Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Kiswaswadu mwongo sana mbaya zaidi anasema uongo akiwa msikitini
Eti Kiswaswandu😁😁🤣🤣😅,dah watu mna maneno jamani,kweli inatakiwa ukiwa mwanasiasa hutakiwi kuwa na hasira,maana na kazi yangu hii halafu uniite hilo jina wallah zitawaka ngumi sio za nchi hii...
 
Aise,uovu ni kitu kibaya sana,unafiki ni mbaya sana.Yaani jamaa macho makavu kabisa,wala hajisikii vibaya hata kidogo,anatafuna uketo tu.Duh!So hawa ndio wanaotaka tuwaamini kwenye zengwe la DP World.Eti mtuamini,tuwaamini ninyi Mungu.Kama mlitudanganya kwenye kifo cha Magufuli,hamna ukomo wa kudanganya ninyi,we cannot believe you in anything.
 
"Kuanzia Juzi hata leo asubuhi nimeona Watanzania wenzetu wenye husda, tena hawako ndani ya Nchi wako huko, wanashawishi Vyombo vya Kimataifa viseme ‘Rais wa Tanzania anaumwa, kajifungia’, tena hawako hapa, wapo huko, tulioko ndani tuko kimya, ni husda”-Waziri Mkuu Majaliwa akiwa Njombe leo

"Watanzania mtulie uongozi wenu upo,Rais Magufuli anaendelea vizuri, kumzushia ugonjwa ni chuki tu, inawasaidia nini?, ‘atoke’, atoke aende wapi?, ‘aje’ aje afanye nini?, umeshamkuta Rais siku moja anazurura kariakoo?, Rais ana mipango yake ya kazi sio Mtu wa kuzurura”-MAJALIWA

"Juzi tu Rais alikuwa Chato akatoka akaenda Kahama, Tabora, Dodoma, akarudi DSM, juzi kaapisha mnataka tena azunguke Nchi nzima, sisi tunafanya nini?, nini umuhimu wa kuwa na Wasaidizi!, azunguke yeye tena Nchi nzima kweli?”- MAJALIWA

#MillardAyoUPDATES

Mie siongezi chochote....
 

Attachments

  • IMG-20231012-WA0172.jpg
    38 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…