Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Yapo jangwani kule nyuma ya nyumba mafundi wameyafanya toolbox yao kila fundi ana basi lake
 
Anapiga gamba; kobe yupo ndani salama salimini.
 
Huyu jamaa toka aseme uwongo akiwa Msikitini kule Njombe namuona ni msanii tu
 
Ngoja kwanza naona hapa kuna jambo la kijinga sana, kwahiyo tulikopa pesa ya kununua mabasi hatukukopa pesa ya kulipa tra? tunauza mabasi kwa mnada baada ya kukaa miaka minne na mkopo na riba ziko palepale, sasa huo mkopo anaulipa nani?

Hayo mabasi yamenunuliwa shs ngapi? na kodi ni shs ngapi? kama kanunua bus 60m mnamwambia alipe kodi 180m na bado ana deni la world bank hatamie nigeyaterekeza.
 
Yarudi kutoka wapi? Yalikuwapo humo humo. Jiulize mbona hawajawahi kununua mabasi? Kwanini hawataki kulipia Kodi yaliyoko bandarini ambayo hayauziki kwenye minada?
Jongoo Ni huyo mkurugenzi.
Upigaji haujawahi kukoma; ila ulikuwa unafanyika gizani. Awamu ya 5 ilizima taa ili raia wasione yanayofanyika. Tusubiri kuona maajabu ya miradi ya Chato.
 
Kaulizwa wameshashakaa vikao vingapi na hawasemi chochote. Kiukweli mwendokasi kuna upigaji sana
Kuna mheshimiwa mmoja aliambiwa na Mkuu wa Nchi kuwa amenunua gari la kifahari bila kufuata utaratibu. Akasimamishwa yeye na wenzake ili kupisha uchunguzi. Kumbe muda wote huo alipewa kibali na Ofisi ya WM. Hili asingeweza kusema mbele ya kadamnasi maana angeonekana kama anamtupia lawama WM.

Katika suala hili kuna mikataba imevunjwa ( hatuambiwi tatizo liko wapi na uamuzi wa kuivunja alifanya nani), Mkurugenzi anaulizwa kwa nini hajanunua magari mapya bila kuulizwa kama huo uwezo anao. Haya yote yangefanyika ofisini na kama kweli ataonekana ni mzembe na mpigaji basi angeondolewa kwenye nafasi yake mara moja. Hapa kama tatizo ni la kimfumo ( upatikanaji wa mikataba, upangaji wa nauli n.k) hata akija mwingine tutarudi hapa hapa.

Amandla....
 
kama ungekuwa mmoja wa anaetumia huu usafiri usingesema haya maana haujawahi kuwa bora hata siku moja
Mràdi ulikosewa tangu awali. Mràdi huo ulitakiwa utumie train za umeme za kuzunguka kwà kutumia barabara hizo hizo. Matokeo yake wakaenda kumtoa mchina shida kwà kununua mabasi ya kichina.pia train ya umeme nauli ingekuwa kidogo, pia uharibifu ni kidogo, kuzitawala ni rahisi pia,
 
samson sialikamatwa kwa uhujumu uchumi, sasa atalipaje kodi yuko jela? halafu kwani lazima tuweke msimamizi binafsi? situajiri DG wenyewe ili akituzingua tuzinguane!
 
Hujui kama jamaa wana mkopo mkubwa....
usirukie vitu usivyojua utapasuka msamba
 
Wachangiaji 90% kwenye huu uzi wanatamani zile enzi za kwapuaaaa, piga cha juu, nk zirudi!
Kassim Majariwa hata marehemu jiwe alikuwa anamgwaya,,,,subiri nione mziki wake!
 

Mnashauri yakifanyika utasikia private sector inanyanyaswa.

Private sectors ya kitanzania wapigaji tu
 
Upigaji haujawahi kukoma; ila ulikuwa unafanyika gizani. Awamu ya 5 ilizima taa ili raia wasione yanayofanyika. Tusubiri kuona maajabu ya miradi ya Chato.
Chato inarudi katika hali yake ya zamani ya Kijiji Cha ujamaa.
Aiseeh Mungu mkubwa. Ilibaki kidogo tu ujengwe uwanja wa mpira Kama kirumba pale.
Ile benki sijui Kama total deposit kwa siku inaingiza milioni.
 
Haina haja ya waziri mkuu kwenda kwa kushtukiza,angetuma wakaguzi wakague wampe ripoti then awapige fire. Kwa Tanzania hii atatembelea ofisi ngapi kwa kushtukiza?
 

Leo ni siku ya furaha kubwa kwangu toka tuondokewe na Jemedari wetu mpendwa mzalendo wa nchi yetu, Mfalme na mtetezi wa wanyonge, Hayati Rais John Joseph Pombe Magufuli, kuona waziri wetu mkuu Majaliwa Majaliwa kwa mara nyingine akichukua hatua ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye shirika la Mabasi ya Mwendo Kasi jijini Dar es salaam.

Pamoja na kuwa ziara ya waziri mkuu huyo kuchelewa toka nilipo toa malalamiko yangu juu ya mtindo na mwenendo wa ukataji tickets kwenye hivyo vituo vya mabasi ya mwendo kasi humu JF mwaka jana, ni kitu bado mimi nashukuru kwa kuona serikali inatimiza wajibu wake wa kusimamia mashirika ya umma.


Furaha yangu ingekuwa kubwa na ya kupindukia kupita kiasi kama ningeona mfumo mzima wa watu au watumishi walio husika na uchakachuaji wa mlolongo mzima wa ubadilifu na wizi wa fedha na mali za umma, mpaka wale wachapishaji na wauzaji wa hizo tickets na ma-engineer na mafundi wote wa magari ukiondolewa na kuajiliwa watu wapya ili liwe fundisho kwa watumishi wengine kwenye mashirika mengine ya umma ambayo nayo yana watendaji wa sampuli hiyo.

Haitakuwa haki wezi na wadokozi wanao shirikiana na viongozi wao wenye mamlaka katika kuliua shirika la umma, wakaendelea na kazi kwenye shirika hilo tena, kwani ikumbukwe kuwa mwizi ni mwizi tu na haitakuwa rahisi kwake kuacha tabia hiyo ya udokozi na ufujaji wa mali za umma kama ataendelea kuwa katika position hiyo hiyo.

Watu wenye fikra za namna hii ni watu ambao maendeleo ya ustawi wa jamii yetu kwao haijalishi. Ni watu ambao wameweka mbele maslahi yao binafsi kuliko maendeleo ya pamoja ya nchi yetu. Watu kama hao wanatakiwa kwanza waadhibiwe vibaya sana kiasi kwamna hata wengine watakao pata nafasi zao baada ya wao kung'olewa, isiwe rahisi kufikiria kufanya maovu ya aina hiyo. Majina yao yawekwe kwenye records za serikali ili wasipate tena nafasi za ajira kwenye mashirika ya umma.

Hali kama hii itakuwa pia ni fundisho kwa vizazi vyao nao watakapo kuja pata nafasi kwenye positions kama hizo ili itapo fikia wakati wa kutaka kutekeleza maovu hayo hayo ya ubadilifu wa mali za umma, kumbukumbu za mateso ya maisha waliyo yapata wakati wazazi wao walipo pata pigo la aina hiyo ziwajie na kuchukua mamamuzi ya kutotenda uhaini huo. Vinginevyo itakuwa ni matatizo ambayo yatakuwa yana jirudiarudia kila mara na hivyo kuchangia kufa kwa mashirika ya umma kama ilivyo kuwa huko nyuma.
 
Hili gonjwa la utumbuaji Jiwe ametuachia janga baya sana.Kwani ni lazima kujipausha kisiasa kutumbua watu,kwanini utawala wa sheria usichukue mkondo wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…