Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Kama mlisema corona hamna kwani mna shindwa nini kusema Jiwe ni mzima?
Subirini arudishwe kwenye box ndiyo mtuambie ana afya njema.
 

Hivi nyinyi mnao mbishia hata Waziri mkuu mna lengo gani?
 
Kwanza kabisa ni kurejesha sio kulejesha, taarifa na sio taatifa, ikulu sio ikuru. Hivi ulipata wapi elimu yako?
Pili, hivi wewe ukiwacha mapenzi yako ya ccm, tuseme uko sasa jembe amesingiziwa kuwa anaumwa sasa kwa nini anashindwa kuja hadharani kukanusha? Hivi wewe rais wako hajahudhuria mkutano wa EAC, hajaonekana kanisani (ambako anakwenda kila jumapili bila kukosa) jumapili mbili, hajahudhuria hafla yeyote ile kwa wiki tatu (si kawaida yake) na bado unaona kuwa ni kosa watu kuuliza cha mno?

Tumia bongo lako! utabaki hadi lini kufanya jinga la mji?
 
Mjomba wako ni tapeli mchunguze vizuri utagundua
Mjomba wangu ni afisa kipenyo mwandamizi kuna jambo zito kaniambia.

Waziri mkuu kama anabisha amwambie Magufuli anyooshe kidole juu ama afanye kama anajikuna halafu apigwe picha.
 
Angempigia Hapo hapo kumjulia hali. Mbona kwenye kampeni walikuwa wakiongea mubashara.
Kauli ya leo imetoa taarifa Rais anaumwa. Siku wakija kusema anaumwa tujue kuwa atakuwa amefariki.
 
Very clear bila hata chenga, mmepata picha kamili kuna chuki kubwa dhidi ya serikali yetu. Mnaweza mkadhania mtego wenu kujua nani anawachukia umefanikiwa lakini ukweli utabaki kuwa mnachukiwa.

Mnachukiwa na waliojeruhiwa na vyombo vya dola, walionyimwa haki ya nyongeza ya mishahara, wapo wanaodai kuporwa uchaguzi. Wapo ambao ndugu zao wameuliwa bila makosa. Wapo ambao wamebaki kuwa vilema.

Ukweli ni kuwa mnachukiwa tena chuki mbaya sana. Msidhani ni chuki za walio nje ya nchi tu. Bali wengi walio ndani hapa Tanzania wanawachukia.

Sidhani kama mna muda wa kujirekebisha, labda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…