Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"...
Hivi ni kwa nini inakuwa nongwa wananchi wanapoonyesha kummis mpendwa wao? Wanataka kumwona awasalimie, wewe Majaliwa unasema hatoki ndani anashughulika na mafaili, sasa mbona mnakuwa wakali? Kwani ni kosa kummis na kumuulizia mpendwa wako usipomwona kwa muda mrefu? Tunashukuru kama ameanza kupata nafuu.
 
Wameshaharibu na wachokonozi wanafurahi kuwa ujumbe umefika. Ni heri wangekaa kimya. Kwahiyo Katelefoni ametumwa kuvunja ukimya badala ya Gerson Msigwa?
 
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"....
Ungejua usivyopendwa na huyo unayemsemea hungenyanyua mdomo. Uliponea kwenye tundu la sindano kutumbuliwa ujue!
 
Ni kweli. Ila ndugu yangu haya mambo ya disinformation kuna watu wanasomea kabisa. Kuna makachero wanasomea kwa kina. Na ninavyoiona Tanzania ya sasa hata kama hawana mtaalam huko kitengo basi wanaweza ku-outsource kazi kwa watu kutoka nchi zilizoendelea.

Unajua nchi zilizoendelea mashushushu wale wakali wakistaafu huwa wanaanzisha kampuni kwa ajili ya kuchukuwa contract kwa malipo. Hapo ulipo sasa hivi kama una mpunga mrefu unaweza kulindwa na wastaafu wa Seal Team kutoka vikosi kama kile kilichomuua Osama.
 
Majungu ya watanzania yako hivi, akionekana sana kwenye Tv na miradi mbalimbali wanasema kwanini Rais mzima anashinda anafanya kazi ambazo wasaidizi wake walitakiwa afanye? anapenda kuonekana kwenye TV peke yake wakati huo kazuia mikutano ya siasa, tukija jungu no 2 amemua apumzike afanye kazi ambazo wengi wanasema anatakiwa fanye kuelekeza tu akiwa ametulia ofsini wamekuja na issue ya Mbona Rais haonekani? tunaomba ajitokeze tumuone, aiii Tz watu hubadilika kama kinyonga any time yaani usishangae hiyo ndio bongo.

Any way mimi sikatai Rais kuwa mgonjwa maana hata yeye ni binadamu, anaweza ugua na lolote linaweza tokea kwa kila binadamu, cha msingi kama ni mzima na anaendelea na kazi zake ni jambo la kheri, kama ni mgonjwa tumtakie ugua pole na apone mapema, hili sio swala la kisiasa tupige kelele nyingi wakati huo serikali ipo na kazi za kiserikali zinaendelea, pia tusiwe wepesi wakuhukumu moja kwa moja kuwa anaumwa corona , kumbe anaweza kuwa na hata vidonda tu mwilini au kapigwa tu na mkewe jicho limevimba na akapumzika nyumbani kwake.
 
Nampongeza sana Ndugu Waziri MKUU kwa kuwajibu wale Watu Ambao hata sisi tumeshangaa haya Mahaba na Chuma chetu yameanza lini?

Naanza kuamini kwamba Mzee Maalim Seif Ndiye Alikua Mshindani wa Kweli katika nchi yetu hawa wengine ni Sinematu.
 
Nampongeza sana Ndugu Waziri MKUU kwa kuwajibu wale Watu Ambao hata sisi tumeshangaa haya Mahaba na Chuma chetu yameanza lini?

Naanza kuamini kwamba Mzee Maalim Seif Ndiye Alikua Mshindani wa Kweli katika nchi yetu hawa wengine ni Sinematu.
Utoto utoto tu watu wazima.
Hii imenikera kusema kweli.
Mwanzoni nililikuwa natetea kwa kujua ni issue ya kawaida lakini sasa hii si kawaida jamani..
Huu ni utoto unaoendelea.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom