Kifo unachomuombea mwenzio chaweza kukurudia mwenyewe
Maendeleo hayana vyama
Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Rais wetu John Pombe Joseph Magufuli [emoji173][emoji1241][emoji106][emoji111][emoji120]
Hivi kuna anaemwombea kifo Rais Magufuli...?
Watu wanauliza tu aliko maana si kawaida yake na pia huyu ni Rais wa nchi kila kitu kumhusu (isipkuwa kuhusu mambo ya nyumba yake) is a public concern...
Na labda mmesahau tu..
Serikali yake kwa maagizo yake mwenyewe imeua watu wengi sana kwa namna na sababu mbalimbali. Wote hawa nao wanalilia haki. Wanamlilia Mungu alipe kisasi dhidi ya waliowaumiza au kukatisha uhai wa ndugu zao...
Kwa kifupi sana ni kuwa, mikono ya Magufuli inanuka na imetapakaa damu za watu wasio na hatia yoyote bali ni kwa sbb tu wametofautiana ama hawakubaliani na mipango na sera na mawazo yake...
Tunakumbuka vizuri sana simanzi iliyolikumba taifa mwaka 2017, mchana kweupe, katikati ya mji wa Dodoma, watu wanaoitwa hadi leo "wasiojulikana" walipomshindilia risasi nyingi mwanasiasa machachari wa upinzani Wakili na Mwanasheria Tundu Lissu....
Serikali hii hii ya Magufuli haijawahi kuchunguza wala kukamata wahalifu hawa wa maisha ya Tundu Lissu na familia yake. Huu ni ushahidi wa wazi kabisa kuwa serikali ya Magufuli ilipanga na kulitekeleza shambulio hilo....
Mimi ni Mkristo, naamini ktk kusameheana na kusahau. Aidha naamini kuwa "kisasi ni cha Mungu mwenyewe, si juu yetu wanadamu"....
Lakini naamini pia kuwa, kila dhambi ni lazima ihukumiwe. Hata Mimi au wewe unayesoma hili andiko, ukitenda dhambi ni lazima ulipe gharama yake maana imeandikwa " ....Mshahara wa dhambi ni mauti....".
Kamwe Mungu hawezi kwenda kinyume na NENO LAKE. Kila Neno la Mungu lazima litende kazi yake. Alichokisema Mungu, HUKITENDA....!;
Kwa dhambi hizi za kuumiza watu, kukatisha uhai wao (kuua), kudhulumu haki zao, nakuhakikishia kuwa, kila aliyehusika directly au indirectly ni lazima apate adhabu yake toka kwa Mungu muumba mwenyewe unless wapate NEEMA YA KUTUBIA MAKOSA YAO...
Hii sisemi Mimi. Ni maandiko matakatifu ambayo ni NENO la Mungu yanasema...
Mimi sipepesi macho, nasema moja kwa moja kuwa Rais Magufuli ni wa kwanza miongoni mwa wote...
Machozi na vilio vya walioumizwa na utawala wake vimefika kwa Mungu na Mungu ameshuka mwenyewe kuja kuwafuta Machozi kwa kila mtu kupata mshahara wake...
Mwambieni suluhu na salama yake ni TOBA YA UCHUNGU tu. Mwambieni atubu dhambi zake. Mungu wetu ni wa rehema na neema, atamsamehe na kumpa muda zaidi wa kuishi. Asipotubu, HAKIKA ATAKUFA...!!!
Awe kama Mfalme (Rais) Hezekia wa Yuda - Israeli [
Soma 2 Wafalme 20: 1 - 6] katika biblia. Alipitia wakati mgumu kama anaopitia Rais Magufuli. Aliugua karibu ya kufa. Nabii Isaya akamletea ujumbe toka kwa Mungu kumueleza sababu ya adhabu yake hiyo. Nabii alimwambia Mfalme Hezekia, kuwa Mungu anasema, rekebisha mambo yako nawe utapona...
Mfamle Hezekiah alikuwa mtu muungwana. Aliupokea ujumbe wa Mungu na yote yampasayo kufanya ili aokoke na kupona...
Akatii na kufanya sawasawa na maagizo ya Isaya mwana wa Amozi. Hezekiah akararua mavazi yake, akafanya maombi makuu....
Hakuagiza Taifa zima lifunge na kuomba kwa ajili yake kwa sababu tatizo ni lake binafsi wala siyo la taifa lote la Israel...
Mungu akayapokea maombi yake. Akamponya ugonjwa uliokuwa unamsumbua na kutishia uhai wake. Akamwingezea miaka 15 zaidi ya kuishi...
Rais Magufuli has to do the same else he will die. Kumbuka Mungu haangalii umefanya mazuri mangapi. Ukimtenda dhambi, anafuta yote. Yeye ana watu wengi sana anaoweza kuwapa jukumu la kuongoza na kutawala watu wake na wakafanya makubwa kuliko hata yeye....!!!
Mungu ampe neema ya kumjua Yesu Kristo ili amwokoe...