Ila naona kama umejaa uchungu Sana, na mahubiri yako hayaonyeshi hata chembe ya neema na upendo! Nikuulize: Je huwa unamwombea Rais wetu Magufuli kama maandiko yanavyotutaka? Maandiko yanasema usihukumu usije ukahukumiwa!
Mbaya zaidi ni kwamba hizo tuhuma unazomtuhumu ni za kusikia mitaani na wala huna ushahidi wake! Matokeo yake umeathirika moyoni na kujaa uchungu ni haitakuwa afya kwako! Ushauri wangu kwako: Usiamini maneno usiyoweza kuyathibitisha.
Sijamhukumu mtu. Sijamhukumu Rais wetu. Nimesema kweli ya Neno la Mungu kama ilivyo...
Ninamwombea Rais, ninaombea serikali yote, ninaomba kwa ajili ya kila mtu na ninaombea nchi yangu kila siku ktk maombi yangu....
Hapa tulipo tuna maombi ya siku 21 kanisani kwetu ya kufunga na kuomba kwa ajili ya nchi yetu. Masaa 12 mchana hatuli chakula wala kunywa kwa ajili ya hii. Leo J2 ni siku ya 7. Tuna siku 14 mbele....
Lakini hebu soma ukweli huu mwingine mchungu sana wa Neno la Mungu:
ISAYA 55: 8 - 9
".....maana mawazo yangu, si mawazo yenu, wala njia zengu si njia zenu, asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu..."
Kazi yetu ni kuomba. Anayejibu maombi ni Mungu muumba mwenyewe. Huwa tunaomba Rehema na Neema toka kwa Mungu ziwe juu yetu na wapendwa wetu..
Ukimwomba Mungu ili amponye/ampe afya njema Rais Magufuli, si lazima ajibu kama tutakavyo sisi. Kama ni ishu ya kiafya "determinant factor" ya uponyaji ni muhusika mwenyewe anayeombewa, kwamba, ni kwa kiasi gani amefungua mlango kuipokea neema ya uponyaji katika Yesu Kristo...
Yeye ni MUNGU WA HAKI. Hampendelei wala hawezi kunuonea mtu awaye yeyote bila kujali huyo mtu ni nani kwa sababu Mungu anasema hivi juu ya hili;
"...mshahara wa dhambi ni mauti..."
Na pengine imeandikwa;
"....Kila atendaye dhambi, hakika ATAKUFA..."
Kwa maandiko haya, Mungu hawezi kwenda kinyume na NENO LAKE. Kila alilosema atalitimiza, kila alilosema atalitenda hakika...
Dhambi inaua ndugu. Na haijalishi wewe ni nani na una nini...
Suluhisho la dhambi ni KILA MTU kukimbilia GOLGOTHA, Msalabani pa mwokozi. Hapo ndipo palipo na UZIMA...
Tunapomwombea Rais wetu John Pombe Magufuli Mungu anaweza kujibu kwa kumpelekea ujumbe wa TOBA kwa njia yoyote kama alivyojibiwa Mfalme Hezekia. Hili nalo ni jibu...
Akisikia sauti ya Bwana Mungu na kutii, ATAISHI. Sisi tunaoomba kwa ajili yake, hatuna cha zaidi cha kufanya zaidi ya kuomba. Anayejibu ni Mungu kwa kadiri ya kanuni zake na si kama vile sisi tupendavyo...!
Mungu amjalie Rais John P. Magufuli Neema ya kumjua Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu na kwa neema hiyo aokolewe kwayo.... Amina