Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Hivi siku ikajulikana Hana afya njema na wala hachapi kazi, huyu Majaliwa ataweka wapi sura yake?
 
hivi hata wewe ukiamua kupumzika hutaki mawasiliano na mtu kwa uamuzi wako mwenyewe majukumu ukawaachia wasaidizi wako nani atakutafuta acheni kiherehere yaani mnakuja kuumbuka vibaya nyau nyie
Rais ni Mtumishi wa umma! Hayo mamlaka ya kujiamulia tu kupumzika anayatoa wapi? Likizo kwa watumishi wote wa umma ni siku 28 tu kila mwaka! Na Rais amekuwa akizitumia hizo siku zake kwa mapumziko kule Chato, nk

Sasa wewe unakuja kutetea kitu ambacho hata hukielewi! Kama anaumwa, tumbiwe tu ukweli maana hakuna kitakachoharibika! Ila hii hali ya kuendelea kuficha ficha vitu, mtakuja kuumbuka tu, siku si nyingi.
 
Mnaumbuka muda si mrefu, sasa ushasema likizo au mapumziko siku 28 sasa hata 20 hazijafika unakuja kuharisha hapa hayo ni mahaba mazito mliyonayo wapinzani kwa JPM.
 
Hv jamaa wakat unandika huu UZI hukuwekewa bastola kichwan kwel?
Niwekewe bastola ili kunilazimisha nini naonyesha tu jinsi mlivyo na mahaba na mtukufu Rais JPM mlijifanya kumkataa leo hii mnatamka wazi rais wetu yuko wapi yaani aisee mnaona hata aibu lakini mlivyokuwa mnamkataa mwanzo
 
kama anachukiwa huwezi kumzungumzia iasi hicho huyu ni kipenzi cha watu ndiyo maana wapinzani wana haha tena walikuwaga wanajifanya eti hawamtambui leo hii wanamuita rais wetu yuko wapi yaani wamemkubali
Sijui kama unajua maana ya "satire" au "kejeli"
Ungekuwa unajuwa usinge andika huo upuuzi
 
ulianza lini kumpenda nawe sky maana sasa hivi ndiyo nakuona unamuita rais wetu hayo mahaba naye yameanza lini tujuze
Kuna MTU kasema anapendwa ndio maana anauliziwa Sana. Majibu hayo😁😁😁
 
Hivi mtu asipoonekana maana yake anaumwa.

Katiba inasema rais aonekane Mara ngapi kwenye public au apige Simu redioni Mara ngapi ili muda ukipita tuanze kumtafuta na kutaka aonekane?
 
Watu wanachosubiri kusikia hakipo kwa wema. Lait presida kesho akatokea hadharani basi wanaouliza hawatafarijika kama ikipigwa parapanda.

So kinachoendelea ni kejeli na unafiki. Huku moyoni watu wakitamani asirudi Jumla.

Alisikika muuza Kibua akisema.
 
Namba moja ni Madelu system Yule kijana ni nyoka Magufuli akiendelea kumkumbatia atavuna mabua.
 
Kweli kabisa aiseeee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…