Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Leo ni siku ya furaha kubwa kwangu toka tuondokewe na Jemedari wetu mpendwa mzalendo wa nchi yetu, Mfalme na mtetezi wa wanyonge, Hayati Rais John Joseph Pombe Magufuli, kuona waziri wetu mkuu Majaliwa Majaliwa kwa mara nyingine akichukua hatua ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye shirika la Mabasi ya Mwendo Kasi jijini Dar es salaam.

Pamoja na kuwa ziara ya waziri mkuu huyo kuchelewa toka nilipo toa malalamiko yangu juu ya mtindo na mwenendo wa ukataji tickets kwenye hivyo vituo vya mabasi ya mwendo kasi humu JF mwaka jana, ni kitu bado mimi nashukuru kwa kuona serikali inatimiza wajibu wake wa kusimamia mashirika ya umma.
Furaha yangu ingekuwa kubwa na ya kupindukia kupita kiasi kama ningeona mfumo mzima wa watu au watumishi walio husika na uchakachuaji wa mlolongo mzima wa ubadilifu na wizi wa fedha na mali za umma, mpaka wale wachapishaji na wauzaji wa hizo tickets na ma-engineer na mafundi wote wa magari ukiondolewa na kuajiliwa watu wapya ili liwe fundisho kwa watumishi wengine kwenye mashirika mengine ya umma ambayo nayo yana watendaji wa sampuli hiyo.

Haitakuwa haki wezi na wadokozi wanao shirikiana na viongozi wao wenye mamlaka katika kuliua shirika la umma, wakaendelea na kazi kwenye shirika hilo tena, kwani ikumbukwe kuwa mwizi ni mwizi tu na haitakuwa rahisi kwake kuacha tabia hiyo ya udokozi na ufujaji wa mali za umma kama ataendelea kuwa katika position hiyo hiyo.

Watu wenye fikra za namna hii ni watu ambao maendeleo ya ustawi wa jamii yetu kwao haijalishi. Ni watu ambao wameweka mbele maslahi yao binafsi kuliko maendeleo ya pamoja ya nchi yetu. Watu kama hao wanatakiwa kwanza waadhibiwe vibaya sana kiasi kwamna hata wengine watakao pata nafasi zao baada ya wao kung'olewa, isiwe rahisi kufikiria kufanya maovu ya aina hiyo. Majina yao yawekwe kwenye records za serikali ili wasipate tena nafasi za ajira kwenye mashirika ya umma.

Hali kama hii itakuwa pia ni fundisho kwa vizazi vyao nao watakapo kuja pata nafasi kwenye positions kama hizo ili itapo fikia wakati wa kutaka kutekeleza maovu hayo hayo ya ubadilifu wa mali za umma, kumbukumbu za mateso ya maisha waliyo yapata wakati wazazi wao walipo pata pigo la aina hiyo ziwajie na kuchukua mamamuzi ya kutotenda uhaini huo. Vinginevyo itakuwa ni matatizo ambayo yatakuwa yana jirudiarudia kila mara na hivyo kuchangia kufa kwa mashirika ya umma kama ilivyo kuwa huko nyuma.

Ndio mnasema mama aongoze hadi hadi 2035?
 
Acha hizo mpigaji hutakiwi kunegotiate naye, Kama ana majibu sahihi ya maswali anayoulizwa hawezi kuaibika. Kama Kuna upigaji wanafanya acha waaibike hadharani mbele ya wananchi.

Haya mambo ya kuoneana aibu yalitutesa Sana awamu ya JK, sasa JPM ameondoka wapigaji wanadhani watapata nafuu kumbe Moto ni uleule.
Kwahiyo hizo shida zimeibuka kipindi cha mwezi mmoja baada ya maghufuli kufa?
 
Hili gonjwa la utumbuaji Jiwe ametuachia janga baya sana.Kwani ni lazima kujipausha kisiasa kutumbua watu,kwanini utawala wa sheria usichukue mkondo wake?
Punda aendi bila mjeledi,ndio tulivyo watanzania kazi yetu majungu, udaku, wivu sio wa maendeleo, husda na maneno mengi utendaji zero.
 
Punda aendi bila mjeledi,ndio tulivyo watanzania kazi yetu majungu, udaku, wivu sio wa maendeleo, husda na maneno mengi utendaji zero.
Wewe unawasema wabunge wakiingizwa na sabufa na wakubwa serikalini wakiongozwa na Tecno kitochi. Sisi wengine hatuko hivyo
 
Sio sana kama hawa private sector lazima kwenye ku procure watakuletea low quality equipments.
Na wanaopitisha hizo low quality equipments ni public servants. Na unaweza kukuta anafanya hivyo kwa sababu faida yote wamechukua public servants wasio waaminifu.

Amandla...
 
Na wanaopitisha hizo low quality equipments ni public servants. Na unaweza kukuta anafanya hivyo kwa sababu faida yote wamechukua public servants wasio waaminifu.

Amandla...
Ila jua hawa private wamezidi
 
Nadhani hili jambo ni lazima tuwe serious serikali imewekeza zama kujenga miundombinu ya mwendokasi hawa wanaondesha lazima wapewe watu wenye nia ya dhati ya kuendesha hii biashara haya mambo ua kupeana wakati hawana weledi hata mtaji ni shida hata SGR leteni kampuni international iendeshe huu mradi msije kurogwa mkawapa walewale waliouwa shirika la reli hawana jipya watauwa na hili.

Hakuna ruzuku toka serikalini yaendeshwe kibiashara na kujitegemea. Hawa wanaagiza magari halafu hawana pesa ya kodi si ukichaa huu.
 
Hii yote ni kwa sababu hatuna mfumo maalumu wa kuendesha nchi,rejea Asskofu Gwajima bungeni last week.

Waziri mkuu anajaribu kufata nyayo za boss wake wa zamani ili kuonyesha watanzania bado wanafanya kazi.

Sikatai ni jambo jema lakini bado tupo nyuma sana sana kama mambo yenyewe ndiyo haya.

Nilitegemea Rais Samia aje na ajenda yake ya kiutendaji kuliko haya mambo ya kujaribu kokopi na kupesti ili kuridhisha wananchi
bado sana.

Wewe unawasema wabunge wakiingizwa na sabufa na wakubwa serikalini wakiongozwa na Tecno kitochi. Sisi wengine hatuko hivyo
Umeona sasa!

Ukipelekwa kusimamia UDART au shirika lolote unafikiri utaleta maajabu gani kazi kujadili watu na vitu.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha mwendokasi eneo la gerezani na kukuta mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi, mtendaji mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya supplier na alieununua. Meneja huyo amesema mfumo mpya unajengwa na waziri mkuu kumuhoji inatumia miaka mingapi kukamilika?

Majaliwa amesema wanaibiwa mapato kwani wao wanatumia mtambo na wengine wanatumia mtambo mwingine na hawana namna ya ku-check.

Pia Meneja amehojiwa tangu aingie amenunua mabasi mangapi baada ya serikali kununua mabasi 140 huku mabasi yanayokadiriwa kuwa barabarani ni wastani wa 100.

Mtoa huduma ya mwendokasi aliagiza mabasi 70 ambayo yamekwama kuingia barabarani kutokana na mgogoro na waziri mkuu akasema anaenda kuyaona. Majaliwa amesema wananchi wanalalamika mabasi hayatoshi akitolea mfano Kimara watu wanaingilia dirishani na kuhoji mapato wanayokusanya wanapeleka wapi kama wanashindwa kununua mabasi.

Pia waziri mkuu amepita karakana ya Jangwani na sasa anaelekea Ubungo kuangalia mabasi yenye mgogoro

==========

UBUNGO: Kinachoendelea waziri mkuu anauliza hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa mabasi yaliyokwama ambapo mtu TRA anasema sheria inamruhusu kamishna kuya-donate au kuyaharibu na waziri mkuu amesema hawezi kupewa Shabiby kwasababu hayamfai kwenda Dodoma kwani ni kwaajili ya barabara za mwendokasi na sasa anauliziwa mwanasheria

Pia waziri mkuu anawaambia forodha waendelee kufanya minada ya mizigo iliyokaa kupita kiasi mara kwa mara ili kusafisha nafasi ya kuagiza mizigo mingine na kuwataka wabadilike kwani baadhi ya wateja wanalalamika process zinachukua muda mrefu

Kassim Majaliwa anasema pesa zilizotumika zimekopwa world bank na zinalipwa na mabasi yameletwa na mjasiriamali laiki ameshindwa ku-comply na sheria na sheria zimechukua mkondo wake tangu 2018 na kutaka kesho wakae waamue

Majaliwa amesema serikali inao uwezo wa kununua mabasi lakini tatizo ni usimamizi na hawawezi kumsimamia msimamizi ambae hawezi na leo amemuweka pembeni mkurugenzi wa fedha na mwingine anamuachia Rais kwani yuko kwenye mamlaka yake.
Mapato yanakusanywa kama ya Daladala unatarajia Kupata Makusanyo
 
The buses were never and will repeat never imported by a World Bank loans please stop spinning the yarns
 
Umeona sasa!

Ukipelekwa kusimamia UDART au shirika lolote unafikiri utaleta maajabu gani kazi kujadili watu na vitu.
Sina shida ya kuongoza udart or any govt ofis.
Bajaji zangu ninazosimamia zinatosha.
 
Kesho nitapanda Mwendokasi.

Maana Kwa hii Kiki ya Majaliwa leo, lazima kesho watazuga zuga kujifanya wameboresha Huduma.[emoji1787][emoji1787]

Ila Mr. PM usijisahaulishe, bado tunasubiri ufafanuzi Wa maelezo yako uliyotoa kwenye nyumba ya Ibada kumhusu Magufuli huku ukijua fika kuwa hayana ukweli.

Sipendagi kudanganywa Mimi.[emoji1787][emoji1787]
 
Amefanya sahihi. Kuhojo hadharani ni sahihi kabisa ila wananchi wajue kinachoendelea.
Kutumbua ndio inapaswa kufuata taratibu za kiutumishi.
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu. Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
 
Back
Top Bottom