Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo Asubuhi wakati nakuja huku nimeongea nae kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli?. Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salam.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.

Chanzo: Jamvi la Habari

Kama ni kweli kwanini Raisi ,wenyewe asitoke na kusimama ikulu mpaka tunafika huku. Wanataka wamlete akipata nafuu kama vile hajaondoka wakati waganga wa Nairobi ndiyo walisema yupo pale. Huu ni utamaduni wa uongo uliopo kwenye uongozi huu. Haya ni mapungufu makubwa ya serikali hii
 
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo Asubuhi wakati nakuja huku nimeongea nae kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli?. Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salam.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.

Chanzo: Jamvi la Habari
Sawa kuna maziko karibuni we hope tutamuona na atatupigia push ups.
 
Mungu mwepushe na Hilo janga wanalomwombea wabaya wa nchi ili akamilishe mazuri aliyoanza ili Tanzania iwe Kama Amsterdam, Tundu akimbilie uhamishoni huku Tanzania palipokuwa nchi yake ya awali
Bora kwanza ujiombee dua mwenyewe kwanza, uwe na uwezo wa kutambua la kweli na la uongo, uweze kufahamu ni kwa nini wanasiasa wote duniani wanajulikana kwa ujuzi wa kusema uongo. Siasa inaitwa si hasha kwa sababu hiyo!!!!
 
Wanajamii forum mbona ni jambo jema kubishana kwa hoja kulikokuanza kutukanana sisi wote humu ni familia 1 kwanini matusi na kebehi zisizo na maana?tujadili hoja mwenye kielelezo anakiweka tunakijadili hapa kisha tunasonga mbele &asanteni
 
Sasa serikali hapa ndio wanaonyesha kupoteana, ilitakiwa kama waliamua kukaa kimya basi wangekaa kimya wala wasishindane na watu wa mitandaoni.

Ila kwa hili la kuanza kumjibia Mh. Rais watu wataanza kuunganisha doti. Cha msingi waendelee kukaka kimya huku wakitimiza majukumu yao ya kila siku.
Kwani mangapi mlishasema na mwisho anatoka mzima na mnakosa kulejesha taarifa zenu?
Wote mnao ongea hamna uwezo wa kwenda ikuru ila mnajifanya mna taatifa za mtu wa ikuru kwa mtizamo wenu.

Kama mnampenda basi anzeni kumpa heshima yake na sio vijembe vyenu.
 
Kifo unachomuombea mwenzio chaweza kukurudia mwenyewe

Maendeleo hayana vyama
Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu John Pombe Joseph Magufuli [emoji173][emoji1241][emoji106][emoji111][emoji120]
Mbona watu waliambiwa wapinzani ndio walichelewesha maendeleo na kwamba wasipochagua CCM Tunduma waliambiwa maji hawatapelekewa..
 
Serikali ipo na inafanya kazi,Mtu aumwe au asiumwe bado kila MTANZANIA ana wajibu wa kufanya kazi na kulinda maslahi ya Taifa hili,haina haja ya kuwa na akili za kijinga kujifanya tunahoji kama vile mikakati na dira zake za maendeleo tunazitambua na kuziwajibikia..Kila jambo la Kitaifa afanyalo Rais wa Jamhuri ni kwa ajili yetu sote..kwani tunashindana na nani? Baba akiombwa na mwanaye Mkate sidhani kama atampatia Ng'e..
Mh.JPM usihangaike ata kuwajibu watu hawa wanahitaji waombewe wapate kurudia utimamu..
 
Jamani hebu tumwombee tuu. Yesu alisema wapendeni adui zenu
 
Back
Top Bottom