peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Leo ni siku ya furaha kubwa kwangu toka tuondokewe na Jemedari wetu mpendwa mzalendo wa nchi yetu, Mfalme na mtetezi wa wanyonge, Hayati Rais John Joseph Pombe Magufuli, kuona waziri wetu mkuu Majaliwa Majaliwa kwa mara nyingine akichukua hatua ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye shirika la Mabasi ya Mwendo Kasi jijini Dar es salaam.
Pamoja na kuwa ziara ya waziri mkuu huyo kuchelewa toka nilipo toa malalamiko yangu juu ya mtindo na mwenendo wa ukataji tickets kwenye hivyo vituo vya mabasi ya mwendo kasi humu JF mwaka jana, ni kitu bado mimi nashukuru kwa kuona serikali inatimiza wajibu wake wa kusimamia mashirika ya umma.
Furaha yangu ingekuwa kubwa na ya kupindukia kupita kiasi kama ningeona mfumo mzima wa watu au watumishi walio husika na uchakachuaji wa mlolongo mzima wa ubadilifu na wizi wa fedha na mali za umma, mpaka wale wachapishaji na wauzaji wa hizo tickets na ma-engineer na mafundi wote wa magari ukiondolewa na kuajiliwa watu wapya ili liwe fundisho kwa watumishi wengine kwenye mashirika mengine ya umma ambayo nayo yana watendaji wa sampuli hiyo.Umeishia wapi mradi wa Commuter Trains Dar?
Naam! Naipongeza serikali ya ndugu zetu wakenya kwa kutambua umuhimu wa kuondoa kero za wananchi wao wanazopata kila siku ya Mungu kwenye misongamano ya magari barabarani kwa ku-introduce Commuter Rail Network mjini Nairobi. Uamuzi huu ni kitendo ambacho kinatakiwa kuigwa na kila serikali ya...www.jamiiforums.com
Haitakuwa haki wezi na wadokozi wanao shirikiana na viongozi wao wenye mamlaka katika kuliua shirika la umma, wakaendelea na kazi kwenye shirika hilo tena, kwani ikumbukwe kuwa mwizi ni mwizi tu na haitakuwa rahisi kwake kuacha tabia hiyo ya udokozi na ufujaji wa mali za umma kama ataendelea kuwa katika position hiyo hiyo.
Watu wenye fikra za namna hii ni watu ambao maendeleo ya ustawi wa jamii yetu kwao haijalishi. Ni watu ambao wameweka mbele maslahi yao binafsi kuliko maendeleo ya pamoja ya nchi yetu. Watu kama hao wanatakiwa kwanza waadhibiwe vibaya sana kiasi kwamna hata wengine watakao pata nafasi zao baada ya wao kung'olewa, isiwe rahisi kufikiria kufanya maovu ya aina hiyo. Majina yao yawekwe kwenye records za serikali ili wasipate tena nafasi za ajira kwenye mashirika ya umma.
Hali kama hii itakuwa pia ni fundisho kwa vizazi vyao nao watakapo kuja pata nafasi kwenye positions kama hizo ili itapo fikia wakati wa kutaka kutekeleza maovu hayo hayo ya ubadilifu wa mali za umma, kumbukumbu za mateso ya maisha waliyo yapata wakati wazazi wao walipo pata pigo la aina hiyo ziwajie na kuchukua mamamuzi ya kutotenda uhaini huo. Vinginevyo itakuwa ni matatizo ambayo yatakuwa yana jirudiarudia kila mara na hivyo kuchangia kufa kwa mashirika ya umma kama ilivyo kuwa huko nyuma.
Ndio mnasema mama aongoze hadi hadi 2035?