Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Watanzania,

Kwani sisi Watz tunataka kitu gani? Swali hili sina jibu lake kabisa maana kwa madudu yaliyopo serikalini - ni wazi kweli hatuwezi kuendesha mashirika yetu ya Umma.

Inauma sana kile sote tulichokiona, UDART, BRT pale jangwani. Najiuliza hatuhujumiwi kweli kwa maksudi kabisa au watz hatutaki kufanya kazi?

Mimi nashauri Tanzania tuanze kuruhusu wageni kufanya kazi ndani ya nchi yetu. Haiwezekani tuendelee kufanya ujinga kwa namna hii.

Kwasasa nimeelewa kwanini wawekezaji wanaajiri wakenya zaidi kuliko watz.

Hii ni aibu kabisa kwa Taifa.
 
Hii ya kusifia wakenya ndio umechemka Ila fahamu kiini cha tatizo sio watendaji bali ni watoa maamuzi.

Maaumuzi ya kuvunja mkataba wa Maxmalipo ndio umeleta kampuni kukosa weledi katika ukusanyaji wa mapato, na imepelekea kampuni kushindwa kulipia gharama mbalimbali.

Sasa nakushauri angalia nani aliyesababisha haya ndio utaelewa wa kumlaumu sio watendaji kabisa.

Tunaingiza siasa kwenye biashara, hilo ndio tatizo plus personal interests.
 
Acha kuzunguka mbuyu. Aliyeua mradi ni Magufuli kwa kuleta ujuaji wake na ugomvi wake na Kisena!
Ww Una Shida na Magufuli, mada Ni udhaifu Wa Management ya udart Ila Ww umekomaa na Magufuli Tu. Upuuzi Huu
 
Acha hizo mpigaji hutakiwi kunegotiate naye, Kama ana majibu sahihi ya maswali anayoulizwa hawezi kuaibika. Kama Kuna upigaji wanafanya acha waaibike hadharani mbele ya wananchi.

Haya mambo ya kuoneana aibu yalitutesa Sana awamu ya JK, sasa JPM ameondoka wapigaji wanadhani watapata nafuu kumbe Moto ni uleule.
Unamaanisha mabasi yameharibika baada ya JPM kufa?
 
Hivi huu ujuha wa kuvamiana na macamera bado upo awamu hii?
Ni CCM katika ubora wao wa kulinda LEGACY!
1618889130357.png
 
Yaani Waziri Mkuu naona hata yeye bado hajui tatizo la Mwendokasi hadi leo hii? Sbb anaenda DART as if yeye ni new comer ktk serikali, DART matatizo yake ni uongozi mbovu na serikali imekaa tu kimya, dawa ni kutimua mwekezaji feki, serikali isimamie kwa 100%
 
Mbezi tiketi unauziwa alafu yule anayekuuzia anaenda kusimama mlangoni unamuonesha anauchukua anashukachini kwenda kumuuzia mwingine. Watu wanapiga hela sana kwenye ticket.
 
Hata SGR, kama inakamilika, yatakuwa ni haya haya tu.
Hawana mipangilio madhubuti ya uwendeshaji sana sana ni siasa tu.

Watu tulipiga kelele zaidi ya miaka minne lakini hawakutusikiliza kwani wao hawasafiri kwa mabasi hayo.

Ila yawezekana Magufuli hakupenda kuingilia kati aliziba masikio,sana sana Jaffo alitulisha propaganda za serikali inampango.

Hiyo SGR inataka uwendeshaji usio na management ya zimamoto.
 
Hii miradi wanaiua wenyewe.

kule vivukoni ukiwa mtu wa kitengo unavuka free hulipi hata sent moja.

risiti zinakatwa lakini mashine hazisomi.

mm walipowatoa tu wale maxmalipo nikajua apa tayari tumeinamishwa.

cio bure lzm kuna wanaofaidika na upuuz huu.
Uwanja wa mkapa wenyewe mashine kitambo hazisomi!ticket ni mwendo wa manual tu.

Nchi hii ngumu twendeni hivyo hivyo tu

Ova
 
Yaani Waziri Mkuu naona hata yeye bado hajui tatizo la Mwendokasi hadi leo hii? Sbb anaenda DART as if yeye ni new comer ktk serikali, DART matatizo yake ni uongozi mbovu na serikali imekaa tu kimya, dawa ni kutimua mwekezaji feki, serikali isimamie kwa 100%
Mwekezaji feki ni nani hapo?

Ova
 
Tatizo la huyu anakopitaga huwa hamna impact yoyote. Kama kiki tu.
Iringa aliagiza Manispaa kuvunja kiholela mkataba na muwekezaji sasa hivi wanadaiwa mamilioni mahakamani.

Akasema DC wa Kilolo ni tatizo kwa kushindwa kushirikiana na watumishi wa chini yake ikiwa ni pamona na kuwapiga vibao, lakini DC hakuguswa hata kidogo mpaka leo yupo na ameanza kuwaziwa kupewa mkoa (uRC).

Matukio bila matokeo
 
Kama mtoa huduma bado ni samson group mjue hatuendi popote. Hao watapeli hawawezi kuaminika kutoa huduma nzuri. Kwanza sifa ya mwekezaji hawana wanategemea waibie serikali kwaza ndio wawekeze.

Lengo lao kuu ni kupata mali kwa kuiba mali ya umma kujitajirisha. Uwekezaji ni kuleta mtaji na ujuzi sio ubabaishaji mtu huna kitu.
Namshangaa waziri mkuu na serikali yake kufanya mambo kama hawamjui Robert Kisena & Co? kuna jamaa yangu walimuajiri pale lakini tatizo lake alikuwa anafanya kazi kama yeye ni mzungu fulani hakuchukua hata miezi mitatu walimfukuza.

Serikali ina vision yake na wao wana focus yakwao sijui lini tutafika.
 
Moja ya Mbinu za kivita zinazotumika nchini ni Under Capeti hakunaga Agenda au Interest za kitaifa. Mradi wa Mwendokasi ulivyokuja watu walishangilia na Wamiliki wa magari ya daladala wakaingia kwenye msoto fedha kupungua na kujiona hawajui.

Mashindano yakaanza hata yamilikiwe na nani taifa likaingia kwenye Elimu chini ya Uangalizi wa Mampuni ya Marekani Ambao ndio Wamiliki wa mabasi (Ambao mkifika kwenye hiyo vita huwa wanauwa hela na kusepa).

Kwa akili za kibongo na umiliki wa kushabikia uchawi ni muda wa kubinafsisha shirika lenyewe na kila mtu amiliki kagari kamoja Taifa lisonge mbele. Hata kampuni ya Marekani itatishia kuwa ni Muda wa Hicha kutawala DAR.... #sisi ni mashindano




#tag Vita ya Story
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema tangu Mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ulipoanza Mabasi yamekuwa yakipungua kutoka 140 hadi 85——-“Watendaji wapo tu ofisini wanapigwa na AC (viyoyozi) wananchi wanaumia, hatuna sababu ya kumbakiza Mtu kama hafanyi kazi”

Amesema wakala huo ulianzishwa na Serikali kwa ajili ya kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi lakini Viongozi hao wameshindwa kusimamia vizuri na hivyo kusababisha mradi huo kutoendelea vizuri.

Waziri Mkuu amesema mapato mengi ya Serikali yamekuwa yakipotea kutokana na uendeshaji wa wakala huo———“kwanini ukatishaji wa tiketi haufanyiki kwa njia ya kielektroniki kwa asilimia 100? , tiketi zinauzwa kwa vifurushi”

“Haiwezekani Watu wanafanya ujanjaujanja tu wakuja na tiketi zao za mfukoni halafu wakimaliza anauza za POS (Mashine ya Kielektroniki ya Kukusanyia Mapato) na Wasimamizi wapo tu, kwanini mnauza tiketi kwa vifurushi hamtumii mashine kukata tiketi, Mnaua wakala huu kwa sababu wauzaji wa tiketi wanakuja na tiketi zao na nyingine mnazileta nyinyi”———MAJALIWA
 
Wasimamishwe, wawekwe sehemu salama zaidi kuliko nyumbani kwao, wachunguzwe kisha wakibainika walipe.
 
Back
Top Bottom