo cha majanga kimemshinda

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kujiuzulu, kitengo cha majanga kimemshinda

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Kijana wa miaka 25 anakufa bila kuugua Tena kwa uzembe wa kutookolewa

Nimeona jumbe za watu waliopo kwenye vifusi nimelia Sana

Mimi ni mwanaume lakini ukweli nimejaribu kuvaa viatu vya kijana mwenye miaka 25 ana mke na mtoto kamuacha nyumbani au kwa dada mwenye miaka 23 ana mme kamuacha

Unakufa ukiwa unaona inauma Sana

Bora wanaougua tunawauguza na wanakufa

Toka aondoke baba wa Taifa nchi hii haijawai kuwa serious kwenye majanga na vita

Nyerere alituvusha Vita ya kagera na janga la njaa Kali kuwai kutokea

Unajiuliza je kwa sasa nchi ikivamiwa itakuwaje? Uliona tu kashikashi za Mtwara watu walivyokufa!!

Mabomu ya Mbagala, mabomu ya Gongo la mboto watu walivyokufa kama inzi.

Tetemeko la ardhi bukoba, kuanguka kwa ndege bukoba watu walivyokufa kizembe.

Sasa ni mwendelezo huo huo hakuna utawala unajali kuhusu uhai wa raia

Vaa viatu vya kijana anayekufa akiwa na miaka 25 au 28 bila hata kufanya chochote hapa duniani Tena kwa uzembe tu wa watu

Hivi gorofa la 20×20 linafukuliwa kwa zaidi ya masaa 24 na bado linafukuliwa?

Waziri mkuu hii ni Mara ya ngapi unazengua?

Waziri mkuu must go pia na Rais lazima aondoke 2025

Hatuwezi kuendelea kuwa na watu ambao hawajui kesho itakuwaje hawana plan zozote za maisha ya watu wao

Ukweli majanga ya Tanzania ni madogo Sana Sana je tungekuwa Kama Japan Hali ingekuwaje?
 
Toka Jana Nina hasira Sana sijui itakuwaje weekend imekuwa ndefu Sana

Sina raha kabisa nasikia uchungu Sana

Ajira hamna vijana wanajitaidi kupambana lakini bado mazingira ya mapano yao hayawekwi sawa!!

Ili tukio limeniumiza Sana sana
Screenshot_20241117-102333.png
 
Aliyeweza Kujiuzuru Ni Nyerere (Ili achukue Nafasi ya Urais wa Tanganyika)..
Na LOWASA (kwa Ajili ya Uzalendo)
Lowasa Mzalendo ? Kwamba alichohusika nacho na kilichomuondoa na kuleta adha ya umeme kwa maelfu ya watu na ulaji kilikuwa ni cha kutunga ? Uzalendo ni kuhakikisha kilichotokea / kufanyika kisingefanyika before hand..., hayo ya kujiuzulu kuondoa uwezekano wa kufukuzwa hence kupata mafao yako kama kawaida sio Uzalendo was a Necessity
 
Lowasa Mzalendo ? Kwamba alichohusika nacho na kilichomuondoa na kuleta adha ya umeme kwa maelfu ya watu na ulaji kilikuwa ni cha kutunga ? Uzalendo ni kuhakikisha kilichotokea / kufanyika kisingefanyika before hand..., hayo ya kujiuzulu kuondoa uwezekano wa kufukuzwa hence kupata mafao yako kama kawaida sio Uzalendo was a Necessity
Lowasa Asingeweza Kufukuzwa!
Nani angemfukuza?
Una uhakika alihusika na Hiyo scandel??

Kwa sheria na Katiba Yetu kulibaki Hoja Moja tu Kuvunja baraza la mawaziri Je, Unafikiri Kuvunja Baraza la Mawaziri Ni kawaida??.

Ukitengua Uteuzi wa Waziri Mkuu, Kupitia Bunge inamaanisha Kuwa Ni partial Impeachments yaani Ni kama Huna Imani na Rais kwahyo..

Moja kwa Moja Rais angekuwa Na yeye Kwenye Mkumbo huo kwahyo isingeweza Kutokea Na ndo maana kwa Uzalendo wa lowasa Ilibidi aepushe hilo
 
Lowasa Asingeweza Kufukuzwa!
Nani angemfukuza?
Una uhakika alihusika na Hiyo scandel??
Kwamba Katiba inampa pingimizi yeye Kufukuzwa ? Turudi hata kwa Ndugai alivyojiuzulu, kwamba alifanya hivyo kama Mzalendo au angeshindwa kubaki kwenye kiti and to fight for his life? Au aliona atoke to sababu angeweza kuanza kupigwa mawe and since anaishi kwenye Jengo la Kioo huenda sasa hivi angekuwa ameshatupwa ndani kwa scandal zake za nyuma...

Scandal ilitokea under his watch na kuhusika kwake hadi akaone atoke sasa kama alikuwa hajui hili wala lile kwanini alitoka ? (Vyoyote vile hata kama sio direct lazima alihusika by association)
Kwa sheria na Katiba Yetu kulibaki Hoja Moja tu Kuvunja baraza la mawaziri Je, Unafikiri Kuvunja Baraza la Mawaziri Ni kawaida??.
Mara ngapi Baraza limeshavunjwa ? Hata Mwinyi tu nadhani alishavunja mara mbili...,
Ukitengua Uteuzi wa Waziri Mkuu, Kupitia Bunge inamaanisha Kuwa Ni partial Impeachments yaani Ni kama Huna Imani na Rais kwahyo..

Moja kwa Moja Rais angekuwa Na yeye Kwenye Mkumbo huo kwahyo isingeweza Kutokea Na ndo maana kwa Uzalendo wa lowasa Ilibidi aepushe hilo
Uzalendo kwa Rais au Uzalendo kwa Wananchi ? Ndio maana nakwambia angekuwa mzalendo yaliyotokea under his watch tena yanayohusu sekta ya Nishati na wellbeing ya kila Raia is not far from being a traitor to your country..

Ila ndio hivyo ashukuru sana kwa Chadema kumsafisha as at one time alijulikana kama mmoja kati ya mchwa waliolitafuna hili Taifa since beginning of time (Ila ndio hivyo Wanasiasa mwisho wa siku wanakwambia he was the best ever na mabaya yote haikuwa yeye bali wengine)
 
Kama kujiuzulu ianze nafasi namba moja kushuka chini. Wote wanawajibika kwa hili, watuambie bajeti ya majanga iko wapi wanayoipitisha kila mwaka wa bajeti. Kusema PM pekee hapana, ni serikali nzima hakuna kinachofanyika. Mgao wa umeme ushapiga hodi, maji ya bomba kuna watu wanayapata baada ya miezi 6.

Janga limetokea, wananchi wamefanya kwa ukubwa kuokoa, hiyo kamati ya majanga wanakula hela za bure, waajiriwe kina Omary waliookoa watu bila kuchoka. Tukimaliza manusura wa ajali, tumgeukie mwenye ghorofa. Ana kesi ya kujibu kuua, kuharibu mali za watu. Unachimbaje chini ya ghorofa na watu wanaendelea na biashara? Aliona hasara kulivunja, sasa hiki ni nini? Asiachwe, angekuwa China muda huu kishanyongwa.
 
Back
Top Bottom