Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri sana. Mimi sina shida na hilo hata kidogo. Lakini kwa huyu mama mh! Anaweza kuwa kiongozi mbaya kuliko Magufuli. Labda kitachachobadilika ni ukatili. Hailekei kuwa katili au kuminya demokrasia kama Magufuli lakini in terms of vision etc... mh. Sijui lakini. BTW haya ''mazungumzo baada ya habari'' tu kwani sidhani kama jamaa kafa kama wanavyosema.
 
Unapoelekea utasema nchi nzima hamna umeme!
Unapoelekea utasema Serikali bado inatengeneza vijiji ili ikopeshe milioni 50 kila kijiji maana mpaka sasa nchi hamna vijiji.
 
Wanataka azurure Magomeni au Kariakoo, siyo? Walizoeaga Rais wa kupishana angani kama daladala!!!!
 
We mwehu kweli kweli mkuu,samia hujamwona juzi kwenye tamasha la siku ya wamama Duniani???

Women's day March 8. Hiyo siyo juzi.

Mara ya mwisho wewe kumsikia ni juzi May 8?

Something is very fishy.

Kwa mustakabala wa wawili hawa ni kwa hali ya dharura mno tunahitaji sasa kusikia kutoka kwao moja kwa moja.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Dunia ya sasa imebadilika sana, watu wanapata taarifa pasipo kuhitaji kuitafuta, wakati nasoma shule ya ukitaka kujua habari yoyote iliyojiri duniani tulikuwa tunasogelea kijiwe cha mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa ndio anatupa story kuanzia za mpira, siasa na za kimataifa.

Leo ni tofauti sana, digitali imerahisisha, ndiyo maana PM Majaliwa anaweza kutumbuliwa leo ikiwa zaarani akikagua shamba la bwana Juma, Bwana Juma amkapashwa habari umetumbuliwa.

Huku mtaani habari inayotrend kwa sasa ni hali ya Rais wetu, kwenye socal media zote ni hilo tu, Mzee wangu kanipigia simu akijua mimi niliepo karibu na Magogoni nina taarifa zaidi.

Huenda mwanzoni watu walichukulia ni za uzushi kama uzushi mwingine tulioushuhudia siku chache zilizopita, Lakini waenga wanasema uongo usipotolewa majibu hususa kwa wakati basi hukomaa na kuwa kweli.

Jana kuna jamaa yangu kiongozi wa chama tawala Chato nilipoongea naye aliniambia amepokea simu zaidi ya kumi kwa issue hiyo, hali hiyo ilimpa hata yeye wasi wasi naye ameanza kuifutilia kwa karibu.

Pamoja na waziri kutoa majibu yalioacha maswali mengi, ndiyo kwanza ameibua upya hoja, watu wanaendelea kudadisi.

Kwa hali ilipofikia ni afya zaidi kwa nchi na raia zake kama kweli Rais ni mzima wa afya, Ni vema kupatarifa rasmi ya serkali, tena na kutoa onyo kali kwa vyombo vya habari vya nje na wote waliozusha taarifa hizo.

Hatua iliyofikia kuendelea kukaa kimya madhara yake ni makubwa kuliko tatizo lenyewe.

Kweli wanasambaza uvumi huu huenda wakawa wanavunja sheria lakini kutoa kutoa taarifa kwa taaruki hii wale wenye mamlaka ya kutoa taarifa wanavunja sheria pia.

Ni kweli kutoa taarifa za hali ya mkuu wa nchi kunaprotocal zake lakini kutoa taarifa za kadri ni haki ya raia pale ambapo wanataka kuzipata as long as hawafunji sheria katika kuzipaka ndiyo maana hijasikia wanataka kuandamana.

Asante hayo no maoni yangu.
 
Si watakuwa Magogoni au chamwino au na huko hawamo?

Za kuambiwa muhimu tuchanganye na zetu.

Watu hawa waongee na sisi.

Tunachohitaji ni kitu cha msingi sana.

Tafadhali wote wanausika na mtuelewe.

Ninaamini wawili hawa watafarijika sana kusikia hatuko tayari kupumzika bila kuwaona au kusikia kutoka kwao moja kwa moja.

Habari ndiyo hiyo.
 
Na siku salamu za rambirambi zikianza kutumwa toka nchi mbalimbali uje kuandika tena huu utumbo
 
We mwehu kweli kweli mkuu,samia hujamwona juzi kwenye tamasha la siku ya wamama Duniani???
Mwambie pia kesho kutwa J4 ya tar 16 yupo ziarani..ratiba tayari

Ni ziara ya siku sita

PM nae anarudi Mbeya kwenye shughuli
 
Umuofia Kwenu,
Leo Jiwe ameonekana ibadani au ndio bado yale mambo ya Yeye si parish worker?
 
Na siku salamu za rambirambi zikianza kutumwa toka nchi mbalimbali uje kuandika tena huu utumbo
Hakuna watu wasio na soni kama Wana Lumumba. Wanajua namna ya kubadili gia angani. Leo wanaweza kuongea hivi kesho wakabadili kama sio wao. Rejea: Maalim Seif kipindi cha kampeni na baadae alipoukwaa umakamu wa Rais!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…