Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Ila naona kama umejaa uchungu Sana, na mahubiri yako hayaonyeshi hata chembe ya neema na upendo! Nikuulize: Je huwa unamwombea Rais wetu Magufuli kama maandiko yanavyotutaka? Maandiko yanasema usihukumu usije ukahukumiwa!
Mbaya zaidi ni kwamba hizo tuhuma unazomtuhumu ni za kusikia mitaani na wala huna ushahidi wake! Matokeo yake umeathirika moyoni na kujaa uchungu ni haitakuwa afya kwako! Ushauri wangu kwako: Usiamini maneno usiyoweza kuyathibitisha.

Sijamhukumu mtu. Sijamhukumu Rais wetu. Nimesema kweli ya Neno la Mungu kama ilivyo...

Ninamwombea Rais, ninaombea serikali yote, ninaomba kwa ajili ya kila mtu na ninaombea nchi yangu kila siku ktk maombi yangu....

Hapa tulipo tuna maombi ya siku 21 kanisani kwetu ya kufunga na kuomba kwa ajili ya nchi yetu. Masaa 12 mchana hatuli chakula wala kunywa kwa ajili ya hii. Leo J2 ni siku ya 7. Tuna siku 14 mbele....

Lakini hebu soma ukweli huu mwingine mchungu sana wa Neno la Mungu:

ISAYA 55: 8 - 9
".....maana mawazo yangu, si mawazo yenu, wala njia zengu si njia zenu, asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu..."

Kazi yetu ni kuomba. Anayejibu maombi ni Mungu muumba mwenyewe. Huwa tunaomba Rehema na Neema toka kwa Mungu ziwe juu yetu na wapendwa wetu..

Ukimwomba Mungu ili amponye/ampe afya njema Rais Magufuli, si lazima ajibu kama tutakavyo sisi. Kama ni ishu ya kiafya "determinant factor" ya uponyaji ni muhusika mwenyewe anayeombewa, kwamba, ni kwa kiasi gani amefungua mlango kuipokea neema ya uponyaji katika Yesu Kristo...

Yeye ni MUNGU WA HAKI. Hampendelei wala hawezi kunuonea mtu awaye yeyote bila kujali huyo mtu ni nani kwa sababu Mungu anasema hivi juu ya hili;

"...mshahara wa dhambi ni mauti..."

Na pengine imeandikwa;

"....Kila atendaye dhambi, hakika ATAKUFA..."

Kwa maandiko haya, Mungu hawezi kwenda kinyume na NENO LAKE. Kila alilosema atalitimiza, kila alilosema atalitenda hakika...

Dhambi inaua ndugu. Na haijalishi wewe ni nani na una nini...

Suluhisho la dhambi ni KILA MTU kukimbilia GOLGOTHA, Msalabani pa mwokozi. Hapo ndipo palipo na UZIMA...

Tunapomwombea Rais wetu John Pombe Magufuli Mungu anaweza kujibu kwa kumpelekea ujumbe wa TOBA kwa njia yoyote kama alivyojibiwa Mfalme Hezekia. Hili nalo ni jibu...

Akisikia sauti ya Bwana Mungu na kutii, ATAISHI. Sisi tunaoomba kwa ajili yake, hatuna cha zaidi cha kufanya zaidi ya kuomba. Anayejibu ni Mungu kwa kadiri ya kanuni zake na si kama vile sisi tupendavyo...!

Mungu amjalie Rais John P. Magufuli Neema ya kumjua Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu na kwa neema hiyo aokolewe kwayo.... Amina
 
Ila naona kama umejaa uchungu Sana, na mahubiri yako hayaonyeshi hata chembe ya neema na upendo! Nikuulize: Je huwa unamwombea Rais wetu Magufuli kama maandiko yanavyotutaka? Maandiko yanasema usihukumu usije ukahukumiwa!
Mbaya zaidi ni kwamba hizo tuhuma unazomtuhumu ni za kusikia mitaani na wala huna ushahidi wake! Matokeo yake umeathirika moyoni na kujaa uchungu ni haitakuwa afya kwako! Ushauri wangu kwako: Usiamini maneno usiyoweza kuyathibitisha.
Acha unafiki.
Mtu anapigwa Risasi mchana kweupe na walinzi wa serikali wakiwepo?
Tumia akili wewe.
 
Angeanza na Shangazi zake siyo neno dogo lile lazima lipo moyoni muda utajibu
Namshangaa mtu ambaye shangazi zake waliponea chupuchupu kushikishwa adabu leo anamtetea muumiza shangazi zake. Hii siyo akili nzuri. Ila anachoongea na anavyoonekana ni kama vinapishana.

Mwili wake unaonekana kufurahi ila mdomo unatoa yasiyoendana na kinachotolewa na mwili wake. Waingereza wanasema "Facial expression", "Body language". Binafsi nimeyaelewa yaliyosemwa na Body language na facial expression.
 
Unajua Yesu alipouawa na wayahudi kisha baadae akafufuka wayahudi hawakuamini kabisa akiwemo Thoma, ilibidi sasa Yesu yeye mwenyewe baada ya kufufuka alitoka hadharani anawaita watu waliokua nae karibu akiwepo Thomasi akamwambia njoo karibu nishike na vazi langu uamini kwamba nipo hai kwa sasa.

Ninashangaa aina ya utawala wetu wa Afrika, huu ni ushamba au nini? Kwanza ni dhambi kiongozi kukaa kimya ikiwa watu ambao wamemchagua wamejawa hofu kujua yupo wapo. Kuendelea kukaa kimya ndiyo hofu kubwa zaidi kuliko kuzungumza. Na hii inauliza kwa sababu watu walizoea huko nyuma ikiwa kiongozi wa wa nchi ana tatizo, kurugenzi za mawasiliano zilikua zikitoa ufafanuzi.

Msigwa kukaa kimya ikiwa ndio idara yake ina mamlaka ya kusema kusema kuhusu kiongozi wa nchi si sawa, kama mtu ni mzima Msigwa amekaa nini kimya mpaka Waziri mkuu aseme? Waziri mkuu kusemea mskitini ni official? Anataka kugundua kitu gani?

Tumeachwa mbali sana na wanaoitwa Mabeberu kwa sababu ya ushamba wetu, kitu kidogo tu tunajifanya kizamani sana. Kusema officially mtu yupo wapi kuna ubaya gani kiwa waliomchagua wanahitaji kujua? Ukaaji kimya itatusaidia kugundua kipi chini ya jua?
 
Iv msela kaacha unga au mbona zisi niuz iz jast kompliketed sana🙄🙄🙄

Wi weitingi foo ze anaunsingi onile.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania
Yupo Anachapa Kazi, Tuwe Watulivua.
Muda Utaongea Yaani Rais Atakapooneka
Mtasema Nini Tena?
 
Unajua Yesu alipouawa na wayahudi kisha baadae akafufuka wayahudi hawakuamini kabisa akiwemo Thoma, ilibidi sasa Yesu yeye mwenyewe baada ya kufufuka alitoka hadharani anawaita watu waliokua nae karibu akiwepo Thomasi akamwambia njoo karibu nishike na vazi langu uamini kwamba nipo hai kwa sasa.

Ninashangaa aina ya utawala wetu wa Afrika, huu ni ushamba au nini? Kwanza ni dhambi kiongozi kukaa kimya ikiwa watu ambao wamemchagua wamejawa hofu kujua yupo wapo. Kuendelea kukaa kimya ndiyo hofu kubwa zaidi kuliko kuzungumza. Na hii inauliza kwa sababu watu walizoea huko nyuma ikiwa kiongozi wa wa nchi ana tatizo, kurugenzi za mawasiliano zilikua zikitoa ufafanuzi.

Msigwa kukaa kimya ikiwa ndio idara yake ina mamlaka ya kusema kusema kuhusu kiongozi wa nchi si sawa, kama mtu ni mzima Msigwa amekaa nini kimya mpaka Waziri mkuu aseme? Waziri mkuu kusemea mskitini ni official? Anataka kugundua kitu gani?

Tumeachwa mbali sana na wanaoitwa Mabeberu kwa sababu ya ushamba wetu, kitu kidogo tu tunajifanya kizamani sana. Kusema officially mtu yupo wapi kuna ubaya gani kiwa waliomchagua wanahitaji kujua? Ukaaji kimya itatusaidia kugundua kipi chini ya jua?
Yawezekana mshamba ni wewe unayedhani wananchi wote wana hofu kwa kuwa tu wewe na viazi wenzako mna hofu.

Mwanzo mlitaka tamko la serikali. Waziri mkuu kaibuka na kutoa tamko (achilia mbali viongozi wengine wa serikali waliotoa matamko yao akiwamo balozi wetu Namibia ambaye kimsingi alikuwa boss wa TISS hivyo anajua anachoongea).

Baada ya kusikia rais yuko poa nyie nyumbu mmegeuza gia mnataka ajitokeze. Serikali ndiyo inajua namna ya kuendesha mambo yake. Ucheni ujuaji, watafutieni watoto wenu ugali nyie nyumbu.
 
Maagano ya kishirikina yapo hata ndani ya serikali na tena hata katiba huyatambua kama mila na desturi za Watanzania. Ambayo ni watawala ambao ni wacha Mungu wa kweli ambao hawako vuguvugu kwa kufungamana na imani za kidini na zile za kisangoma ndio wenye kuweza kuzishinda nguvu za kuzimu.

Suala la matambiko ya tausi viungani mwa ikulu na mbio za mwenge ni mojawapo ya nguvu za kuzimu ambazo ziliwekwa ili kukilinda chama tawala na taasisi ya urais. Chaguo ni moja tu kwa utawala wa awamu hii, ama kutubu kwa dhati ili kuuondoa uovu huu, ama kuzidi kufangamana na maagano ya kishetani yaliyokwisha kufanyika.
Kweli mkuu hii habari ilishawahi kuja hapa JF:
 
Unajua Yesu alipouawa na wayahudi kisha baadae akafufuka wayahudi hawakuamini kabisa akiwemo Thoma, ilibidi sasa Yesu yeye mwenyewe baada ya kufufuka alitoka hadharani anawaita watu waliokua nae karibu akiwepo Thomasi akamwambia njoo karibu nishike na vazi langu uamini kwamba nipo hai kwa sasa.

Ninashangaa aina ya utawala wetu wa Afrika, huu ni ushamba au nini? Kwanza ni dhambi kiongozi kukaa kimya ikiwa watu ambao wamemchagua wamejawa hofu kujua yupo wapo. Kuendelea kukaa kimya ndiyo hofu kubwa zaidi kuliko kuzungumza. Na hii inauliza kwa sababu watu walizoea huko nyuma ikiwa kiongozi wa wa nchi ana tatizo, kurugenzi za mawasiliano zilikua zikitoa ufafanuzi.

Msigwa kukaa kimya ikiwa ndio idara yake ina mamlaka ya kusema kusema kuhusu kiongozi wa nchi si sawa, kama mtu ni mzima Msigwa amekaa nini kimya mpaka Waziri mkuu aseme? Waziri mkuu kusemea mskitini ni official? Anataka kugundua kitu gani?

Tumeachwa mbali sana na wanaoitwa Mabeberu kwa sababu ya ushamba wetu, kitu kidogo tu tunajifanya kizamani sana. Kusema officially mtu yupo wapi kuna ubaya gani kiwa waliomchagua wanahitaji kujua? Ukaaji kimya itatusaidia kugundua kipi chini ya jua?
Wewe ulimpigia kura Magufuli?
 
Mama Samiah akiwa kama raisi mpaka sasa hivi,aseme tu hali ya Jiwe,Watanzania tujue.Haya mambo ya kufichaficha sio sawa!
 
Ila kwa uhalisia kama Rais angekuwa katika hali kama hiyo inayosemwa ni dhahiri kungekuwa na taharuki na isingewezekana kamwe kwa waziri Mkuu kuendelea na ziara kama hizo.

I BET THE PRESIDENT IS FULLY FIT AND FINE
Unafikiri ni kwa nini
1. Hakuhudhuria virtual meeting ya viongozi wa nchi za EAC?
2. Hakuonekana kanisani jumapili tatu sasa, na hakuna clip zake za kuhuburi zinazorushwa kila jumapili?
3. Kama kweli yuko busy, ameshindwaje kutuma ujumbe binafsi kwa Taifa kwa kupitia TV au radio, ili kuwakikishia wananchi kuwa yeye ni mzima?
4. Pia kwa nini wakuu wa serikali wamachukua zaidi ya wiki kabla ya kuanza kukanusha juu ya hali ya rais?
 
Binafsi, anayesema Rais anaumwa na anayesema Rais ni mzima, Kwa kipindi hiki na kipindi chochote, kama hatumwoni hadharani, hawana tofauti ... wote wanazusha tu...
Ajabu zaidi ni kwa nini mheshimiwa, anashindwa hata kupost clip kwa tv na mtandaoni kukanusha kuwa anaumwa. Ok yuko busy basi hata clip ya dakika 2 ya kukata mzizi wa fitna inamshinda?
 
Naomba sana tena sana kwamba uvumi ulioenea kwamba Rais wetu, kioenzi cha watanzania ni mgonjwa usiwe kweli. Lakini ikidhihirika ni kweli na viongozi wakatuficha, na kwa kufanya hivyo tukakosa nafasi ya kumwombea Rais ili apone, tutawalumu sana viongozi hawa.

Kwa kweli watakuwa hawajatutendea haki. Maana sasa tunashindwa kufanya maombi kwa kitu ambacho ni uvumi.
 
Back
Top Bottom